johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,919
- 141,885
Maneno hayo yamesemwa na mwanasiasa mstaafu Mzee Mgaya kwamba waasisi wa CUF wakina mzee Mapalala (RIP) ndio walikuwa na malengo ya kushika dola tofauti na wenzao wa NCCR - Mageuzi na Chadema.
Mzee Mgaya amenihabarisha kuwa ukiyaelewa kwa makini malengo ya waasisi wa Chadema utakubali pasipo shaka kuwa Mbowe ndio mtu pekee mwenye sifa za kukiongoza chama hicho kwa sasa.
Waasisi wa Chadema wakina mzee Mtei, Bob Makani, Ndesamburo na Shanga walikuwa ni wafanyabiashara makini wakati wanaasisi chama chao na walikuwa wanaziba pengo lililoachwa na CCM ambacho ni chama cha wakulima na wafanyakazi anafafanua Mgaya.
Wengi walimshangaa Mbowe alivyomleta Lowassa kugombea CCM lakini ni ukweli ulio wazi Mbowe alijua fika kuwa Lowassa hawezi kushinda kama ambavyo hata Dr Slaa asingeshinda ila Freeman aliuangalia uchaguzi wa 2015 kwa jicho la kibiashara zaidi, ananieleza mzee Mgaya.
Kwa muundo wa Chadema na katiba yao ilivyo si rahisi kumtoa Mbowe madarakani hadi atakapopenda mwenyewe na hao makamanda wao wakilazimisha kumtoa basi chama hichi kitakufa kwani hakuna Chadema bila mzee Mtei na mh Mbowe, amemalizia mstaafu huyu wa siasa za Tanzania mzee Mgaya.
Maendeleo hayana vyama!