Tofauti ya Mwizi msomi na ambaye si Msomi

Tofauti ya Mwizi msomi na ambaye si Msomi

Magehema

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
428
Reaction score
28
Mwizi ambaye si msomi huiba vitu kama mafuta ya jenereta, vifaa vidogo vidogo vilivyo ndani ya gari kama laptop, simu. ipod n.k. Mwizi huyu ambaye si msomi akijitahidi sana kuiba kitu kikubwa ataiba gari! Kwa upande wa pili mwizi ambaye ni msomi yeye haibi vitu kama mafuta ya jenereta, ataiba umeme na kuisababishia nchi nzima kuwa giza, na pia hawezi kusumbuka kuiba vitu kama gari, yeye ataiba barabara na kuwaachia wananchi vumbi na mashimo!!!!!
 
Vilevile mwizi msomi badala ya kusumbuka kubomoa sefu ya hela yeye ataongea na wanaohusika kizichapisha hizo hela very simple.
 
bwizi hajasoma yuko keko,aliyesoma(mfisadi) yuko mtaani,hakuna anayemweza,ni mbunge au waziri !hawezi kuingia keko
 
bwizi hajasoma yuko keko,aliyesoma(mfisadi) yuko mtaani,hakuna anayemweza,ni mbunge au waziri !hawezi kuingia keko


kweli aiseee, na mwizi msomi hawi mfungwa hata mala moja ila anaweza kuwa mahabusu tuu tena kwa mda.
 
Mwizi asiyesoma akiiba anapigwa mawe, mwizi msomi akiiba anapongezwa na wananchi.
 
Na pia mwizi msomi hatumii silaha kubwakubwa wala mabomu.Hateki mabasi na kuwavua nguo abiria na kuwaimbisha wimbo wa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.Yeye silaha yake kubwa ni KALAMU.hii ni silaha inayochapa na kuangamiza kuliko tetemeko la HAITI.
 
Mwizi msomi hatumii nguvu zaidi ya akili kama afanyavyo mwizi asiye na elimu
 
Hakika, mwizi msomi anatisha. ni wasomi wanaoweza kumgundua kirahisi
 
mwizi msomi anakuwa na mtetezi mahakamani, na kama pesa ya kumlipa lawyer ipo, kesi hiyo atashinda! Lakini mwizi ambaye hajasoma, hana mtetezi anaishia jela!
 
mwizi msomi anakuwa na mtetezi mahakamani, na kama pesa ya kumlipa lawyer ipo, kesi hiyo atashinda! Lakini mwizi ambaye hajasoma, hana mtetezi anaishia jela! au atapigwa mawe mpaka kufa.
 
kweli mwizi msomi hawezi kuteka ndege yeye anaiba shirika zima la ndege na kulifutilia mbali katika ramani ya mashirika makubwa nchini.
 
Mwizi msomi husaini mkataba wenye 10% na kusababisha Ingine zote na mabehewa yake yapaki pale workshop ya TRC na adhabu yake ni kubadilishiwa tu wizara.
 
Mwizi mjinga anakwenda kuchota akiba walizojiwekea wenzake uzeeni.
 
Mwizi msomi anachangia sana kuibuka kwa wimbi la wezi wasio wasomi!!
 
Mmejitahidi kujibu utafikiri mpo kwenye mtihani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom