Tofauti ya kura 1% yamliza Sei...........................f | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti ya kura 1% yamliza Sei...........................f

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Tofauti ya kura 1% yamliza Seif


  Na Mwajuma Juma, Zanzibar

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho kukaa chini na kutafakari kwa namna gani waliikosa asilimia moja ya kura, ambayo iliwapatia
  ushindi CCM katika uchaguzi wa Oktoba 31 mwaka huu.

  Tamko hilo alilitoa juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Nungwi Wilaya ya Kaskazini Unguja, ambao uliandaliwa maalumu kwa ajili ya kupongezana.

  Alisema kuwa katika uchaguzi huo CCM ilishinda kwa asilimia 50.1 na wao wakapata asilimia 49.1, jambo ambalo alisema wanapaswa kuliangalia kwa kina na kulipatia ufumbuzi wake.

  Katika uchaguzi huo tulitarajia kwa kiasi kikubwa kupata ushindi, lakini tulizidiwa na wenzetu na hatimaye tukashindwa kwa asilimia hiyo moja, suala hili tunapaswa tukae na kujiuliza ni kwanini tuliikosa asilimia hii,� alieleza.

  Ushindi ni ushindi hata uwe wa asilimia moja kwa vile nchi yetu inaongozwa na katiba, hivyo ni wajibu wetu kujiuliza hii asilimia moja tumeikosa vipi, na tujipange si kwa kuitafuta asilimia moja pekee bali tujiandae kwa ushindi wa asilimia 71, aliongeza.

  Aliwataka viongozi na wanachama hao wasije wakaridhika na hatua iliyopo na badala yake wajipange ili kukiimarisha chama chao, kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Maalim Seif alisema akiwa katibu wa chama hicho amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara katika majimbo na matawi ili kuwakumbusha namna ya kupanga mikakati ambayo itawasaidia katika kukipatia ushindi chama chao.

  Tusije tukaona kwamba muda bado ni mrefu kwa sababu nguo ya Ijumaa hufuliwa Alhamisi lakini nayo inaweza kuwa na mawingu kwa hivyo fueni Jumatatu,� alisistiza maalimu.

  Alieleza kuwa siku zote chama kinakuwa na malengo yake maalumu ambayo kimejiwekea, yanapaswa kutekelezwa ili kuyafikia.

  Alisema kuwa katika mfumo wa serikali chama kina umuhimu wake kwa sababu ndicho kinachochagua viongozi na kuunda serikali, hivyo katika mfumo huo huwezi kukidharau chama hicho.Wakati wote tusisahau kwamba chama kina sera zake, malengo yake na makusudio yake ambayo kutekelezwa kwake ni lazima kiwemo kwenye serikali, alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa kama chama kinataka kutekeleza hilo ni lazima kufanywe kazi na kupata kura nyingi ili kuongoza serikali yenyewe.

  Aliwataka viongozi hao pamoja na wanachama wajipange kwa uchaguzi ujao kwa kuhakikisha kuwa chama chao kinashinda hasa kwa vile bado wananchi wa Zanzibar wanahitaji kuongozwa na CUF.

  [​IMG]


  3 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Ndugu zangu mlikubali tu kwakuwa ulijua utakuwa makamu wa kwanza wa raisi otherwise sidhani kama ungeweza kukubali matokeo kirahisi hivyo kwa kushindwa kwa asilimia moja tu!!!!!!
  Hii inadhihirisha jinsi gani tanzania hatuna viongozi bali tuna waroho wa madaraka!!!!!!
  KWA JINSI HII JE TUTAFIKA KWELI!!!

  December 28, 2010 12:54 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... WALA USIKONDE, ULIYATAKA MWENYEWE NA MUAFAKA WAKO ILI WEWE UPATA UMAKAMU. Wewe ndio utafakari, uwape jibu wenzako badala ya kuwazunguka na kuwatupia mzigo wa kutafakari madudu yako!
  December 28, 2010 1:41 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... acheni coment za chuki watu wakiuuwana ndio raha yenu uroho wa madaraka hautusaidii kama hujui kifo chungulia kaburi SEIF Kafanya na MUNGU ATAMBARIKI safari hii hatujaumizana nyie mnaopenda watu wakiumizana hameni
  December 28, 2010 2:02 AM
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Hivi Seif haoni serikali ya mseto ilikuwa ni hongo kutoka kwa CCM ya kumfanya yeye akubaliane na matokeo ili mradi asiachwe kwenye mataa kwa kuvikwa kilemba cha ukoka ambacho hakikumpa madaraka yoyote yale juu ya ubunifu, usimamizi na uratibu wa sera?
   
 3. m

  maarufu Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lakini jamani fuatilieni historia ya maalim ni bonge la msaliti.
   
 4. m

  maarufu Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na vile vile huyu ndo alimgeuka aboud jumbe kwa kupeleka umbeya kwa jkn
  siyo mtu kabisa wacha cdm wawakatae kama wapinzani
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Nahisi harufu ya Unafiki hapa.....
   
 6. n

  niweze JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hana Hata Aibu Sharif Kauza Visiwani Kote. Sasa Sharif ni Moja wa Sale Out Politician. Kitu cha Kuangalia Mbeleni ni Kwamba Wananchi Tutawajuaje Binadamu Kama Hawa Wasitu Haribie Tanzania Yetu. Wapo Wengi Wana Njaa Njingi na Unafiki... Kwa Wengi CUF Kimekufa Mbele ya Watanzania.
   
 7. M

  MLEKWA Senior Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It was easy and simple how CCM won in Zanzibar Maalim dont need to tell his supporters why CUF lose elction. 4 weeks before the eelction Dr Shein send out the inaguration invitataion to his friends and telling them he was confident he have the number to be President. The invitation was all over the world to his old Friends some of his Friends made Publicly the invitation to us we saw it and we ask our self why Zanziabri we are scraching our heads while there is no election in Zanzibar except new technic ever 5yrs.
  The whole secret of this year election was CUF know how CCM victmized thousands of CUF suppporters not to register to Vote , intimidation, CCM militia was live during election registration time but was quite during the voting time.
  See Pictures of how CUF supporters was victimized by thousands

  http://www.ifra-nairobi.net/observatoire/The%202010%20Elections%20in%20Zanzibar1.pdf

  Zanzibar Violence April 2005
  http://www.ilpi.org/ILPI/Documents_files/31_Voter-registration_Overall-Summary-report.pdf

  How can Maalim win ?
  According to reliable sources, Mkapa came to Zanzibar that night with Mwinyi after getting worried of failing on their strategy. It is believed that he has directed ZEC not to announce Maalim Seif as the winner every one know this Mwinyi is the master mind of the manipulation in Zanzibar it is allover the evidence is every where CCM can not win election in ZNZ fairly.

  Briefing: The Zanzibar election ? Afr Aff (Lond)
  Maalim if you love your party CUF time is up for grab you are in part of the system who was not given Zanzibar ID should be given now as well any one was not registered to vote should be registered now .
  Why Zanzibari cant register any time if they are eligible to register we have national unity Serikali now hello!
  Why ZEC is not reformed ?
  Why ZEC cant solve the problem now not wait until 2014 and say we dont have enough time to solve this time ?
  Why CUF can come clear and explain the people the reality CCM was advitising every where we dinied 30,000 CUF supporters to register this year this is our number to win Presidency for more than 1% and few protected seats of Ubunge and Uwakilishi in Unguja Island. CUF has bright future if Maalim is willing to be clear not to feel shy to his boss not to embarrass him how won election. It is ok to friend in the office and work together but to be truth ful kwenye majukwaa CCM cant win in Zanzibar if election was fair from the start of the registration.
  CUF ca n work with CCM now in Zanzibar but the future iof CCM is to manipulate and if Maalim can use the Vice president position to mobilise more supporters in Unguja Island there is no dout next election Zanzibari will wave CCM bye bye unless onother Magic come up.
  I will advise Maalim not to have hang over of VP five yrs is nothing we need to build CUF in Mainland we have huge opportunity to grow over 110%.
  The way we see Maalim Tumbatu today we need to see Maalim in Mainland as well like Pemba and Tumbatu we demend apreciation in Southern Tanzania CUF got huge supporters this year even grap two seat in Lindi and Kilwa.
  Yours
  Mlekwa. Tunduru
   
 8. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maalim Seif ni kati ya wanasiasa wajanja..wanaoweza kucheza na akili za Watanzania (or Wazanzibar,u can call it), sitaki na sitokaa niamini kuwa alishindwa uchaguzi mkuu 2010..ila ni MAKUBALIANO kuwa awe Makamu waz kwanza wa Rais..historia yake inamsuta kwa hili..ni huyu huyu tunafahamu wazi alimsaliti na kumhujumu Aboud Jumbe kwa Mwalimu Nyerere, akidhani kuwa baada ya Jumbe angekabidhiwa usukani yeye, lakini kwa akili na iliyobobea ya Mwalimu,na wasaidizi wake makini..mambo yalijulikana,na Maalim hakuambulia alichotaka..shame on him..LAKINI IPO SIKU WATU KAMA HAWA-pamoja na mazuri waliyofanya, MABAYA YAO yatajulikana kwa umma,na umma ujifunze namna ya KUISHI NAO-kama watatokea wa wengine wa aina hii ya MAALIM seif-
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  IT IS too late for Seif Sharif Hamad na CUF yake mimi kwa sasa i can see CUF like branch ya CCM...sioni kwa nini Maalim alalamike wakati alifurahia kabisa hatua iliyofikiwa..Si katai Mseto lakini je! Maalimu hakushinda??? Tujiulize jamani
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Du! Maalim kachokoza nyuki!
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  mkuu,
  Kwa JF uko sawa lakini nafikiri Seif anajuwa anachokifanya. Ni mmoja wa wanasiasa mahiri TZ na si fisadi kwa kadiri nimjuavyo na anavyoripotiwa katika habari.

  mimi nafikiri Seif ameanza hiyo mobilisation ya wapiga kura kwa kuwaambia watu wake kuwa next time iwe 71% ya kura.

  Mimi naona watu wanajaribu kupindisha ukweli kuhusu siasa za mageuzi TZ. CUF naona wamejitahidi sana na wanaikosesha CCM usingizi.
  Kuwa wamehimili jembe na nyundo ya CCM na vyombo vya dola tokea 1995 na wamo katika kujitandaza kimtandao mpaka wamepata ushindi huku bara ni dalili kuwa hawajalala. Na kama wameibiwa ushindi katika majimbo mengine huku bara basi dhana ya kuwa hakijitangazi bara haina mashiko.
   
Loading...