Top ten ya wabunge wa bara wanaomaliza muda wao

Top ten ya wabunge wa bara wanaomaliza muda wao

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
202
Reaction score
1,588
Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani kuna wabunge wengi sn hawatarudi. Karibu nusu ya wabunge waliopo sasa watakua wanaangalia bunge kupitia TV. Kuna watakaochujwa kwny kura za maoni ndani ya vyama vyao, lakini wengine wataangushwa kwny uchaguzi mkuu.

Kwa maoni yangu hawa ndio wabunge 10 ambao WANA UHAKIKA wa kutokurudi bungeni mwakani. Hawa wataungana na wengine zaidi ya 100 ambao safari yao pia inaishia mwakani.!

1.Cyril August Chami-Moshi (V)
(Ameshindwa kuleta maendeleo jimboni, wananchi wamemkinai na pia chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

2.Said Arfi-Sumbawanga (m).
(Wananchi wamemkinai na chama chake kimemchoka).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

3.John Shibuda-Maswa (mash)
(Wananchi wamemkinai na chama chake kimemchoka).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

4.Aggrey Mwanri (Siha).
(ana uwezo lakini chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake na CHADEMA imedominate sn. Hata baadhi ya wanafamilia wake ni Chadema).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

5.Joseph Selasini-Rombo
(wananchi wamemkinai japo chama chake bado kina nguvu jimboni).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

6.Stephen Massele-Shinyanga (m)
(wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

7.Willium Ngeleja (Sengerema).
(Wananchi wamemkinai japo bado chama chake bado kina nguvu jimboni kwake)
ANTICIPATION: CCM watashinda.

8.Mch.Luckson Mwanjali-Mbeya (v)
(wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake. However hajui kujenga hoja kbs huyu mzee).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

9.Emmanuel John Nchimbi-Songea (m)
(Wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

10.Kisyeri Chambiri-Babati (m)
(wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

**NB: Haya ni maoni yangu binafsi na hayafungamani na chama/asasi au kikundi chochote. Si lazima ukubaliane nayo, maana na wewe unaweza kuwa na maoni yako pia.!
 
upo sahihi kabisa ila kumi na moja mwigulu aka gaidi wananchi wamemchoka
 
Mimi nilivyoona heading nikawahi nije nicomment cyrill chami wa moshi vijijini,hafai kabisa ni kweli wananchi wake wamemchoka hakuna chochote alichofanya zaidi ya kukarabati barabara ya kwenda kwake manushi
 
Umemsahau muheshimiwaSana Makongoro Mahanga na Mama Mwaiposa. Wanajimbo maeneo ya Tabata na Ukonga wataniunga mkono hapa. Hawa walishakubali matokeo kuwa hawarudi tena Bungeni, usishangae wakaigiza kustaafu
 
Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani kuna wabunge wengi sn hawatarudi.

8.Mch.Luckson Mwanjali-Mbeya (v)
(wananchi wamemkinai na chama chake kimepoteza umaarufu jimboni kwake. However hajui kujenga hoja kbs huyu mzee).
ANTICIPATION: Chadema watashinda.

**NB: Haya ni maoni yangu binafsi na hayafungamani na chama/asasi au kikundi chochote. Si lazima ukubaliane nayo, maana na wewe unaweza kuwa na maoni yako pia.!

Una haki ya kuwa na maoni yako, lakini kama unalifahamu hili jimbo la Mbeya Vijijini na nguvu ilizokuwa nazo Chadema kwenye jimbo hili kuelekea uchaguzi wa 2010 lakini pamoja na hivyo nguvu hizo hazikutosha kushinda.

Kwa sasa Chadema sio tishio tena kwenye jimbo hili. Ukilinganisha nguvu zao (waliposhindwa) na nguvu zao za sasa bila shaka hili jimbo litabaki CCM.Mbunge wa jimbo hili ataamuliwa kwa kura za maoni za ndani ya CCM, na kwa hali iliyopo sasa bado Mchungaji Mwanjali ana uwezekano mkubwa wa kushinda ndani ya chama chake pia.

Kwa mkoa wa Mbeya ushindani mkali bila shaka utakuwa katika majimbo ya Mbeya Mjini, Mbozi Mashariki, na Mbozi
Magharibi. Majimbo yaliyobaki CCM haitakuwa na shida sana

Jimbo la Mbarali linaweza kuwa na ushindani kama CCM watamtema Kirufi ambaye amekuwa na migogoro sana na viongozi wenzake kwenye chama, wakifanya hivyo bila shaka atatafuta chama cha kugombea na kuwasumbua sana.
 
Profesa Jumanne Abdalla Maghembe
Wananchi wamemchoka anaishi kwa nguvu ya Dola kutokana na Jiografia ya Mwanga!
ANTICIPATION: Mshindi wa Uchaguzu atatangazwa saa tisa Usiku kati ya Tadayo Joseph (CCM) na Henry Kileo (CHADEMA) kutokana na jinsi Uchaguzi utakavyokuwa na ushindani Mkali!
 
Jitu lenye soni Babati vijijini mbunge wa mkurugenzi mlay hatorudi alisaidiwa kushinda kwa Hila CDM itashida kilaini sana
 
Bila kuwasahau: -
1. Dr. Hamis "Said Bagaile" Kigwangala a.k.a mzee wa vitumbua. Kule msomali - Bashe - kamkalia kooni, Anapumulia mashine!! NZEGA
ANTICIPATION: CCM itashinda

2. Luhaga J. Mpina - ana mgogoro wa chini chini na kamati yake ya siasa (W) ingawa kwa wananchi hana tatizo kubwa
ANTICIPATION: CHADEMA itashinda
 
Hamisi Kagasheki - anamgogoro na chama. Ametanguliza ubabe na matusi, wapo wanomuunga mkono lakini wachache akina kagasheki family: chamadema/ccm yeyote aweza kushinda
 
Ongezea #[Prof Mark Mwandosya*] jimbo lake liko wazi

Mwakyusa japo wanaobashiri wanadai Kasesera anaweza kunyakua lakini cdm wakishupalia tunampoka kasesera kirahisi
 
Kuna mbunge mmoja ni zigo anaitwa Bukwimba wa jimbo la Busanda akirudi bungeni 2015 nitajua watu wa Busanda tumerogwa, pia hata Marx wa Geita mjini ni wale wale kasoro majina.
 
Watu wa Bunda Tafadhali saana, tuondolee hilo dude, weka mtu sense za utu si za kinyama. Nadhani na huyu ataondoka.
 
Back
Top Bottom