Top ten yangu kwa uvivu

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,360
Haya ni mambo 10 ya kivivu zaidi kuwahi kuyafanya tokea nizaliwe

10. Nikiwa na miaka 9 au 10 nimewahi kulala bafuni baada kuona uvivu kwenda chumbani baada ya kumaliza kupiga mswaki

9. Niliwahi kupitiliza na daladala kituoni hadi mwisho baada ya kuona uvivu kuamka kwenye siti. Nilitakiwa kushuka Makonde nikapitiliza hadi Tegeta ilikuwa saa saba usiku nikakosa gari ya kurudi nikalala stendi hadi saa kumi na moja.

8. Nimewahi kulala kwenye mtihani wa taifa wa form two kwa saa zima, mtihani ulikuwa wa saa moja na dakika 15. Ulikuwa ni mtihani wa French na nilikuwa nauchukulia ni mtihani mwepesi sana, baada kuamka nilishindwa kujibu hata swali moja. Nilipata F ingawa nilikuwa naongoza darasani.

7. Niliwahi kunywa dawa ya kikohozi ( mkojo wa punda ) chupa nzima ili nisisumbuliwe kunywa kila siku hadi iishe. Nililewa karibia siku tatu mfululizo ( usiige hii sio pombe)

6. Niliwahi kuzimia kwa dakika kama mbili nilipoanguka nikiwa nacheza mpira, nilipoamka nikagundua nimebebwa nilirudi kuzimia ili waendelee kunibeba. Mwalimu aliogopa nikapelekwa hospitali wakaniweka chini ya uangalizi kwa siku tatu (shenzi nilitamani kusema ukweli)

5. Nimewahi kugeuza boxer nje ndani baada kuivaa kwa siku sita mfulululizo, niliona uvivu kuifua nikaamua kuigeza nje ndani kupunguza makali.

4. Nimewahi kupiga simu kwa mmiliki wa bar ili amuite mhudumu arudi kwenye meza yetu ili tubadilishe oda, mhudumu alikuwa kaunta kama mita nne hivi.

3. Hii imetokea juzi tu, nimevunja sahani kama sita hivi ili wife asizikute chafu baada kuzitumia alipokuwa kasafiri

2. Niliwahi kufunga TV kwenye ceiling ili niweze kuangalia nikiwa nimelala, nilipogundua napitwa na baadhi ya matukio nikaamua niongeze TV kwenye kila angle mpya ninayogeukia, sasa hivi tuna TV nane chumbani na zote zime connectiwa kuonesha kitu kimoja. Wife anatafuta therapist anadhani nahitaji msaada.

1. Hii ndio inaniuma zaidi, hadi leo officially natambulika kwa jina la mdogo wangu baada ya kuona uvivu kumrekebisha mwalimu wangu aliyekuwa ananifanani na mdogo wangu. Hii imesababisha nibadilishe documents zote zifanane na majina yangu ya kwenye vyeti vya shule.

Unadhani kuna mtu mvivu kuliko mimi hapa Afrika mashariki na kati?
 
Jaribu siku moja kajipumzishe relini treni itakupisha tu usijali.

Unaweza kudhani ni joke, ila kuna jamaa mmoja huko station ya Wami aliwahi kugongwa na treni akiwa amejipumzisha relini. Huyu bwana hakufa ila ana ulemavu wa maisha.
 
ungepost hewa ungeingia guiness,,
ila umetisha

Mkuu Guiness kule ni habari nyingine kabisa, siwezi hata kutia mguu. Hapa hapa bongo kuna watu ni noma. Jirani yangu alimuingiza mtoto kwenye Oven kwa kuona uvivu kutafuta taulo. Unadhani naweza kumfikia huyu?
 
Ah kumbe ndie wewe ,uliyeona uvivu kunifumania ukaniacha niondoke mdogo mdogo? endelea na uvivi wako si tunafaidi !
 
Mkuu nyie mkiendaga jela inakua shida sana unaskia mtu anakupapasa unaona uvivu tu......

Wewe ukipapaswa huwa unafanyaje? Na huwa unapapaswa mara ngapi kwa wiki? Na wanaokupapasa ni kina nani?
 
Duuh! We naeeee.... Boxer siku sita?!!!

Hii zamani sana kabla sijanunua mtu wa kunichagulia boxer ya kuvaa kila siku na ndio mhusika mkuu kuhakikisha naivua kila siku.
 
Haya ni mambo 10 ya kivivu zaidi kuwahi kuyafanya tokea nizaliwe

10. Nikiwa na miaka 9 au 10 nimewahi kulala bafuni baada kuona uvivu kwenda chumbani baada ya kumaliza kupiga mswaki

9. Niliwahi kupitiliza na daladala kituoni hadi mwisho baada ya kuona uvivu kuamka kwenye siti. Nilitakiwa kushuka Makonde nikapitiliza hadi Tegeta ilikuwa saa saba usiku nikakosa gari ya kurudi nikalala stendi hadi saa kumi na moja.

8. Nimewahi kulala kwenye mtihani wa taifa wa form two kwa saa zima, mtihani ulikuwa wa saa moja na dakika 15. Ulikuwa ni mtihani wa French na nilikuwa nauchukulia ni mtihani mwepesi sana, baada kuamka nilishindwa kujibu hata swali moja. Nilipata F ingawa nilikuwa naongoza darasani.

7. Niliwahi kunywa dawa ya kikohozi ( mkojo wa punda ) chupa nzima ili nisisumbuliwe kunywa kila siku hadi iishe. Nililewa karibia siku tatu mfululizo ( usiige hii sio pombe)

6. Niliwahi kuzimia kwa dakika kama mbili nilipoanguka nikiwa nacheza mpira, nilipoamka nikagundua nimebebwa nilirudi kuzimia ili waendelee kunibeba. Mwalimu aliogopa nikapelekwa hospitali wakaniweka chini ya uangalizi kwa siku tatu (shenzi nilitamani kusema ukweli)

5. Nimewahi kugeuza boxer nje ndani baada kuivaa kwa siku sita mfulululizo, niliona uvivu kuifua nikaamua kuigeza nje ndani kupunguza makali.

4. Nimewahi kupiga simu kwa mmiliki wa bar ili amuite mhudumu arudi kwenye meza yetu ili tubadilishe oda, mhudumu alikuwa kaunta kama mita nne hivi.

3. Hii imetokea juzi tu, nimevunja sahani kama sita hivi ili wife asizikute chafu baada kuzitumia alipokuwa kasafiri

2. Niliwahi kufunga TV kwenye ceiling ili niweze kuangalia nikiwa nimelala, nilipogundua napitwa na baadhi ya matukio nikaamua niongeze TV kwenye kila angle mpya ninayogeukia, sasa hivi tuna TV nane chumbani na zote zime connectiwa kuonesha kitu kimoja. Wife anatafuta therapist anadhani nahitaji msaada.

1. Hii ndio inaniuma zaidi, hadi leo officially natambulika kwa jina la mdogo wangu baada ya kuona uvivu kumrekebisha mwalimu wangu aliyekuwa ananifanani na mdogo wangu. Hii imesababisha nibadilishe documents zote zifanane na majina yangu ya kwenye vyeti vya shule.

Unadhani kuna mtu mvivu kuliko mimi hapa Afrika mashariki na kati?

Nimeona uvivu kusoma
 
Back
Top Bottom