Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Nimepata hamasa ya kufanya hichi kilimo cha nyanya. Ningependa kujua kama nyanya ili kustawi zinahitaji udongo wa aina gani? Eneo kama Kibaha is it favourable?

Kwa mbegu hii unaweza panda nyanya na zikastawwi maeneo yote katika nchi hii. Mfano hilo shamba langu kwenye hiyo video hapo juu liko kibaha. Kwa wale walioko dar udongo wa wa dar na kibaha ni sawa tu kwa kilimo cha kisasa
 
Hamna kitu hapo longo longo tu tuoneshe shamba bana aah dissapointing,wewe unatangaza biashara ya nyanya sio kumsaidia mkulima

Kaka hasira za nini sasa. kama vile una stress zinakusumbua sana maana from nowhere tu huwezi andika hivyo. Hiyo ndio effect ya kumpa mtu nafasi ya free ya kujieleza kwa mtu aliyekuwa kwa akinyimwa hiyo fursa na wazazi wake kwa miaka. Kwani umepiga simu ukakataliwa kuja kuangalia shamba? mbona watu wengi tu washakuja kwenye shambalangu au unatafuta tu sababu ya mimi na wewe tujibizane hapa na nadhani utaendelea kuijibu meseji hii ili kuendeleza majibizano kati yangu mimi na wewe na wewe unafahamu ndani yako nachoongea ni ukweli
 
Jamani ningependa kuomba kuwa km mtu unaishu yoyote ni vizuri ukatumia tu lugha nzuri tu kujieleza kila mtu atakuelewa na mi naamini kabisa watu wengi humu ndani ni wastaarabu wasingependa lugha kakasi. Mi niko tayari kusaidia watu ila wote tusaidiane. Watu wengi wamefaidika kutokana na mimi so tusaidianeni ili wote tufaidikie ili tusongeshe maendeleo ya vijana wetu nchini
 
Unajua mi najaribu kusaidia kadri iwezekanavyo ndio maana mtu akipata haya mafunzo haya ya greenhouse na kilimo wazi anapata mafunzo mengine bure ya miradi niliyokuwa nafanya zamani pamoja na rafiki zangu km vile kutengeneza sabuni, perfume, losheni, chaki, ice cream km za azam, wine, mafuta ya nazi nk bure ili kumwezesha kijana awe na fursa kubwa ya kuweza kufanya kitu chochote ili asikae tu. Magufuli wala lowasa hawataweka pesa mifukoni mwako ila ni wewe tu.
 
Mkuu Biashara 2000.
Ukiwa na shamba la greenhouse la 8×15 ambalo approximate yake ni miche 400. Unaweza ukavuna ndoo au tenga ngapi za nyanya kwa mwezi au kwa wiki.???

Kwa utafiti nilio fanya tenga moja ni sawa na ndoo tatu.
 
Kwanza kabisa nadhani aliyekwambia gh hiyo inakaa miche mia nne amekudanganya. Huwa inakaa miche 300 ikiwa imejaa. Inategemea mbegu gani unatumia, km unatumia km hii yangu unapata ndo moja na nusu kwa mwezi ktk mche mmoja. 1.5 x 300 ni kilo 450 kwa mwezi x miezi nane ni kilo 3600
 
Mkuu Biashara 2000.
Ukiwa na shamba la greenhouse la 8×15 ambalo approximate yake ni miche 400. Unaweza ukavuna ndoo au tenga ngapi za nyanya kwa mwezi au kwa wiki.???

Kwa utafiti nilio fanya tenga moja ni sawa na ndoo tatu.

Shamba lako la gh liko wapi?
 
Mkuu bado sijawa na shamba ila nipo kwenye maandalizi ya kupata shamba na kufanya kilimo hiki.

Nategemea kupata shamba kibaha miembe saba.
 
Mkuu bado sijawa na shamba ila nipo kwenye maandalizi ya kupata shamba na kufanya kilimo hiki.

Nategemea kupata shamba kibaha miembe saba.

Miembe saba ni eneo zuri sana hasa km unataka kuchimba na kisima ktk eneo lako maana kuna mtu aliniambia kuwa ktk maeneo hayo hadi mlandizi kuna maji ya kutosha
 
Nimekuwa nikipokea simu nyingi sana watu wakiulizia kuhusu ule mfano niliotoa hapo juu kuhusu ni jinsi gani unaweza pata laki saba kwa mwezi. Swali hasa limekuwa likielekezwa kwenye mtaji. Wanaulizia ni mtaji kiasi gani utauhitaji wakati unaanza. Kama eneo lako ushafanya utaratibu wa kupata maji tuseme hauna maji ktk eneo lako ia unaletewa na mkokoteni na kuyahifadhi kwenye pipa, Zaidi ya hapo utahitaji sh. 150,000 ambayo watu wengi wanaweza kuimudu
 
nikiwa na water pump mkuu itanigarim kiasi gani cha ziada ili kukamilish kilimo hicho
 
Back
Top Bottom