Toyota Brevis zina nini cha ziada?

Toyota Brevis zina nini cha ziada?

altezza gari ya mashindano bana sio ya starehe kama brevis, mark x na grand... altezza unaweza piga drift na turning za kutosha kama subaru lkn huwezi fanya ujinga huu na mark x , grand au brevis sio nyepesi kufanya mambo haya.. toyota altezza habari ya mujini....

Mkuu kwanini usiweze piga drift na mark X ??? Kuna watu wanapiga drift na Hardtop landcrusier vizuri tu
 
Wajeru wanatoa gari za uhakika, ni kweli unayosemayo, ukitumia right parts ata kama utaingia gharama lkn utadumu nayo, lakini sijui utie oil filter ya buku 5, gari yenyewe itanuna na kuanza kukutia mashoti.

Halafu bimmer kama ina warranty ndo utaenjoy hasa. Bro wangu alikua na bimmer 2008 kipindi icho, ikamsumbua, yaani kitu unawacall kwenye dashboard ya gari wanajua ulipo na wanakufata apo apo kukutengezea gari na sio uwafate wewe, tena kama ipo na warranty inasumbua unapewa service bure ya kutengezewa (sio kwa matatizo ulosababisha wewe lakini) na kama itachukua muda kutwngezewa gari yako basi unapewa jengine uzurure nalo mpaka yako itakapokuwa fixed. Ndo mana nasema hawa bmw gari zao hazipo over priced.... Mi nkiwa na hela mi mwenyewe nahamia bmw, wacha saiv nibangaize na ka lexus is200 in the mean time :-D

Mkuu hii Huduma unaipata hapa bongo au unaongelea wapi ???
 
Hiyo brevis ina match na gari zimeingia sana mjini sasa hivi ni progress nzuri sana zina uwezo kama wa benz na system yake ni kama ya benz wajapan wamecopy

Sio benz, sema brevis.....unajua brevis na progress ni mtu na mdogo wake, sawa na kusema gx100 na gx110.....mkuu ukitumia benz ndio utaona umeendesha gari siku hiyo na utaona utofauti mkubwa na hiyo progress
 
naombeni wasifu wa mark x compared to other cars mostly hizi zisizokula sana mafuta

Comfortable
Wishbone mbele na nyuma zinaifanya itulie sana road.

Inayo nafasi kubwa ndani na head room yakutosha.

Consumption nzuri, nadhani nayo lita 9 inaenda kilometa 100 japo ni V6

Ni gari nzuri kwakweli hila kama umezoea passo na vitz au fun cargo sikushauri uingie huku kichwa kichwa, unatakiwa uende kwa stage anzia kwenye gx110 then panda huku juu
 
Ulishawahi kuona matairi ya rav4 jinsi yanavyokuwa slanted?

Hule ni mfumo na sio tatizo, gari nyingi zinazotumia wishbone nyuma huwa nazo zinakua hivyo especially zikiwa zimebeba na mzigo, hiyo inasaidia kuleta balance ndio maana utaona Rav 4 inakimbia mpaka kwenye corner unalala tu tofauti na mwenye landcruiser hardtop au defender tdi
 
Brevis ni mashine man nitakutafutia drag race ya Brevis na Mark X tumalize hubishi, lakin jua kama Mark x nizito sana tofaut na Brevis amabyo ni nyepesi, alafu kuhusu horsepower unakuta gari ina horsepower kubwa sana lakin hawezi mpata mwenye horsepower dongo,kuhusu gari kukimbia siyo horsepower tu kuna vitu vingi sana kama uzito wa gari,gear box yake ipoje na vingine vingi, kuhusu horse power tafuta gari linaitwa nissani gtr unakuta linahorsepower 650 lakini gari zinakujana horsepower 800 mpaka 900 hawakamati gtr, ndio gtr inapendawa sana usa na Europe ingawa ni gari ya japan

Mkuu gari zote ni nzito kwanza uzito wake nadhani brevis ni 1520kg na Mark X ni 1530kg kama sijasahau......utofauti unakuja kuwa mark X ni V-engine while brevis ni Straight engine....nadhani unajua shughuli ya V-engine kama haujui angalia gari zote zinazokimbia duniani ni V-engine hili ziwe zinapokea fasta, hila brevis yako ni Straight engine inapokea sawa hila sio kivile ndio maana brevis ya 250i hata ukimbie vipi huwa kwenye gps inasoma imeenda sana speed 182km/h, hila mark X kwenye gps speed meter huwa inasoma mpaka 235km/h.....na brevis inayokimbia ambayo inaweza kuisumbua mark x ni hile brevis ya CC 2900.
 
Inaweza kuifikia toyota camry mkuu
 
Nimechelewa ila nipo mark x ni gar nzur ina auto na manual brevis ina auto tuu na progress ina auto mark x ni nyepes sana kwenye gear na hata kufika 180 ni ndan ya dakika chache ata 2 kama road ni nzuri niliwah endesha mark x dar tarme tukifukuzana na bmw x5 nilienda nayo sambamba
 
Bei inategemeana kama wataka brand new, used both Bongo and nje ya nchi.. Nyingi zinazokuja Bongo ni used tayari, si unajua wenzetu matumizi yao kidogo yako poa hata kama used inaonekana iko powa tu. Tatizo kubwa hizi brand mfano kuipata Brevis latest brand kwa maisha yetu ni ngumu. Ndio maana tunabase za kati ya 2001 or 2003.

Yangu nilichukua million 13 Japanese used milage 68000, Saa hizi hata million 11 unapata ila kama mwoga wa maisha kama wengine hao hii gari inanyonya wese hatari! Kwa spidi utapenda, Six Valve hata new force utampumulia kwa nyuma.
new force sawa,ila sio happy nation(mtukutu)710 dar-mwanza
 
Nimechelewa ila nipo mark x ni gar nzur ina auto na manual brevis ina auto tuu na progress ina auto mark x ni nyepes sana kwenye gear na hata kufika 180 ni ndan ya dakika chache ata 2 kama road ni nzuri niliwah endesha mark x dar tarme tukifukuzana na bmw x5 nilienda nayo sambamba

Mwenye X5 atakua alikua.anataka company yako labda, hila angesema adidimize kidogo tu basi nadhani wewe ungeingia moro yeye muda huo anaingia gairo 😀😀😀
 
Camry se ndo inamwendo kias ila kwa mark x itasubiri sana

Inategemeana na model, kama ni model za XV40 zinazoanzia 2007 mpaka 2010 basi mark X yako itasubiri sana hapo....maana kuna camry hybrid 3.5L V6 hapo hiyo level yake labda toyota crown athlete kwa mbali.....hila kama ni camry XV30 series kushuka chini huko sawa mark X atakua mbabe
 
Nimechelewa ila nipo mark x ni gar nzur ina auto na manual brevis ina auto tuu na progress ina auto mark x ni nyepes sana kwenye gear na hata kufika 180 ni ndan ya dakika chache ata 2 kama road ni nzuri niliwah endesha mark x dar tarme tukifukuzana na bmw x5 nilienda nayo sambamba

Ulitoboa dar-tarime?
 
Mi nawashangaa mkisema utawapumulia mabasi kwa nyuma, hivi, hata nikiwa na gx100 yangu, kuna basi gani la kucheza mbele yangu, ile ni machine bhana sema sijawahi kupata ligi ya brevis, mark x au alteeza

Yemen's kiongozi mm nina 110 hayo mabasi nayapita kama yamesimama, na hizi tochi za skuizi utakimbilia wapi
 
Mi nawashangaa mkisema utawapumulia mabasi kwa nyuma, hivi, hata nikiwa na gx100 yangu, kuna basi gani la kucheza mbele yangu, ile ni machine bhana sema sijawahi kupata ligi ya brevis, mark x au alteeza

Hapo umesema kiongozi mm nina 110 hayo mabasi nayapita kama yamesimama, na hizi tochi za skuizi utakimbilia wapi
 
Back
Top Bottom