Top 10 African Countries With the Most Chinese Debt

Top 10 African Countries With the Most Chinese Debt

yamindinda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
1,589
Reaction score
1,320


MATAIFA KUMI BORA AFRIKA YANAYODAIWA NA CHINA.

10. Congo DRC - Usd 3.4 Billion.

Taifa hili lilikuwa Taifa la kwanza kabisa kuingia Mikataba ya Mambo ya madini na Taifa la China.

09. GHANA - Usd 3.5 Billion.

Hali ya Ghana kiuchumi ni Mbaya kwa sasa kiasi kwamba imebidi wayakubali Masharti kadhaa ya IMF ili waweze kupewa Masaada wa pesa ili walipe deni la China.

08. NIGERIA - Usd 4.8 Billion

Kutakana na deni hili kuwakaba koo, Taifa hili kubwa la Afrika ya Magharibi sasa imebidi liikubali Shilingi ya China (Chinese Yen kutumika kama fedha ya kigeni katika Taifa lao - Foreign Currency)

07. CAMEROON - 5.5 Usd Billion

China imekubali kuwasamehe Cameroon sehemu ya Deni hili kwa masharti ambayo hayajawekwa hadharani.

06. ZAMBIA - 6.0 Usd Billion.

China imechukua Shirika la Umeme la Zambia kama Sehemu ya Malipo ya deni hili mara baada ya Zambia kushindwa kulipa...Republic of Zambia sasa unaweza kuiita "Repupuliki ofu Chambia"

05. SUDAN - 6.4 Usd Billion

Sudan kwa sasa wamepeleka Ombi maalumu huko China kuomba Msamaha wa Sehemu ya Deni,

04. CONGO BRAZAVILLE - 7.3 Usd Billion

Deni hili kwa sehemu kubwa Limesababishwa na Rushwa iuliyoshamiri nchini humo, fedha nyingi zimeliwa bila manufaa yoyote, Hali tete.

03. KENYA - 7.9 Usd Billion

Mabilioni haya mengi yalikopwa kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu, lakini fedha nyingi zimeliwa na wajanja, Deni hili kubwa limechochewa hasa na Rushwa, Reli ya SGR kenya imejengwa kwa Gharama mara 4 zaidi ya Gharama za viwango vya kimataifa ..hata hivyo kenya imeongeza Ushuru wa Mafuta na bidhaa mbali mbali ili iweze kulipa deni hilo, na pia imeomba Msaada IMF na kuyakubali Masharti yao.

02. ETHIOPIA - 13.5 Usd Billion

Walikopa mapesa mengi kwa ajili ya maradi wa reli ya kutoka Ethiopia kwenda Djibouti, deni hili kubwa leo linawagharimu.

01. ANGOLA - 25 Usd Billion.

China wanaendelea kuchukua Mafuta kwa wingi huko Angola kama Sehemu ya malipo ya deni lao.
 
Kufikia 2025 kama hatutachukua tahadhari na sisi tunaweza kuingia kwenye mkenge wa madeni ya China.

Tanzania hatuna uchumi imara kiasi cha kusema kuwa tutakamilisha miundo mbinu yote kwa muda mfupi kwa fedha zetu za ndani.
Mara bandara ,Mara , reli ,Mara , Umeme, Mara ,kiwanja cha mpira ,Mara ndege ,Mara Meli,mara vivuko ,Mara makao makuu, mara kiwanja cha ndege cha kimataifa,Mara marudio ya chaguzi zinazosababishwa na ubinafsi wa watu.
Hapo bado kununua Treni ya umeme za umeme na mabehewa yake. Vitu vyote hivyo vinahitaji fedha nyingi na havitaendeshwa kibiashara bali kihuduma.

Athari ya deni tutaiona miaka 10 - 25 ijayo.
Kwa sasa huko mitaani tunaanza kuona magari yenye nembo ya "China Aid". Ni dhahiri kuwa hata kwetu China inafadhili baadhi ya miradi kwa sasa japo usiri ni mkubwa.

Wanasema ,"Mwenzako akinyolewa wewe tia maji".
 
chin africa debt.jpeg
 
Wachina wamechochea moto kweli baada ya Trump kukaza sasa wanahitaji kuhakikisha nchi za Afrika nyingi tuingie (into debt) na wao na kiukweli bara letu bila mtazamo tofauti tumeumia hakuna taifa lolote kubwa lililo na mema kwetu.
 
Hii ni jibu kwa all haters wa Serikali wanaoisingizia kwa kila jambo baya. Baadhi hadi wanajisikia vibaya kuona Tanzania tumekosekana katika top 10, right?
hata tukidaiwa USD 500M kwa uchumi huu uliokufa tutazilipaje. Makusanyo ya Mapato yetu ya mwezi mzima yanalipa mshahara tu hela zimeisha.
 
hata tukidaiwa USD 500M kwa uchumi huu uliokufa tutazilipaje. Makusanyo ya Mapato yetu ya mwezi mzima yanalipa mshahara tu hela zimeisha.
Uchumi ulio kufa ni Wa mfuko wako
Pole sana
 
Tanzania itakuwemo ni swala la muda tu na kuna facilities zitakuja kuwekwa rehani huko tuendako. Tuna Myopic Leaders Ever.
 
Hii ni jibu kwa all haters wa Serikali wanaoisingizia kwa kila jambo baya. Baadhi hadi wanajisikia vibaya kuona Tanzania tumekosekana katika top 10, right?
Roho mbaya tu zinatusumbua mkuu, ndo maana hatufanikiwi
 
Back
Top Bottom