Top 100 Universities in Africa...Heko UDSM!!!

Nimejaribu kufanya utafiti kuhusu ranking ya chuo chetu kikuu UDSM, lakini naona hapa ni siasa zaidi au huwa wanatumia theoretical assumptions zaidi kuliko reality...! Hivi unaweza vipi kurank chuo ni cha 24 wakati kina lecture theatre moja? Seminar room 3?

Maprofesa wasiozidi 20? tena wengi wao ni uchwara wanoaamini kufelisha wanafunzi na kutunga mitihani migumu na isiyojibika ndio kupima akili au uwezo wa mtu kitaaluma?Irrelevant courses basing on the global need and country needs? Student lecturer ratio is 1:80? Je hicho ndio chuo cha 24 Africa? Kama ni hivyo basi hali ya hivyo vyuo vingine vinavyotufuata ni mbaya sana, na haipaswi mtu kwenda kusoma huko...!

Mhafidhina punguza munkari bwana.
Kwa taarifa yako ranking za vyuo vikuu zinaweza kutizamwa ktk mambo matatu;RESEARCH,CUNSULTANCY na ACADEMIC exccellence.Siyo kweli kuwa wapo professors wasiozidi 20.Wapo zaidi ya hao na ushahidi ni idadi ya postgratuate degrees zinazotolewa pale.Kwa wingi wa wanafunzi na courses haiwezekani chuo kikawa na dadi ndigo hivyo.Ushahdi upo.

Pili siyo kweli kuwa professors pale wanaamini katika kufelisha.Yawezekana ikawa ni mchezo wa wachache lakini hauondoi ukweli kuwa UDSM inareputation ya kuigwa popote.
Tatu,ratio ya lecturer na wanafunzi kwa UDSM ni ndogo kuliko mahala pengine africa na duniani.Kumbuka wenzetu wana mpaka wanafunzi elfu tano kwa kozo moja na professor mmoja anatoa lecture.Sema wenzetu wana facilities za kusaidia (ICT).Vilevile wenzetu wanachofanya ni kuwa na assistants wakutosha kuendesha semina na tutorials kusudi wawe na groups ndogo.
Kwa taarifa yako ,kilichoipandishaUDSM kwenye ranki ni RESEARCH zaidi kuliko academics.Hii haina maana kuwa chuo chetu hakifanyi vizuri

Tatizo la kufeli lipo zaidi kwa wanfunzi na ushahidi upo.Kwa miaka hii ya elfu mbili kumekuwa na the so called bad crop vyuoni na hivyo matokeo yamekuwa mabaya na wanafunzi wamekuwa wakilalamika kana kwamba wanafelishwa.

Let us give our university its due respect and encourage studnts to study hard.
 
Hii thread ina mlengo wa kutofautisha watu wanaochangia... nani kasoma mzumbe, nani kasoma ulaya, nani kasoma UDSM, nani kasoma tumaini n.k. Nijuavyo mimi ni kuwa UDSM ni chuo chenye reputation kubwa sana kwa utafiti na elimu bora especially katika miaka ya tisini. Hii ni kwasababu ya ubora wa wanafunzi waliokuwa wakiingia chuoni hapo. na GPA walizopata ni haki kulingana na uwezo wao. sina uhakika na sasa kwa chuo hiki na nakubaliana na wanaosema kuwa kina matatizo mengi kutokana na sera mbaya za serikali yetu kama vile kulazimisha kuongeza idadi ya wanafuzi wakati miundombinu ni ileile. Theatre rooms ni chache, vitabu vya kugombea n.k

kwahiyo wakati tukijadili hili tusiangalie ushabiki kama wa arsenal na manu U. yani hata kama timu ni mbaya lakini kwakuwa ni yako unaishabikia tu.

Tumesikia ya UDSM, tuchambue ya Mzumbe, Ardhi, Sokoine kwa mlengo wa constructive critisism. kuliko kuegemea pale ulipotata digrii yako.
 
vyuo vyote tanzania vina mapungufu. tuwe wawazi na tusifiche maana ukisema udsm au mzumbe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom