Too early to die at 21 yrs my love.

Too early to die at 21 yrs my love.

mmmmh....bongo inabadilika eehe...?
 
Inahuzunisha sana wanajamvi, mpenzi wangu alifariki ghafla. Alikuwa na tatizo la moyo alilokuwa anatibiwa kwa miaka 4,
Nataka kushare shairi nililoliandika leo, toka nimeanza liandika asubuhi mentally nimepata relief.Napenda kuwa na normal bereavement, usiombe yakukute

1
Siku kwanza nakuona, nilikupenda nikili
Ulivutia kisura, tabasamu na mavazi
Nilikupa simu namba, tukashika urafiki
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

2
Upole yako tabia, ukarimu na ucheshi
Na akili nyingi pia, Mola alikubariki
Sirahisi kudanganywa, ulikuwa dada nguli
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

3
Uislam washika, ulipenda yako dini
Ulivutia tabia, ulishika maadili
Mavazi yako mazuri, hijabu na baibui
Umetutoka mapema, upumzike mapema

4
Kukuficha nilishindwa, mapenzi ni kikohozi
Kipole nikakuomba, kweli ukanikubali
Kwadhati nilikupenda, penzi la hali na mali
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

5
Yako makini tabia, ilinikwaza mwanzoni
Kukurubuni napanga, kufanikiwa nafeli
Msimamo hukuyumba, ulinifunza nakili
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

6
Ni ishirini na moja, wa mwisho wako umri
Ndani ya mwaka mmoja, tumekuwa wapenzi
Tulipendana hakika, hilo kweli nakili
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

7
Zawadi uliitunza, kweli niliisubiri
Ulisema utanipa, tukishafanya harusi
Na niyako bikra, uliitunza zawadi
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

8
Ni ndani ya huu mwaka, ndo umetutoka mpenzi
Ni thelathini na moja, siku ya mwezi wa kumi
Nikama vile naota, iwe ndoto natamani
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

9
Ni kifo kimetutenga, kabla ya yetu harusi
Inatushangaza sana, Mola ajua siri
Tarehe zako ni sawa, kuzaliwa kufariki
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani

10
Mimi nitakukumbuka, ni kwapendo lako zuri
Familia inalia, inayonyingi huzuni
Ni Mola ameruhusu, tumebaki na majonzi
Umetutoka mapema, upumzike kwa amani.


Pumzika kwa amani mpenzi, kila uliponiweka kitimoto nikutajie sababu zote kwa nini nakupenda mara zote nilikuwa sitaji sababu moja, nilikuahidi hiyo nitakuja kukwambia muda ukifika. wapi tena ntakwambia?
Ni kwa sababu ulinikatalia tusikutane kimwili hadi ndoa, hiyo ilichangia nikupende zaidi na kukuheshimu. I will always love u, your were so unique.
pole sana itabidi umtafute linex akuimbie halafu uwe unasikiliza sawa mkuu enheee..
 
She is gone## bt she will always remain closer to ur heart# her memories will liv forever......trust me,i knw hw it feels to loose someone you love.SHE IS IN A BETTER PLACE NOW.Be strong for her.
 
Asante sana Security Code, wanaweza kuwa wanaungana katika majonzi haya, sema shortcut options ni chache

mkuu like inakuwa misused, maana hasa ya like ni nini? like maana yake mependa kitu fulani! si ndiyo? sasa we habari ya kifo we unagonga like una maana kwamba umependa yamtokee yaliyomtokea ama vipi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom