Tofauti ya kichuri na kichiri hii

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,999
Hivi sio vyakula bali ni vichocheo vya kula nyama zaidi.

KICHURI
Kichuri kinatengenezwa na kutokana chakula ambacho hakijameng'enywa ndani ya tumbo la mnyama kinachanganywa na ndimu au limao, pilipili na nyongo kinapashwa kwenye moto kinachujwa na baada ya kuwa tayari kinapendeza zaidi ukila na nyuma choma.

Kwa Dar maeneo ya Kitunda kinapatikana kirahisi sabahu wakaazi wengi ni wakurya. Hata mm mara ya kwanza nimelia huko, kizuri sana.

KICHIRI
Hiki huenda kikawa kigeni kwenye masikio ya wengi isipokuwa wachaga hasa wa Kibosho. Binafsi bado sijafanikiwa kuuliza wazee maana au asili ya hili jina.

Mahitaji ni Damu ya mnyama, pilipili, limau na chumvi.
Utachanganya kulingana ujazo wa damu. Ukiweka mchanganyo huo kwenye damu na kukoroga unaacha na kufunika vizuri dk 30 hivi, baada ya hapo ile damu inabadilika rangi na kuwa damu ya mzee ikiwa nzito kiasi(imeiva).
Kama ukila na nyama unaweza kula kilo 1 mwenyewe. Uzuri wake hauelezeki. Ikitokea mwandaaji ameiharibu au kubwaga badi faini yake ni pipa la mbege hapo hapo.

Picha zinakuja...
 
Back
Top Bottom