Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,701
- 9,779
Utaratibu huu wa kutembeza dozi uanzie bungeni. Haiwezekani mwakilishi wa wananchi uwapotoshe wananchi wa jimbo lako na watanzania wote kwa ujumla kwa kushindwa kuelewa vyema maana halisi ya neno "onyesha". Ipangwe siku, ateuliwe mbunge mmoja kwa ajili ya kusikiliza kwa makini wabunge wanaoshindwa kutumia vyema neno " onyesha" ili bunge linapoelekea kuisha tushuhudie jinsi spika wetu anavyotembeza bakora kwa wabunge walioshindwa kuliheshimisha neno "Onyesha"
Hali kadhalika kwenye vyombo vya habari hasa hasa channels za taifa, haiwezekani serikali ikuamini na kukupa kitengo cha usomaji wa taarifa ya habari, mwisho wa siku ulipotoshe taifa kwa matumizi mabaya ya neno "Onyesha". Serikali ipange siku ya marejereo ya taarifa zenu za habari, ikibainika tu, viboko vya mgongoni vitembezwe mubashala
Inasikitisha sana msomi na kitambi chake, amefunga tai yake vizuri na makarabasha mkononi, halafu kwa bahati mbaya amesomea shahada ya Kiswahili anashindwa kuwasahihisha watu wanaotumia neno " Onyesha" wakimaanisha kuonesha, badala yake anakuwa mstari wa mbele kuharibu lugha
Viboko visiishie hapo, badala yake viwafikie wakalimani kwa kishindwa kuliheshimisha neno hilo. Baada ya hapo serikali iangalie utaratibu mzuri wa kutembeza bakora kwa watanzania wote wanaoshindwa kutofautisha neno Onyesha na neno Onesha. Napendekeza jeshi la kulinda taifa kuchukua jukumu hili
TURUDI DARASANI
Neno "Onyesha" si sawa na neno "Onesha"
Neno "Onesha" limetokana na neno "Ona". Lakini neno " Onyesha" limetokana na neno "Onya". Kwa hiyo kauli za waandishi wa habari za " Mwenyekiti wa mtaa amemuonyesha mkuu wa mkoa mifuko ya seruji iliyotolewa na Mhe. Jokate Mwegero" ife, badala yake tusikie "Mwenyekiti wa mtaa amemuonesha mkuu wa mkoa mifuko ya seruji iliyotolewa na mh..."
Nahisi nimeeleweka, neno "Onyesha" limetokana na kuonya, na neno "Onesha" limetokana na "Kuona". Tuweni makini kwa kweli
Kwa hiyo neno lilitakiwa kutumiwa kwenye nyanja hizo ni neno " Onesha" ."..amemuonesha"
Karibuni hapa Kitambaa Cheupe tuumwagilie moyo