msafiri.razaro
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,239
- 731
Mimi kelo yangu uuzwaji wa madawa ya kelevya Sinza makabulini. Kuna mama mmoja anaitwa MAMA DOMI huyu mama anauza madawa mchana kweupe, akiripotiwa hukamatwa na polisi baada ya masaa mawili utamkuta mtaani kama kawa. Vijana wadogo wameharibika kweli, iliwapate madawa sometimes inabidi wajiingize kwenye uvibaka, wakipora au kukwapua wanapokosa wa kummuuzia utakuta wanabadilisha vitu vya wizi na madawa kwa huyu mama. Ukiibiwa kitu ukiwahi kwa huyu mama utakuta vitu vyako anasema kanunua, akipelekwa polisi kijitonyama anaachiwa faster. Kila polisi anamjua pale. Huyu mama sijui na ajenti wa kuuza madawa ya nani kwani inaonekana ni kigogo kwani simu tuu inatosha kumtoa huyu mama polisi na kufuta kesi. My take huyu mama anaweza kuonyesha mtandao wa madawa ya kulevya.