Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,871
- 6,468
Na DaVinc XV
Katika dunia hii pana yenye milima na mabonde, mito na bahari, jua kali na theluji yenye baridi tele, mwanadamu ameendelea kuishi karne kwa dahri akiwa tofauti kwa sura, sauti,kimo, unene na rangi ya ngozi. Kutoka mweusi kama usiku wa nyika, hadi aliye mweupe kama barafu ya Milima ya Himalaya, kikawaida binadamu amejigawa katika maumbo yanayowashangaza wengi, lakini kimsingi tunatoka katika chanzo kimoja.
Lakini swali linabaki palepale.... Kwa nini sisi, viumbe wa asili moja, tuwe na rangi tofauti??
Je, ni mkono wa Mwenyezi Mungu mwenyewe fundi wa uumbaji unaochora kwa rangi mbalimbali? Au ni kazi ya vichocheo vya nje kama jua au baridi, au labda historia yenyewe imeisugua dunia na watu wake kwa brush ya muda??
Katika makala hii, tunachambua kwa uchache utofauti huu kwa jicho la sayansi, historia, na imani tukimulikwa na mawazo ya wanasayansi, wanahistoria na hata maandiko ya kiroho. Kwa mtindo wa uchambuzi wenye mizizi ya kielimu.
Tutazama katika asili ya mwanadamu na chimbuko la utofauti wa rangi zake.
1. MTAZAMO WA KISAYANSI
a) Asili ya Binadamu
Wanasayansi wengi wanakubaliana kwamba binadamu wa kisasa (Homo sapiens/Modern man) walitokea Afrika ya Mashariki, zaidi ya miaka 200,000 iliyopita. Hili limethibitishwa na tafiti za DNA na utafiti wa visukuku vya kale (fossils).
Wanadai Binadamu wa mwanzo walizaliwa na Afrika ambako kunajulikana kwa kuwa na jua kali katika maeneo mengi, Wataalamu wa sayansi ya vinasaba (genetics) wanatuambia kuwa wote tumetokana na chanzo kimoja ambacho ni africa kisha tukaanza kusambaa pande ngingine za maeneo ya dunia.
"We are all Africans under the skin.”
— Spencer Wells, mtaalamu wa vinasaba wa Marekani, katika kitabu chake The Journey of Man (2002).
Binadamu wa mwanzo walikuwa na ngozi nyeusi sana kwa sababu walihitaji kiwango kikubwa cha melanin ili kujilinda dhidi ya mionzi mikali ya jua (UV).
b) Mabadiliko ya Mazingira na Rangi
Kadiri binadamu walivyoenea nje ya Afrika katika maeneo kama Ulaya, Asia na sehemu za baridi walikumbana na mazingira yenye mionzi hafifu ya jua. Hii ilisababisha viwango vya melanin kupungua ili kuruhusu mwanga wa jua kupenya vizuri kwenye ngozi na kusaidia uzalishaji wa vitamini D.
“Skin color is largely a product of sunlight and evolution.”
Nina G. Jablonski, mtaalamu wa anthropolojia, katika utafiti wake maarufu “The Evolution of Human Skin Color” (2004)
Jablonski alieleza kuwa:
Rangi nyeusi ina faida ya kulinda folate dhidi ya UV.
Rangi nyeupe inasaidia mwili kuzalisha vitamini D katika mazingira ya mwanga mdogo.
c) Mabadiliko ya Vinasaba
Tofauti za ngozi pia zinachangiwa na mabadiliko ya kinasaba (gene mutations). gene kama SLC24A5, MC1R, na TYRP1 zinahusiana moja kwa moja na uzalishaji wa melanin. Tafiti zimeonyesha kuwa jeni moja tu (kama SLC24A5) linaweza kuwa na athari kubwa katika utofauti wa rangi kati ya Waafrika na Wazungu.
Na ni kwa njia ya geni kama SLC24A5 na MC1R, tofauti hizi ziliwekwa ndani ya miili yetu .
Gene mutation nii nini??
Badiliko katika mpangilio wa taarifa ya kiGene ya kiumbe.
Hili badiliko linaweza kutokea kwa bahati mbaya, kurithiwa, au kusababishwa na mazingira kama sumu, mionzi au virusi.
kuna aina nyingi za gene mutation ambazo zinasabanisha athari hizi tukisema tuanze kueleza moja badala ya nyingine muda hautatoshi hizo zinahitaji muda wake.
2. MTAZAMO WA KIHISTORIA:
Safari, Mchanganyiko na Mabadiliko
a) Uhamaji wa Binadamu
Takwimu za kihistoria zinaonyesha kuwa binadamu walianza kutoka Afrika kwenda maeneo mengine zaidi ya miaka 60,000–80,000 iliyopita. Kila kundi lililoishi kwa muda mrefu katika mazingira tofauti lilibadilika kulingana na hali ya hewa na jua.
“As people moved into new environments, their bodies responded in ways that improved their chances of survival.”
— Dr. Sarah Tishkoff, mtaalamu wa jenetiki ya binadamu, Chuo Kikuu cha Pennsylvania.
Wakati historia ilipokuwa bado changa sana binadamu walianza kuhama kutoka Afrika wakiingia Asia, Ulaya, hata visiwa vya mbali
Walikumbana na hali tofauti wengine wakakutana na baridi kali ya Ulaya, wengine joto kali kwenye nchi kama za India na maeneo ya karibu na hapo,
Na kila mazingira yalikuwa kama mwalimu mkali, yakibadilisha maumbile ya mwili polepole — bila hata binadamu mwenyewe kujua.
b) Mchanganyiko wa Makabila na Mataifa
Kupitia biashara, ndoa, vita na utumwa, jamii mbalimbali zilichanganyika. Hali hii ilisababisha uzalishaji wa watu wenye rangi za kati na mseto wa tabia za kinasaba kutoka pande zote.
Kupitia ndoa, vita, na safari za biashara, jamii zikaanza kuchanganyika. Na kutoka humo wakazaliwa watu wa kati si mweusi, si mweupe bali mchanganyiko wa mataifa mawili. Historia ikaandika kupitia miili yetu, kwamba dunia ni moja na sisi ni matawi ya mti mmoja.
🔍 Watafiti kama Richard Lewontin walithibitisha kwamba tofauti za rangi ni ndogo mno kulinganisha na ule 99.9% wa DNA inayotufanya kuwa binadamu.
“There is more genetic variation within so-called racial groups than between them.”
— Richard Lewontin, mtaalamu wa jenetiki.
3. MTAZAMO WA KIDINI:
Wakati sayansi inatafuta siri na inachambua kuhusu gene za wanaadamu na historia inahangaika kupembua kuhusu misafara na miingiliano ya jamii za kale, dini yenyewe inaleta tafakari ya kiroho.
Katika Uislamu, tofauti za rangi ni ishara ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu Uislamu unatambua tofauti za rangi kama alama ya uumbaji na si sababu ya ubaguzi bali wala fulani kuwa zaidi ya kutafakari ufundi na uumbaji wa mwenyezimungu.
QUR'AN
"Na katika Ishara zake ni kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na tofauti ya lugha zenu na rangi zenu..."
(Surat Ar-Rum, 30:22)
Mtume Muhammad (SAW) pia alisema:
"Hakuna ubora wa Mwarabu juu ya asiye Mwarabu, wala wa mweupe juu ya mweusi, ila kwa uchamungu."
Kwa kifupi tutaona katika dini ya kiislam M/Mungu alifanya kuumba kwa utofauti ili tu kuweka namna tofauti tofauti za uumbaji na kumfanya mwanaadamu atafakari zaidi kuhusu uumbaji wa mwenyezimungu. na hakuna class yoyote ya Uumbaji baina yao.
Katika Ukristo, Biblia inasisitiza kuwa wanadamu wote wanatokana na Adamu.
📖 “Na kwa damu moja alifanya kila taifa la wanadamu wakae juu ya uso wa dunia yote.”
(Matendo 17:26)
Hii inaashiria usawa wa binadamu wote na kuthibitisha kuwa tofauti za nje hazina nafasi mbele ya Mungu.
Dini Nyingine
Katika baadhi ya dini za kale kama Hinduism, tofauti za rangi zilihusishwa na tabaka (varna), lakini tafsiri za sasa zinapinga ubaguzi huo. Dini nyingi zimekua zikikubali kuwa tofauti za rangi ni sehemu ya mpangilio wa kimaumbile na kiroho.
✨ HITIMISHO: Sisi ni Miili ya Tofauti, Lakini Damu Moja
Tofauti ya rangi ni kama tofauti ya maua kwenye bustani moja kuna waridi jekundu, maua meupe, na manjano yenye harufu ya kipekee. Hatuwezi kupunguza uzuri wa bustani kwa kusema waridi pekee ndilo lenye thamani. Na vivyo hivyo, tofauti za ngozi ni mpangilio wa maumbile, si kigezo cha ubora.
Katika kila tone la rangi lililo mwilini mwako, kuna historia, kuna mabadiliko ya hali ya hewa, kuna chembe za DNA zilizoandika safari ya babu zako, na zaidi ya yote kuna ushahidi kuwa wewe ni wa kipekee.
Je?
Tofauti za rangi za ngozi kwa binadamu ni matokeo ya safari ya muda mrefu ya mabadiliko ya kimazingira, kihistoria na kijenetiki. Wanasayansi, wanahistoria na viongozi wa kidini wanakubaliana kuwa rangi si kigezo cha ubora au udhaifu, bali ni ishara ya maumbile, mabadiliko na uzuri wa kipekee wa mwanadamu.
Kwa hivyo, badala ya kutumia tofauti hizi kuleta migawanyiko, tunapaswa kuzitazama kama zawadi ya kimungu na uthibitisho wa jinsi binadamu walivyo na uwezo mkubwa wa kuishi na kustawi katika mazingira yoyote duniani.
na DAVINCI XV