- Thread starter
- #41
Kwake Mola amekwenda, imani mtaonana,
Japo Kimwili Kakutoka, kiroho ninyi wamoja,
Dua tunamuombea, pumziko liwe jema,
peponi mkikutana, ya Mungu Mtapeana.
Ni hatua unapitia, maumivu na machungu,
Muhimu kuvumilia, kipindi hiki kigumu,
Kwa kuwa ulimpenda, Kumsahau vigumu,
Tulizo utalipata, kutoka kwa Mungu wetu
Shemeji twamuombea, ahela yake makazi,
Zetu dua twapeleka, tukitikwa na machozi,
Majozi alokuachia, yafutwe na nzuri njozi,
Mola atazokujalia, umkumbukapo lazizi
Asante sana masatujr na wana mmu wote kwa maneno yenu ya faraja