Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Nyumba za Watanzania zaidi ya 8000 zilizojengwa kwa gharama kubwa na maeneo nyeti zilizogaiwa kwa wajanja wachache kama wakina Mussa na Sundi huku Taifa likiingia gharama ya mamilioni ya fedha kuwalipia watumishi wake hotel za kifahari na nyumba za kupanga ni jipu kubwa linalohitaji kutumbuliwa na kutibiwa.Kwa ufupi:#WeNeedBackOurHouses!!
 
Mimi naona Majipu ni Halmashauri zote nchini. Zikiongozwa na Majiji ya Mwanza na Dar, majiji hayajawahi kupata HATI SAFI YA MKAGUZI WA HESABU za Serikali eti Mkurugenzi wake anahamishwa kutoka Mwanza anapelekwa Dar!! Duhh maajabu Tz!! Zaidi ya miaka 8 hati Chafu na Hati ya Mashaka ndio mchezo wa Halmashauri zetu!!!!!

Hapa ndipo uhusiano wa Serikali na wananchi ulipo moja kwa moja. Miradi yote ya Maji ni madudu tu!! MEM, MESS ni madudu tu. Vyoo ni madudu tu. Usafi ni madudu tu. Upimaji wa miji ni madudu tu. Michoro ya kisasa ya barabara na ujenzi wa barabara za kisasa ni madudu tu.
 
Trafic
akiacha bomoa bomoa Mafuriko hayatawaacha, akiacha, akiacha walijenga maeneo ya wazi watoto wetu watakosa sehemu ya kuchezea. Nafikiri bomomoa ni halali maana tunawapenda ndugu zetu.

Police traffic pale kituo cha salender jana amekura rushwa ya sh 5000 kwa mzungu alikua anaendesha gari aina ya range rover, Mzungu huyo alipita service road ya ktk akashikwa akampa police sh 5000 akaachiliwa, nilijaribu kupiga picha kama ushahidi nikashindwa upande walikua hakuwa rahisi kupiga picha.

Naomba waonywe waache kujidhalilisha kwa kupokea rushwa kwa wavunja sheria na pia waache kutegea waendesha magari ili watengeneze mazingira ya rushwa!
 
Police traffic pale kituo cha salender jana amekura rushwa ya sh 5000 kwa mzungu alikua anaendesha gari aina ya range rover, Mzungu huyo alipita service road ya ktk akashikwa akampa police sh 5000 akaachiliwa, nilijaribu kupiga picha kama ushahidi nikashindwa upande walikua hakuwa rahisi kupiga picha.

Naomba waonywe waache kujidhalilisha kwa kupokea rushwa kwa wavunja sheria na pia waache kutegea waendesha magari ili watengeneze mazingira ya rushwa!
 
Aende na kwenye mifuko ya jamii hasa NSSF kuna ulaji WA kufuru kwa viongozi. Karibu wote wamejilimbikizia utajiri WA kufuru, kuanzia mkurugenzi mkuu na ghorofa lake pale karibu na leaders club, uje kwa akina Msemo na hotel yake ya Safina Kijitonyama. Lile shirika limejaa ufisadi wa ajabu
 
"JIPU LA POOL COLLECTION ACCOUNT BUGANDO HOSPITAL MWANZA"
SIFA YA HII ACCOUNT-NO COST ANALYSIS,FIXED AMOUNT FOR 3DAYS
-NI MAAMUZI YA SERIKALI KWA WANANCHI WAKE.

Kwa mgonjwa anaelazwa anatakiwa atoe 150,000/=cash au kupitia bima ya afya,hii hela hudumu kwa siku 3,na siku ya 4 unaanza kulipia extra charge(40,000/-) kama utaendelea kukaa hospitali, ila hela hii wengi wamechargiwa na kulipia gharama zingine kama vipimo na dawa(ndani ya hizo siku 3)wakiwa ndani ya kifurushi cha matibabu, na mbaya zaidi ikatokea ukakaa cku moja hii hela haina maelezo ya aina ya matibabu umepata na gharama gani umetumia, hivyo ikitokea ulilazwa kwa dharula au kimakosa imekula kwako utajibiwa kirahisi kuwa "HELA IMETOSHA, HUDAIWI"

Kwa Mgonjwa anelazwa na kuhitaji upasuaji unawajibika kulipa 320,000/- vile vile nimekutana na vilio mtu analipa hii pesa na bahati mbaya mtaalam wa upasuaji huo akiwa hayupo,imekwenda na maji,vilio ni vingi kuhusu malipo haya.

Bahati nzuri nimekaa na uongozi wa hospitali mara ya kwanza kunionea huruma, kiongozi aliniandikia nirejeshewe 100,000/-lakini alivyokwenda kumuona mkurugenzi kuidhinisha, wakabatilisha na nikajibiwa kuwa haya ni maagizo ya serikali, nikaomba kama kuna waraka wowote, niliambiwa hapana!kwa mtaji huu serikali itakusanya fedha hata haramu kwa watu wa hali ya chini kwa mfumo wa POOL COLLECTION ACCOUNT.-

Mh.Ummy Mwalimu, na Naibu Mh Kigwangala.,
 
Trafic


Police traffic pale kituo cha salender jana amekura rushwa ya sh 5000 kwa mzungu alikua anaendesha gari aina ya range rover, Mzungu huyo alipita service road ya ktk akashikwa akampa police sh 5000 akaachiliwa, nilijaribu kupiga picha kama ushahidi nikashindwa upande walikua hakuwa rahisi kupiga picha. .........

Ikiwa haikuwa rahisi kupiga picha hiyo elfu tano uliiona kivipi?
 
Hotuba ya Rais kwa wazee wa dsm imenikumbusha JIPU moja alipo sema watanzania wanauliza na kujadili kuwa katika siku 100 za kuingia madarakani Rais amefanya nini na kwamba wao hawajiulizi wameifanyia nini Tanzania.

Pia, amewataka watanzania kulipa kodi, kudai risiti kila wanapo nunua kitu.

Baada ya kuunganisha kuhimizwa kulipa kodi, kudai risiti, nimewaza kuwa hata unapo pata huduma serikalini na ukatakiwa kutoa fedha yakupasa kudai risiti.

Katika tafakuli hilo, nimejiuliza ni watanzania wangapi wamenunua mashamba au nyumba na hawakutekeleza au hawatekelezi kulipa kihalali 10% kodi ya serikali?

Ni hivi, kuna kautaratibu fulani kwamba unapo nunua shamba, nyumba na ukataka uthibitisho wa serikali ya kijiji, mtaa ama mahakama una ambiwa kutoa asilimia kumi ya thamani ya mauziano/manunuzi na kwamba matumizi ya fedha hiyo eti ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya eneo / chombo husika!

Kwanza
Naomba mwenye ujuzi wa hili anifahamishe kama ni kweli ndiyo matakwa ya sheria na sheria ipo. Ukiambatanisha kifungu husika itasaidia sana.

Pili
Naona kiasi hiki ni kikubwa sana na kinaweka mwanya wa kutoa rushwa badala ya utekelezaji wa takwa lenyewe.

Tatu
Kwa nini kiasi hiki kisipunguzwe ili a) kilipike b) mnunuzi ama muuzaji asishawishike kutoa rushwa kukwepa kutoa kiasi kikubwa cha fedha c) kuepuka kunemeesha viongozi wa ngazi husika d) serikali ipate haki yake kitu ambacho hata mtoaji atanufaika na mchango wake kwa Taifa?

Hili ni ombi maalum, serikali itafakari vizuri ipunguze kiasi hiki I we asilimia 1 tu. Nina amini ikiwa 1% ni kiasi ambacho kinalipika na serikali itanufaika nacho kuliko hali ilivyo sasa. Niombe pia serikali isione kwamba kupunguza kiasi hiki kutoka 10% hadi 1% itapunjika badala yake itanufaika na ni kiasi kitakacho msukuma mtanzania kulipa hususani anapo ona kodi yake inatumika vizuri na inamnufaisha!
Hili nalo jipu.
 
jipu lingine ni magari ya mwendo kasi yatazinduliwa lini i mean kuanza kupiga mzigo?????
 
Barabara ya Akachube inayoanzia Kijitonyama shuleni inapitabMakumbusho mpaka Mwananyamala Ro ,BRabara hii ina ndugu yake innapita Polisi mabatini. Hizi zote ni majipuyal ni zaidi ya jipu.
 
JIPU KUU: 1. CCM kuondoa maadili na miiko ya uongozi katika siasa na utumishi wa umma. Uongozi ukageuzwa ni fursa ya kupiga dili za kupora mali ya umma.

2. CCM kukumbatia utamaduni wa kutumia rushwa katika chaguzi zake za ndani. Viongozi wanaochaguliwa, ambao tayari ni wahalifu, wanaunda mtandao mkubwa wa kifisadi.

3. Kitendo cha CCM kufunga ndoa haramu na wafanyabiashara katika msingi wa "Scratch my back and I will scratch yours" (kichangie chama na chama kitakusaidia kupata "unafuu wa kulipa kodi").

4. CCM kukataa Rasimu ya Warioba ambayo ingerejesha miiko ya uongozi. CCM ni mhimili mkuu wa ufisadi nchini. To eradicate institutionalised corruption in Tanzania CCM must be outlawed.
 
Mh Rais,

Chunguza watumishi wa NAO wanavyojipatia pesa na kuficha maovu mengi hasa katika wizara na taasisi za umma. Wao huficha maovu na kuwataka ma CEO au Wakurugenzi kuwalipa pesa nyingi ili kuficha maovu yao.

Pili ni watumishi wa hizi zinazoitwa mamlaka; mfano PPRA, TPDC, TRA. Hawa wamekuwa ni chanzo kikubwa cha kuonesha kutokuwapo na usawa Tanzania kwakuwa wanalipwa mishahara mikubwa saaana tofauti na taasisi nyingine kama serikali kuu.

Kwa hili, kuna haja ya kuangalia upya mifumo ya mishahara kwa watumishi wote wa umma
 
Majipu yangu yapo DIT:

1) Kuna Teaching Tower imeanza kujengwa tokea 2007 lakini hadhi leo 2016 jengo halijakamilika na pia jengo limeanza kupasuka (Lina nyufa)! Sijui wanajiita wahandisi wa nini?

2) Hakuna viti vya kutosha madarasa ya A7, A8, A9, B12, B15 na T classes

3) Workshops zimejaa vumbi, hakuna feni, taa, viti , na madawati poa ni shida (All workshops except W16, 12, D2, Multimedia 1 &2 )!

4) Vyoo vimejaa na kibaya zaidi vinatiririsha maji machafu ovyo ovyo; hii ni hatari kwa afya za wanafunzi.
 
Jipu langu:

St. Joseph University in Tanzania, Mbezi na TCU kuna harufu ya rushwa. Walikuja wakaguzi kutoka TCU, wahindi walihangaika siku mbili au tatu kuficha maovu yao

- Kukarabati mazingira ya maabara kuficha kompyuta zilizo chini ya kiwango

- Kuandaa wanafunzi wa kujibu maswali ikiwa watauliza wakazi

Lakini walipofika hawakukagua maabara wala mazingira ya chuo ila walijifungia ofisini ikawa vikao tu; na kula na kunywa huku wahindi wakisimamia show, baada ya hapo wakaondoka lakini hali ni mbaya.

Wizara husika inahitajika kufuatilia wasiende huku wametoa taarifa

Washtukize
 
Jipu kubwa limeiva wilayani Mbinga kwenye machimbo ya mkaa wa mawe Ngaka.

Watu wamehamishwa kwa usimamizi wa mbunge wa zamani G.Kayombo lakini hawakulipwa fidia halali. Makaa yanayochimbwa na waAustralia kwa madai ni majaribio lakini wanauza na kusafirisha sana nje.

Pale ziwani Nyasa kumetengenezwa gati inapakia makaa na kuvushwa kupitia Malawi hadi Afrika kusini. Pale hakuna TRA, Customs, Uhamihaji nk. Nchi inapoteza mapato makubwa sana.

Majaliwa nenda huko wewe unarudia Mbinga mjini tu napo hukutumbua lile jipu la ubadhirifu wa Halmashauri ya Mbinga.
 
Mbunge wa Wilaya ya Mvomero wakati huo Ndg. Makala ambaye pia alikuwa Waziri Mdogo wa maji alitamka kwamba serikali imetenga Sh. Millioni mia tatu kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji unaohudumia Wami Dakawa na Wami Sokoine ambapo yapo makao makuu ya Wilaya ya Mvomero.

Tunazo habari kwamba fedha hizo serikali ilitoa lakini wajanja Wilayani wamezitafuna.

Tunaomba serikali itusaidie kwanza kuwawajibisha waliotafuna hizo fedha,lakini pia tupate hela nyingine ya kuboresha mradi huu kwa kuwa hali ya maji Wami Dakawa na Wami Sokoine ni mbaya kwa ujumla.

Diwani wa eneo husika ni jipu linalopaswa kutumbuliwa.

Huyu anashirikiana na halimashauri kuwahujumu wananchi.
 
Serikali ilitangaza baada ya mafuriko ya April 2015 kuwa ilikuwa na fedha za kukarabati na kuimarisha kingo za mto unaotokea Kimara kupitia Ubungo darajani, Legho darajani, Sinza Uzuri mpaka bonde la Msimbazi lkn mpaka leo kimya. Hizo hela zinasubiri nini au zilitumika kwenye uchaguzi?

Nawasilisha jipu...
 
Jipu huko Morogoro...

Sehemu inaitwa Kasanga karibu na manispaa ya Morogoro...kuna mradi wa maji ulikwama... Mbunge wa kipindi hicho(mwaka jana) na anayeendelea alitoa siku zisizozidi kumi na nne(14) mkandarasi afanye marekebisho ya mfumo wa maji sehemu hiyo.

Hili lilitokana na Mbunge kwenda kufungua mradi huo lakini maji yalishindwa kufika kwa wateja baada ya mfumo kupasuka kutokana na kutumia mabomba madogo na yaliyo chini ya kiwango....

Kipele hicho - Waziri wa maji.
 
Back
Top Bottom