Toothless TAKUKURU?

1800

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
2,215
603
Wadau naomba kujuzwaa hawa watu wa TAKUKURU, ni namna gani waendeshavyo shughuli zao? Imekuwa ni taasisi isiyo na meno bali ipo kama pambo, sina uhakika sana kama nitakua sahihi kwa ili nalotaka liweka hapa litahusiana na TAKUKURU, kama TAKUKURU hawahusiki basi naomba elimishwa juu ya taasisi ihusikayo na ili!

Hapa Morogoro ukumbi wa starehe wa Chilalakale kila mtu anaujua kutokana na ujenzi wake wa gharama sambamba na hotel ya gharama kubwa zinazojengwa kwenye milima ya uluguru, kuna minong'one mingi kua ukumbi huo na hotel hiyo ni za mtoto wa mkuu wa kaya/mkuu wa kaya mwenyewe, na minong'ono hiyo imepata nyama zaidi baada ya kijana mjasiri wa kupora mali Riz moja kuonekana mara kadhaha akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wake unaoendelea!

Mbali ya ujenzi huo wa gharama za kupindukia unaohusisha hotel kubwa na ukumbi wa starehe vinavyojengwa maeneo mawili tofauti,pia kuna magari 14 yaliyoifadhiwa/kufichwa katika hotel hiyo huko milima ya Uluguru yakisubiri ufunguzi wa hotel nayo yaanze ku oparate!

Cha msingi hapa nachojaribu kujiuliza, je Takukuru haioni kua kuna umuhimu wa kumchunguza huyu anaejinasibu kumiliki hotel na ukumbi huo wa gharama kwa kua ni mtumishi wa umma? Je kipato chake hata kama amechukua mikopo kinaendana na ujenzi wa mabilioni ya pesa unaofanyika huko Moro?

Kipindi cha Mwl Nyerere huyu mtu alikua kishahojiwa zamani sana! Mmiliki anaejinisibu kua ndie mmiliki wa vitu hivyo anaitwa Malumbi ambae ni close friend wa mkuu wa kaya na pia ni mfanyakazi wa serikali!

Nia yangu si kupinga maendeleo yanayofanywa na mtu/watu hao bali ni uhalali wa kipato cha kuweza kufanya mambo hayo kwa wakati mmoja!
 
Hii ndiyo ile taasisi ya kuzalisha na kuendeleza rushwa tanzania? Nasikia katika uchaguzi wa ccm uliopita maeneo mengine (mf Bukoba) wajumbe walihongwa elfu 50 na maofisa wa takukuru waliokuwepo laki 500
 
Hawa jamaa wanachukua rushwa kama watumishi wengine wa serikali,,, wengine tumeishawadelete hawa jamaa
 
Hii ni Taasisi ya Kulinda na Kuficha Ufisadi wa Viongozi!!!

Kinachosikitisha wanapenda kujihusisha na virushwa vidogo,vya 50,000 mara rushwa za chakula,wakati rushwa kubwa zilizo na ushaidi wa wazi na ambazo ni sumu kubwa kwa ustawi wa nchi yetu wanazifumbia macho!Watanzania lazima tuamke na kupinga wizi huu wa wazi wazi,kulalamika pembeni wakati wao wanatuona kama vikatuni hakutatusaidia
 
Siku zote mbwa haumi aliemlea na kumpa chakula.
Takukuru hawezi fanya kazi akiwa chini ya ikulu

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hawa jamaa wakikabidhiwa uchunguzi basi mi hua nasahau kabisa coz hakuna cha zaidi kitacholeta hatua za kisheria kuchukuliwa......!
 
Hawa jamaa wakikabidhiwa uchunguzi basi mi hua nasahau kabisa coz hakuna cha zaidi kitacholeta hatua za kisheria kuchukuliwa......!

Na sidhani kama uwa wanashindaga kesi zilizoko mahakamani,nina shaka hata huo ushahidi uwa wana uharibu wenyewe
 
Ukitaka kujua umahiri wao wa kazi waone wanavyojitutumua wakimkamata Mtendaji wa kijiji akishindwa kusimamia ujenzi wa darasa au zahanati!
 
Na mbaya zaidi wakati mradi huo wa ma billion ya hela ukiendelea,wananchi wa Bigwa wanashiba vumbi tu kutokana na barabara ya Bigwa kutokua hata na changalawe tu,na week end ndio uwa wanaipata fresh maana kuanzia ijumaha mpaka jumapili hakuna wa kupata usingizi kwa kelele za muziki zitokazo Chilakale,pia mtu huyo anaejifanya mmiliki wa Chilakale,amevunja hata sheria za mazingira,kwa kujenga ukuta umbali wa mita si zaidi ya moja kutoka kwenye mkondo wa mto,ila hakuna wa kumuambia wala wa kuthubutu kuhoji au kuvunja ukuta!mbunge Aboud yuko kimya kabisa yeye kakalia amani na utulivu
 
Kijana Riz moja hataki mchezo,naona kila mkoa anawekeza tu!ile project ya Chilakale si mchezo wakuu,ni billion nyingi sana zinayoyoma!dogo ni billionea in Tshs
 
Nimeambiwa kwamba Ijumaa iliyopita baada ya mkurugenzi wa zamani wa Tanesco, william Mhando kufikishwa Kisutu kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka ya ufisadi na wizi, ghafla ikaja simu kutoka ngazi za juu kwenda kwa Mwendesha masihitaka wa takukuru ikimuuliza: "Kwani huyo Mhando ameiba kuku? Hebu mwondoeni hapo mara moja!"
 
TAKUKURU wanameno yote 32 ila Boss wao Dr. Hosea ni jamii ya Tendwa, IHEMA na wachumia tumbo wengine. Ana nafasi sawa tu na Jaji Manento, lkn yeye ni kama mbwa aliyefungwa mpaka ambiwe kamata! Uwezo wa vijana wake uwezo wa kufanya kazi ni mkubwa mno (Kumbuka Kura za maoni ndani ya CCM 2010).

Dr. Hosea anaaibisha PhD ya sheria na wale walimpatia pia. Shame on him.
 
Unayo yaongea ni mambo ya msingi sana katika nchi inayojali utawala wa sheria, lakini katika nchi ya kishenzi kama yetu, nani amfunge paka kengele.

Ni nchi ya wenye nchi,the untouchables na watwana.The untouchables hawaulizwi kitu, wao kila kitu ni ruksa.TAKUKURU ni mali yao,nani atie neno?

Hivi umeshawahi kuona kesi ya Ngedere akapelekewa Nyani?TAKUKURU ipo kwa ajili ya kulinda maslahi yao na kuwakandamiza watwana.
 
Unayo yaongea ni mambo ya msingi sana katika nchi inayojali utawala wa sheria, lakini katika nchi ya kishenzi kama yetu, nani amfunge paka kengele.Ni nchi ya wenye nchi,the untouchables na watwana.The untouchables hawaulizwi kitu, wao kila kitu ni ruksa.TAKUKURU ni mali yao,nani atie neno?Hivi umeshawahi kuona kesi ya Ngedere akapelekewa Nyani?TAKUKURU ipo kwa ajili ya kulinda maslahi yao na kuwakandamiza watwana.

Mkuu ni kweli kabisa usemayo,kuna genge la wahuni na majambazi wachache ambao wanajifanya viongozi,kifupi naweza sema hatuna viongozi bali genge la watu hao!ila lazima Watanzania tujue kua hii nchi ni yetu wote,hatuwezi kuendelea kukaa pembeni na kuwaangalia tu hawa hiki kikundi cha watu wachache kiendelee kuitafuna bila huruma nchi na kunufaisha familia zao tu,lazima tupaze sauti na kuwaonyesha hasira zetu ili wajue wazi kua hawako salama na uhuni waufanyao!na tunajua wizi wote wanaofanya,awe rais,waziri au balozi
 
Kulikuwa na tetesi kuwa ofisi zao za mikoani na wilayani zilishafungwa? Ni kweli au ilikuwa ni fix tu!
 
Back
Top Bottom