Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Huyu mzee amezaliwa hivyo haigizi hatanii na wala hana mzaha JPM amekuwa ni mtu mwenye misimamo isiyoyumba anasimamia anachokiamini hapepesi macho sasa nyie mnaozoea mzaha mtaumia bure
Msimamo ni kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge? Huo ndiyo msimamo wa kukiuka Sheria na katiba? Msimamo ni kumfukuza CAG kisa kaomba kukagua mahesabu ya ununuzi wa Ndege, ofisi ya Bunge na kusema ukweli juu ya trillion 1.5 zilizopigwa kienyeji? Hiyo misimamo ya kuwafukuza wasio na vyeti lakini akabagua na kumlinda Bashite asiye na cheti ni misimamo ya aina gani?
 
ID yako imasema umejiunga JamiiForums 20/09/2019, nyie ndio wale "MAVUVUZELA WA LUMUMBA" mnaopewa posho za bando 2,000/= wenye ID 40 za kuja kujaza server za JF.
Watetezi wa CCM wengi ni mbumbumbu vilaza wapo ghetto kwa cyprian Musiba na le mutuz wakivuta Bangi kisha kukariri kila wanacholishwa na hao wabwekaji wa Taifa ndiyo maana utetezi wao wote hufanana
 
hivi kumbe bado kuna watu hawawezi kujenga hoja yaani wew ndo wakusema anamisimamo inamaana kuvunja katiba ni msimamo this is bullshit yey ni nan katika nchi mpak amewafanya watu kusahau kua na yeye kuna misingi ya uongozi lazima aifate
Huyu mzee amezaliwa hivyo haigizi hatanii na wala hana mzaha JPM amekuwa ni mtu mwenye misimamo isiyoyumba anasimamia anachokiamini hapepesi macho sasa nyie mnaozoea mzaha mtaumia bure
 
Magufuli hana vigezo vyovyote vya uwezo wa maisha ya ki utawala kijamii na kifamilia yeye kwake kila kitu mzaha mzaha tu poor him
Mshauri wake mkuu ni Naibu Rais Daud Bashite na huyo Bashite ni mkuu wa kitengo wa kamati za ufundi a.k.a Ndumba unategemea nini hapo?
 
Hadi kiasi cha rushwa wanachopokea kwa siku unajua.

Du!!!, uko vizuri kiuchunguzi.
 

wew kinachokuuma n nini
 
Kabisa hilo inabidi lifanyiwe kazi na wahusika.
 
Kero yangu ni katika barabara itokayo Zakhem Mbagala kwenda Mbagala Kuu ipitayo kibonde maji.

KERO: Kipande cha barabara kinachoanzia kibonde maji hadi Kichemchem hakijawekwa lami ina Mashimo Mashimo makubwa na mengi

MADHARA:-

-Magari yanaharibikaMara kwa Mara
- muda mwingi hupotea sana kukipita na kuvuka kipande hiki cha barabara
- Mvua ikinyesha Gari ndogo hazipiti kirahisi
- Daladala nzim hazipiti eneo hili kwa kuogopa kuharibika kwa hiyo route hii inatambulika kama ya Daladala mbovu.

Hoja zinazosikika mtaani zinasema kipande hiki kilirukwa hii barabara ilipokuwainajengwa lami sababu ya bomba la TAZAMA linalosafirisha mafuta kwenda Zambia.

Najiuliza mara kwa mara, kwamba ina maana hatuna utaalama wowote wa kuhakikisha lami inajengwa eneo hili bila kuathiri miundo mbinu ya Bomba la TAZAMA..!!!

Maana nakumbuka Bomba hili huko mbele limekatisha na kuvuka barabara itokayo Dar kwenda Tunduma..
Je? hapa inashindikana vipi.!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebu raisi wetu musimpe mzigo atatuwa kero za wananchi ngapi kwani viongozi wengine wanafanya nini au wanaunga mkono huku wao ni mkono kinywani tu ?
 
Wasalimie
 
Treni ya reli ya Kati DSM hadi mwanza, mabehewa ya second na first class hayatutoshi.
Mabehewa mawili ni machache. CEO TRL Ben Kadogosa tafadhali Kanda ya ziwa tuongezee mabehewa.
 
Ndugu viongozi wa ngazi mbalimbali katika Nchi yetu, nijuavyo mimi ni kwamba, WASALITI,WAHAINI na WAASI hawana nafasi ya kuendelea kuishi katika Nchi husika. Hata Malaika Mbinguni walipoasi tu Mungu aliwatimua,itakuwaje Binanadamu?
 

Hili swala liko kushoto kidogo, is this the official Robot or a hoax? As far as I know JF is already bought by a certain party, kulikoni?
 
Mheshimiwa Waziri wa Nishati, sisi wananchi wa Kijiji cha Ihowanza, Kata ya Ihowanza, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, tunaomba utusaidie kutatua kero ya umeme. Umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara bila utaratibu. Muda mwingine zinapita hadi Wiki mbili bila umeme kuwepo. Tuna mashaka na Mkandarasi aliyeleta umeme huku kwetu. Tunaomba msaada wako.
 
Ni wanufaika wa vyeo tenda mbalimbali kwenye kampuni zake binafsi na Serikalini hao kutwa kumsifia bila Aibu

April 11, 2020

ZITTO KABWE AICHAMBUA RIPOTI YA CAG 2018/19
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Mh. Zitto Kabwe (Mbunge Kigoma Mjini), akichambua ripoti ya CAG kwa mwaka 2018-19 na Ripoti za CAG kwa miaka 5 ya serikali ya awamu ya tano .
Hivyo uchambuzi huo unalenga ktk maeneo makubwa kumi muhimu :


Source: Mwanahalisi TV
  1. Kuporomoka kwa makusanyo ya kodi : hivyo serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya bajeti na hivyo bajeti kukosa maana inayo kusudiwa ya uwiano wa makusanyo dhidi ya matumizi pia ufanisi wa kukusanya kodi.
  2. Deni la Taifa ktk awamu ya tano ya serikali ya CCM linakuwa kwa kasi kubwa yaani asilimia 12% kuliko kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi ulio ktk wastani wa asilimia. Serikali imeanza kushindwa kulipa madeni ya ndani mfano kulipia Hati Fungani yaani Government Bonds jambo lililo hatari maana yake wananchi na wanunuzi wengine wa hati fungani kukosa imani ya serikali kuweza kulipwa amana zao. Serikali inadaiwa kiwango kikubwa na watoa huduma ikiwemo wakandarasi, makampuni na watu binafsi. Wakala wa Barabara yaani TANROADS ni mdaiwa sugu mwenye deni kubwa yaani Bilioni 900. Serikali pia inaficha kipande cha madeni ya Hifadhi za Jamii yanayofikia trilioni 3 shilingi za kiTanzania na wastaafu kuwa ktk hatihati ya kushindwa kulipwa malipo yao.
  3. Ufisadi umerudi nchini kupitia transit goods kwenda nchi jirani umeongezeka sana kufuatana na taarifa ya CAG. Kiasi cha bilioni 300 ni kimepotea ktk awamu ya 5 huku awamu ya Jakaya Kikwete upotevu ulikuwa bilioni 45 tu.
  4. Kesi dhidi ya serikali yaani contingent liability kimefikia trilioni 1.8 za shilingi za kiTanzania kutokana na kutotii mikataba na wadai kukosa imani ya kulipwa.
  5. Manunuzi yasiyofuata sheria yafikia Shilingi Trilioni moja kwa unapproved suppliers.
  6. Serikali inaendelea kutumia fedha za umma bila kufuata katiba ibara ya 135 yaani kupitia mfuko Mkuu wa serikali yaani Consolidated fund bila idhini ya Controller and Auditor General.
  7. Ukaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania umefanywa na GAG bila kutumia kampuni za Ukaguzi za binafsi Dillotte, KPMG n.k hivyo kukosa uwazi na uhuru wa kufanya ukaguzi huru unaoaminiwa na IMF, WORLD BANK na wabia wengine.
  8. Korosho zanunuliwa na fedha kutoka Benki Kuu na fedha hizi hazijarejeshwa Benki Kuu
  9. Ndege kununuliwa bila taratibu za kifedha zilizo wazi.
 
Tunahitaji katiba mpya ambayo hizo sauti zitapewa uzito
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…