Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama Watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.

 
Jipu uchungu nimeliona hospitali ya Mwananyamala kitengo cha maabara watu wanaanza kupewa huduma saa tano. Na wakati wafanyakazi wanafika ofisini saa moja wao ni stori tu na kuacha wagonjwa wanaendelea kuzidiwa.

Mtu amepima toka jana lakini kumpa tu majibu yake asubiri hadi saa tano ndo waanze kutoa majibu....wao na stori tu ofisini
 
Kuna wafanyakazi wa TANROADS wanakuwa na gari Hardbody Ya Tanroads nyeupe inasimama njia ya Msata - Bagamoyo mida ya usiku, wanakula rushwa kwa kila fuso za mizigo zinazopita njia ile.

Kwa siku wafanyakazi hao huenda nyumbani na sh3m.

Tuanze na jipu hilo kwanza maana huo mchezo ulikuwepo tangu yeye akiwa waziri wa ujenzi.

utaifakwanza
 
Jipu uchungu nimeliona hospitali ya mwananyamala kitengo cha maabara watu wanaanza kupewa huduma saa tano. Na wakati wafanyakazi wanafika ofisini saa moja wao ni stori tu na kuacha wagonjwa wanaendelea kuzidiwa....mtu amepima toka jana lakini kumpa tu majibu yake asubiri hadi saa tano ndo waanze kutoa majibu....wao na stori tu ofisini
Asante sana mkuu. Hili kusema kweli ni jipu uchungu. Mamlaka inayohusika imesikia na wasipochukua hatua nao watatumbuliwa. Hapa kazi tu
 
Kuna wafanyakazi wa Tanroads wanakua na gari Hardbody Ya Tanroads nyeupe inasimama njia ya msata -bagamoyo mida ya usiku wanakula rushwa kwa kila fuso za mizigo zinazopita njia ile.Kwa siku wafanyakazi hao huenda nyumbani na sh3m.Tuanze na jipu hilo kwanza maana huo mchezo ulikuwepo tangu yeye akiwa waziri wa ujenzi
utaifakwanza
Njia ya Msata-Bagamoyo sehemu gani exactly mkuu!? Pia ukiweza hata utuwekee namba za hiyo gari hapa. Ahsante sana.
 
Kuna wafanyakazi wa Tanroads wanakua na gari Hardbody Ya Tanroads nyeupe inasimama njia ya msata -bagamoyo mida ya usiku wanakula rushwa kwa kila fuso za mizigo zinazopita njia ile.Kwa siku wafanyakazi hao huenda nyumbani na sh3m.Tuanze na jipu hilo kwanza maana huo mchezo ulikuwepo tangu yeye akiwa waziri wa ujenzi
utaifakwanza
Asante sana sana mkuu. Hii ni taarifa muhimu sana. Hatua zitachukuliwa haraka sana. Na je mkuu Huwezi kupata namba za hiyo hardbody? Ili kurahisishia mamlaka husika kutumbua.
 
Asante kwa kutia moyo suala litashughulikiwa maana vifo vingne ni vya makusudi.

Nakumbuka kuna dogo alikuwa amepimwa siku moja nyuma ila anaonekana kuzidiwa sana, ila wao hawajali kama ni mda wa kazi wanapga stori za michepuko yao na siasa waliniuzi kweli aisee na umati wa watu upo nje unasubiri majibu na vipimo ila wao hawaanzi kazi ni stori mbele.
 
Jipu lipo barabara ya Makumbusho kituoni. Ni mbovu sana na mvua ikinyesha magari na vyombo vyote vya usafiri vinatuama sana na kuharibikia hapo, pia gari inabidi ziwashushie abiria njiani ili wakwepe hiyo barabara.

Hili ni jipu kwa injinia wa wilaya ya kindoni anatakiwa awajibike hii barabara iweze kupitika kwani magari mengi yanashindwa kufika kituoni
 
Kuna majipu bado yapo mengi mfano:

Utafiti mdogo niliofanya, umeonesha kuna shule za msingi zinaendesha tuisheni, mfano.

Shule ya msingi Tumaini na Kimanga zote shule hizi zimeunganishwa pamoja. Walimu wao wamekuwa wakiendesha tuisheni, pembeni kidogo ya shule hizo.

Walimu hao huendesha tuisheni, katika majengo ya shule ya sekondari ya wazazi iliyoko maeneo ya sokoni huko huko tabata kimanga

Chanzo mimi mwenyewe nimefanya utafiti.
 
Kuna majipu bado yapo mengi mfano:

Utafiti mdogo niliofanya, umeonesha kuna shule za msingi zinaendesha tuisheni, mfano.

Shule ya msingi Tumaini na Kimanga zote shule hizi zimeunganishwa pamoja. Walimu wao wamekuwa wakiendesha tuisheni, pembeni kidogo ya shule hizo.

Walimu hao huendesha tuisheni, katika majengo ya shule ya sekondari ya wazazi iliyoko maeneo ya sokoni huko huko tabata kimanga

Chanzo mimi mwenyewe nimefanya utafiti.
Hili sio jipu bali ni chunusi. Waache waalimu wajiongezee kipato halali. Hawaibi na wazazi wa nataka watoto wao wapate elimu. Tafuta jipu ulilete hapa.
 
Pale temeke hospitali wakinamama imekuwa ni wimbo kila siku, Kuna majengo ya kawaida ya chini, haya yanaitwa ya walalahoi ile lile la ghorofa ni kutibiwa wale mahee hee....!!!
Ifike kipindi tujiulize na haya mambo, watendaji wa serikali wanaangaliaje hela panapokutoa hiduma....!!!!!?
 
Njia ya Msata-Bagamoyo sehemu gani exactly mkuu!? Pia ukiweza hata utuwekee namba za hiyo gari hapa. Ahsante sana.
Hawakai sehemu moja wanahama kila siku,kuhusu namba ya gari ni bora aulizwe manager tanroads anajua gari ya shift njia ile. Yaani wale wafanyakazi wote wanaokaa night shift njia ile wakamatwe na kufukuzwa kazi.Au wawekewe mtego
utaifakwanza
 
Huu ni uzi wa whistle blowers kama hamna barabara malizaeni na mbunge wenu hapa leteni nondo za mijitu inayoliibia taifa kwa namna yoyote ile au kama unafahamu mtu aliyejipatia mali kiudanganyifu au wauza ngada huu ndo uwanja wenu
 
Jipu uchungu nimeliona hospitali ya Mwananyamala kitengo cha maabara watu wanaanza kupewa huduma saa tano. Na wakati wafanyakazi wanafika ofisini saa moja wao ni stori tu na kuacha wagonjwa wanaendelea kuzidiwa....

Mtu amepima toka jana lakini kumpa tu majibu yake asubiri hadi saa tano ndo waanze kutoa majibu....wao na stori tu ofisini
Muda wa kuanza huduma hospitali au vituo vya afya vya umma ni tatizo. Usafi unafanywa kuanzia saa 2. Wodini ndo usiseme, kunanunuka, majibu yanasikitisha!
 
Jipu kubwa zaidi lipo kwa uhamiaji kuna wahamiaji haramu wanaofanya kazi bila vibali na hawana vibali vya kuishi nchini pia.

Tumetoa sana ripoti kwa maafisa wa uhamiaji lakini tukageuziwa kibao tukaitwa na boss tueleze kwa nini tunataka kuua kampuni yake yeye hana pesa ya kulipia wageni maana wapo zaid ya 50 so serikali hapa imekosa zaidi ya million 100.

Huyo afisa aliyetuchoma anaitwa John M jina la pili tumemstai kwa sasa tu natafuta namna ya kuakikisha tunafikisha hizi taarifa kwa Magufuli maana huyo Waziri Kitwanga nae ni mzigo tu hatumuamini.

Huu ni ujipu wa hali ya juu sisi tunatoa sapoti kwa taifa wao wanaenda kuchukua rushwa alafu wanatuchoma. Uhamiaji ni jipu jipu kubwa sana.
 
Back
Top Bottom