ram
Platinum Member
- Oct 5, 2007
- 9,385
- 8,645
Kuna mbunge anaitwa hili jina, huyu nadhani hajawahi kuchangia chochote ndani ya bunge
Suma Mamlo mbunge wa Tabora Kaskazini.
Suma Mamlo mbunge wa Tabora Kaskazini.
Mkuu unajua sana, mungu aendelee kukubaliki hili taifa linakuhitaji sana the upcoming talented leader. ila umesahau mbunge 1 anaitwa festo limbu jimbo la magu na ameshatangaza kutogombea kabisa.
Ulitaka niseme CCM watashinda ndipo uamini ni maoni yangu??
Yaani wote mlio wataja wana hafadhali. Kuna huu mzigo. Abdul Mteketa! Wa jimbo la kilombero. Huu ni mzigo.
Nyambari Nyangwine wa Tarime hatarejea mjengoni hata kwa dawa. Hata yeye mwenyewe analijua hilo, na ameishaanza kufungasha virago.
Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani kuna wabunge wengi sn hawatarudi. Karibu nusu ya wabunge waliopo sasa watakua wanaangalia bunge kupitia TV. Kuna watakaochujwa kwny kura za maoni ndani ya vyama vyao, lakini wengine wataangushwa kwny uchaguzi mkuu.
Kwa maoni yangu hawa ndio wabunge 10 ambao WANA UHAKIKA wa kutokurudi bungeni mwakani. Hawa wataungana na wengine zaidi ya 100 ambao safari yao pia inaishia mwakani.!
1.Cyril August Chami-Moshi (V)
(Ameshindwa kuleta maendeleo jimboni, wananchi wamemkinai na pia chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
2.Said Arfi-Sumbawanga (m).
(Wananchi wamemkinai na chama chake kimemchoka).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
3.John Shibuda-Maswa (mash)
(Wananchi wamemkinai na chama chake kimemchoka).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
4.Aggrey Mwanri (Siha).
(ana uwezo lakini chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake na CHADEMA imedominate sn. Hata baadhi ya wanafamilia wake ni Chadema).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
5.Joseph Selasini-Rombo
(wananchi wamemkinai japo chama chake bado kina nguvu jimboni).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
6.Stephen Massele-Shinyanga (m)
(wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
7.Willium Ngeleja (Sengerema).
(Wananchi wamemkinai japo bado chama chake bado kina nguvu jimboni kwake)
ANTICIPATION: CCM watashinda.
8.Mch.Luckson Mwanjali-Mbeya (v)
(wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake. However hajui kujenga hoja kbs huyu mzee).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
9.Emmanuel John Nchimbi-Songea (m)
(Wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
10.Kisyeri Chambiri-Babati (m)
(wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.
**NB: Haya ni maoni yangu binafsi na hayafungamani na chama/asasi au kikundi chochote. Si lazima ukubaliane nayo, maana na wewe unaweza kuwa na maoni yako pia.!
Nyambari Nyangwine lazima atarudi bungeni, jua liwake ama mvua inyeshe ni lazima atarudi bungeni. Nitakwenda kumsaidia kupiga kampeni nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa. Ni mbunge anayejua matatizo ya wananchi wake na anayashughulika ipasavyo. Ninashundwa kuelewa kwanini hapewi nafasi ya uwaziri.