Top ten yangu kwa uvivu

Top ten yangu kwa uvivu

Hii zamani sana kabla sijanunua mtu wa kunichagulia boxer ya kuvaa kila siku na ndio mhusika mkuu kuhakikisha naivua kila siku.

Natumai umebadilika sasa....
 
Ha ha ha haaah,,,,,,,,,wewe nadhani mpaka sasa bado ni mvivu.
 
Mkuu jaribu kua mvivu kwenye Kula au haja kubwa
 
Mkuu jaribu kua mvivu kwenye Kula au haja kubwa

Mkuu umenikumbusha kitu niliwahi kunya ofisini kwa headmaster baadaya kuona uvivu kwenda chooni, nilikamatwa na mlinzi ilibidi kumhonga elfu thelathini asiuze news.
 
Dear Honestly Hii si bure bali ni Pepo sugu...if its true what you wrote definetly you need a serious help .. And the person will cast out your demons must be Fasting for 40 days with prayers.. . Uwii God help us.. Mkeo ana moyo..duuh.. Thanks..
 
Haya ni mambo 10 ya kivivu zaidi kuwahi kuyafanya tokea nizaliwe

10. Nikiwa na miaka 9 au 10 nimewahi kulala bafuni baada kuona uvivu kwenda chumbani baada ya kumaliza kupiga mswaki

9. Niliwahi kupitiliza na daladala kituoni hadi mwisho baada ya kuona uvivu kuamka kwenye siti. Nilitakiwa kushuka Makonde nikapitiliza hadi Tegeta ilikuwa saa saba usiku nikakosa gari ya kurudi nikalala stendi hadi saa kumi na moja.

8. Nimewahi kulala kwenye mtihani wa taifa wa form two kwa saa zima, mtihani ulikuwa wa saa moja na dakika 15. Ulikuwa ni mtihani wa French na nilikuwa nauchukulia ni mtihani mwepesi sana, baada kuamka nilishindwa kujibu hata swali moja. Nilipata F ingawa nilikuwa naongoza darasani.

7. Niliwahi kunywa dawa ya kikohozi ( mkojo wa punda ) chupa nzima ili nisisumbuliwe kunywa kila siku hadi iishe. Nililewa karibia siku tatu mfululizo ( usiige hii sio pombe)

6. Niliwahi kuzimia kwa dakika kama mbili nilipoanguka nikiwa nacheza mpira, nilipoamka nikagundua nimebebwa nilirudi kuzimia ili waendelee kunibeba. Mwalimu aliogopa nikapelekwa hospitali wakaniweka chini ya uangalizi kwa siku tatu (shenzi nilitamani kusema ukweli)

5. Nimewahi kugeuza boxer nje ndani baada kuivaa kwa siku sita mfulululizo, niliona uvivu kuifua nikaamua kuigeza nje ndani kupunguza makali.

4. Nimewahi kupiga simu kwa mmiliki wa bar ili amuite mhudumu arudi kwenye meza yetu ili tubadilishe oda, mhudumu alikuwa kaunta kama mita nne hivi.

3. Hii imetokea juzi tu, nimevunja sahani kama sita hivi ili wife asizikute chafu baada kuzitumia alipokuwa kasafiri

2. Niliwahi kufunga TV kwenye ceiling ili niweze kuangalia nikiwa nimelala, nilipogundua napitwa na baadhi ya matukio nikaamua niongeze TV kwenye kila angle mpya ninayogeukia, sasa hivi tuna TV nane chumbani na zote zime connectiwa kuonesha kitu kimoja. Wife anatafuta therapist anadhani nahitaji msaada.

1. Hii ndio inaniuma zaidi, hadi leo officially natambulika kwa jina la mdogo wangu baada ya kuona uvivu kumrekebisha mwalimu wangu aliyekuwa ananifanani na mdogo wangu. Hii imesababisha nibadilishe documents zote zifanane na majina yangu ya kwenye vyeti vya shule.

Unadhani kuna mtu mvivu kuliko mimi hapa Afrika mashariki na kati?

Ungekuwa mvivu kwa kiasi hicho usingeweza kuandika habari ndefu kiasi hiki....hujavunja rekodi wala nn, ila asante kwa kuchangamsha jukwaa.
 
Dear Honestly Hii si bure bali ni Pepo sugu...if its true what you wrote definetly you need a serious help .. And the person will cast out your demons must be Fasting for 40 days with prayers.. . Uwii God help us.. Mkeo ana moyo..duuh.. Thanks..

teh teh teh...nimeona uvivu kucheka.,nimebaki natabasamu tu!
...thanks!
 
yani hapo ni zaidi ya uvivu.
hata kwenye record ya dunia umepita kiwango.
 
TV nane? Hicho chumba ni zaidi ya ukumbi wa Disko au bar.Sipati picha mandhari yake inavyokua usiku.
 
TV nane? Hicho chumba ni zaidi ya ukumbi wa Disko au bar.Sipati picha mandhari yake inavyokua usiku.

Mkuu umeufumua uzi wa zamani, sasa nikihojiwa kwa upotevu wa makontena utajibu.
 
Back
Top Bottom