...kulala ni kujinyoosha kwenye mahali bapa au panapofanana na hapo wakati kusinzia ni matokeo ya usingizi. Unaweza kusinzia wakati umesimama,unaendesha gari hata wakati unakula. Ila mara nyingi mtu anayesinzia hupenda kulala ili asinzie vizuri...
Mi naona kulala ni kitendo cha kuuweka mwili sehemu bapa na kusinzia ni kitendo cha kupoteza fahamu kwa muda bila kupata mshtuko. Na inategemea kipi kinaweza kuanza, mfano mwingine anaweza kusinzia kwenye kochi akaenda kulala kitandani na akasinzia. Mwingine anaweza kulala kwanza na akawa anaongea baadae akasinzia