Tofauti kati ya ONESHA na ONYESHA

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Wataalam wa lugha wanijuze tofauti ya Onesha na Onyesha hasa wakizingatia chanzo cha maneneo hayo na matumizi yake katika jamii
 
hiyo onyesha iko na "y" na hiyo onesha haiko na "y". tuwasubiri vilaza wengine walete tafauti nyengine mimi nishafungua dalasa.
 
Onesha: kitendo, mzizi wa neno ONA; lina maana ya kusaidia/kulazimisha kuona/kutambulisha.
Onyesha: kitendo, mzizi wa neno ONYA; maana yake toa tahadhari (tahadharisha).

Wataalam wa lugha wanijuze tofauti ya Onesha na Onyesha hasa wakizingatia chanzo cha maneneo hayo na matumizi yake katika jamii
 
Onesha: kitendo, mzizi wa neno ONA; lina maana ya kusaidia/kulazimisha kuona/kutambulisha. Onyesha: kitendo, mzizi wa neno ONYA; maana yake toa tahadhari (tahadharisha).
Nimekuwa nikishangaa kwa jinsi vyombo vya habari vya Bongo vimekuwa vikiendesha kampeni dhidi ya mtumizi ya neno ONESHA ambalo kimsingi ndilo linalotakiwa kutumika kwenye matangazo ya Sanaa za majukwaani.
 
Kwa hiyo kusema kutakuwa na Maonyesho ya mavazi,onyesho la mpira ni makosa?
Lakini kwa Bongo Neno Onesha limemezwa na Onyesha,je hiyo inaweza kusababisha kubadilishwa kwa matumizi ya maneno hayo?
 
Back
Top Bottom