Tofauti kati ya pasaka ya Agano la kale, pasaka aliyoiacha Yesu na pasaka ya sasa (easter)

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
6,486
10,996

Jibu la Biblia​

Pasaka ni sherehe ya Kiyahudi iliyowakumbusha jinsi Mungu alivyowakomboa Waisraeli kutoka katika utumwa wa Misri mwaka wa 1513 K.W.K. Mungu aliwaagiza Waisraeli wakumbuke tukio hilo muhimu kila mwaka katika siku ya 14 ya mwezi wa Kiyahudi, Abibu, ambao baadaye uliitwa Nisani.—Kutoka 12:42; Mambo ya Walawi 23:5.

Kwa nini iliitwa Pasaka?​

Neno “Pasaka” linarejelea kipindi ambacho Mungu aliwalinda Waisraeli kutokana na lile pigo kubwa la kuuawa kwa kila mzaliwa wa kwanza wa Misri. (Kutoka 12:27; 13:15) Kabla ya Mungu kuanza kutekeleza pigo hilo kubwa, aliwaambia Waisraeli wapake damu ya mwanakondoo au mbuzi kwenye milango yao. (Kutoka 12:21, 22, maelezo ya chini) Mungu angeona ishara hiyo na “kupita juu” ya nyumba zao na hivyo wazaliwa wao wa kwanza wangeokoka.—Kutoka 12:7, 13



Kuadhimisha Pasaka ya kwanza

Kutoka 12:
1 BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, 2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. 3Waambieni mkutano wote, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;

4na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo. 5 Mwana-kondoo wenu atakuwa hana dosari, wa kiume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. 6 Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.

7Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. 8 Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. 9Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. 10 Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.

11 Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni Pasaka ya BWANA.

12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri. 14 Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele

15 Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu yeyote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli.

16Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yoyote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.

17 Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. 18 Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni. 19 Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu yeyote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa kama mgeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. 20Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote.

Hizi sherehe ziliendelea na wakati Yesu anazaliwa alizikuta
Kufunga kwa Yesu siku 40 haihusiani na pasaka

Alichoelekeza Yesu

Kuanzishwa kwa Chakula cha Bwana


Luka22:14Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. 15Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 16kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.

17Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; 18Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. 19Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

20Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]

1 Wakorintho 11:23-26​

Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: Kwamba, usiku ule Bwana Yesu alipotolewa, alitwaa mkate, akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: “Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu.
Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.” Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.

Pasaka ya Sasa

ni sikukuu ambayo Wakristo karibu wote hufanya kila mwaka ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa, kufa na kuzikwa kwake.
Hiyo ni tafsiri ya Wikipedia

Baada ya Yesu kusherehekea Pasaka katika Nisani 14, 33 W.K., alianzisha mwadhimisho mpya:
Mlo wa Jioni wa Bwana. (Luka 22:19, 20; 1 Wakorintho 11:20) Mlo huo ulichukua mahali pa Pasaka, kwa kuwa unaadhimisha dhabihu ya “Kristo mwanakondoo . . . wa Pasaka.” (1 Wakorintho 5:7) Dhabihu ya fidia ya Yesu ni kuu kuliko dhabihu ya Pasaka kwa sababu kupitia fidia ya Yesu watu wote wanaachiliwa huru kutokana na utumwa wa dhambi na kifo.—Mathayo 20:28; Waebrania 9:15.

Je wewe unafuata ipi
 
Harafu anakuja mtu anakwambia Mungu alnaijua kesho kabla ya jana. Wakati tu alikuwa hana uwezo wa kujua hata familia za wayahudi mpaka akawambia kupaka rangi milango. Inamaana kama siri ingevuja wa wamisiri wakapaka na wao basi angekoaa wa kuuwawa siku hiyo

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Wana dini bana sas kulkuwa na haja gan ya huyo Mungu wa ibrahimu kumtoa kafara charii ake aje awafie wanadamu dunian ambapo bado hawa wanadamu walmpinga huyo charii wa Mungu(yesu), sas Mungu akujua kuwa hii njia haitofanikiwa na badala yake si angemuadhibu shetan ili kila kitu kiishe kulko kumfuga hiv anausumbua ulimwengu
FB_IMG_16095048482229044.jpg
 
Sikuja kuitangua nipo kwa ajili ya kukamilisha na hakuna atakae ongeza wala kupunguza. ( Nawaachia amri mpya pendaneni kama nilivyo wapenda mimi). Kubuka upanga kwa upanga, ila yeye alisema Kofi la kushoto basi mgeuzie na kulia ili kuondoa utata na ghadhab isiwepo.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom