Too early to die at 21 yrs my love.

Too early to die at 21 yrs my love.

tangaraha

Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
51
Reaction score
9
Inahuzunisha sana wanajamvi, mpenzi wangu alifariki ghafla. Alikuwa na tatizo la moyo alilokuwa anatibiwa kwa miaka 4,
Nataka kushare shairi nililoliandika leo, toka nimeanza liandika asubuhi mentally nimepata relief.Napenda kuwa na normal bereavement, usiombe yakukute

1
Siku kwanza nakuona, nilikupenda nikili
Ulivutia kisura, tabasamu na mavazi
Nilikupa simu namba, tukashika urafiki
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

2
Upole yako tabia, ukarimu na ucheshi
Na akili nyingi pia, Mola alikubariki
Sirahisi kudanganywa, ulikuwa dada nguli
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

3
Uislam washika, ulipenda yako dini
Ulivutia tabia, ulishika maadili
Mavazi yako mazuri, hijabu na baibui
Umetutoka mapema, upumzike mapema

4
Kukuficha nilishindwa, mapenzi ni kikohozi
Kipole nikakuomba, kweli ukanikubali
Kwadhati nilikupenda, penzi la hali na mali
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

5
Yako makini tabia, ilinikwaza mwanzoni
Kukurubuni napanga, kufanikiwa nafeli
Msimamo hukuyumba, ulinifunza nakili
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

6
Ni ishirini na moja, wa mwisho wako umri
Ndani ya mwaka mmoja, tumekuwa wapenzi
Tulipendana hakika, hilo kweli nakili
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

7
Zawadi uliitunza, kweli niliisubiri
Ulisema utanipa, tukishafanya harusi
Na niyako bikra, uliitunza zawadi
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

8
Ni ndani ya huu mwaka, ndo umetutoka mpenzi
Ni thelathini na moja, siku ya mwezi wa kumi
Nikama vile naota, iwe ndoto natamani
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

9
Ni kifo kimetutenga, kabla ya yetu harusi
Inatushangaza sana, Mola ajua siri
Tarehe zako ni sawa, kuzaliwa kufariki
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

10
Mimi nitakukumbuka, ni kwapendo lako zuri
Familia inalia, inayonyingi huzuni
Ni Mola ameruhusu, tumebaki na majonzi
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani.


Pumzika kwa amani mpenzi, kila uliponiweka kitimoto nikutajie sababu zote kwa nini nakupenda mara zote nilikuwa sitaji sababu moja, nilikuahidi hiyo nitakuja kukwambia muda ukifika. wapi tena ntakwambia?
Ni kwa sababu ulinikatalia tusikutane kimwili hadi ndoa, hiyo ilichangia nikupende zaidi na kukuheshimu. I will always love u, your were so unique.
 
pole sana. Mungu akujalie faraja ya moyo.
 
pole sana mkuu!!

sijui waliogonga like wamemaanisha nini!!?
 
Have a strong heart to contains all pains. R.i.p my shemeji.
 
Kwake Mola amekwenda, imani mtaonana,
Japo Kimwili Kakutoka, kiroho ninyi wamoja,
Dua tunamuombea, pumziko liwe jema,
peponi mkikutana, ya Mungu Mtapeana.

Ni hatua unapitia, maumivu na machungu,
Muhimu kuvumilia, kipindi hiki kigumu,
Kwa kuwa ulimpenda, Kumsahau vigumu,
Tulizo utalipata, kutoka kwa Mungu wetu

Shemeji twamuombea, ahela yake makazi,
Zetu dua twapeleka, tukitikwa na machozi,
Majozi alokuachia, yafutwe na nzuri njozi,
Mola atazokujalia, umkumbukapo lazizi
 
aiseee vina vimeenda shule.
R.I.P my wiiii
 
pole sana chief. Mungu akuongoze ktk kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana.

Mungu ampe safari ya kheri na wee akujaalie subrah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom