Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,609
- 1,739
Katika vyama vikuu vya upinzani Tanzania inasemekana vimo vyama vivuli au wakala.Nilichowahi kusikia ni kuwa Chama cha CHADEMA ndio chama nambari one kinachotumika au kutumiliwa na CCM ,vilevile wapo wanaosema Chama cha CHADEMA ni Tawi la CCM ambalo ndilo linajuwa mambo yote ya CCM.Kuzushwa kwa siri za mafisadi ,mahesabu ya fedha za walala hoi zilizo chotwa kutoka BOT zote zimeibuliwa na CHADEMA.
Kwa kuwa Chadema ndio Chama kinacholengwa kuwa ni tawi mama la CCM ,ni watu wachache tu wanalilijua hilo ,na hivyo kuifanya Chadema kutoonekana moja kwa moja uhusiano wake na CCM naweza kusema ni TOP Secret.
Hatari ya uhusiano huu ni pale wanasera wanapogongana na kufarikiana katika hekaheka za kutafuta tonge.
Tonge ya mlo wa BOT ,Richmond na nyenginezo ziliwatenga vigogo wa CHADEMA na kuwafanya wavurugike akili kwa kuona wenzao wamewakosesha mgao.Na matokeo yake ni siri nyingi za ufisadi kuanza kutolewa pamoja na mahesabu ,yote hayoyakiongozwa na CHADEMA.
Ingawa WATANZANIA wananchi wengi wapo nyuma katika kuliona hili kiasi cha kuwafanya washindwe kutambua upi ni Mchele na zipi ni Pumba panahitajika ukachero mkubwa kuezua na kuuweka wazi ushirikiano wa chini kwa chini wa CCM na CHADEMA.