Tofauti ya Baba na Mama nimeoiona Leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Wakuu wazazi wa Kiume huwa wana Roho Ngumu sana Ukilinganisha na Mama hii Picha imeniliza na Kunifanya Niongeze Upendo zaidi kwa mama yangu.

Hii ni picha wakati maiti zinaagwa mama akiwa hana nguvu kabisha huyu baba hayuko

IMG_20170508_122856_471.jpg

Uchungu huuu hakuna wa kufananisha
 
Mkuu kila jambo lina faida na hasara, huyu mama anavyolia anatoa uchungu na huzuni lkn huyu baba anayejikaza atateseka kwa muda mrefu moyoni na mara nyingine hupelekea magonjwa ya moyo. Siku hizi kuna wajane wengi kuliko wagane na hii ni moja ya sababu. Machozi ni dawa ya kusahau mambo machungu
 
Wakuu wazazi wa Kiume huwa wana Roho Ngumu sana Ukilinganisha na Mama hii Picha imeniliza na Kunifanya Niongeze Upendo zaidi kwa mama yangu.

Hii ni picha wakati maiti zinaagwa mama akiwa hana nguvu kabisha huyu baba hayuko

View attachment 506186
Una uhakika gani kama huyo mzee ni mume wa huyo mama? Usipoteshe dhamira za watu,unajuaje labda mzee amelia usiku kucha hapo amepata relief...
 
Wakuu wazazi wa Kiume huwa wana Roho Ngumu sana Ukilinganisha na Mama hii Picha imeniliza na Kunifanya Niongeze Upendo zaidi kwa mama yangu.

Hii ni picha wakati maiti zinaagwa mama akiwa hana nguvu kabisha huyu baba hayuko

View attachment 506186
Mkuu wanaume tunaugulia kimyakimya na hivyo maumivu yanatuchoma muda mrefu. Mkuu kwenye tukio kama hilo mwanaume lazima uwe mkakamavu ili mambo yaende. "Poleni wazazi wote mlioondokewa na watoto wetu wapendwa, mwenyezi mungu awape moyo wa subira na akujaalieni wana wengine"
 
Huyo mzazi wa kiume amelichukua jambo kiutu uzima, ameumia na amekubali kwamba yote ni mapenzi ya Mungu, kulia sawa ni moja ya vielelezo vya uchungu lakaini sisi wanaume machozi yetu yako mbali, nasimama pamoja na mababa wote wenye uchungu ambao hawaonyeshi uchungu wao kwa machozi.
 
Back
Top Bottom