Mapito haya ya Mnyakyusa Ipinda: Hii ndio simulizi yake

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,927
Nilifahamiana na Mnyakyusa Ipinda mwishoni mwa mwaka 2021 kwenye ishu za kushirikishana fursa za biashara mtandaoni.. Hatukuwahi kuonana ana kwa ana lakini tulikuwa na mawasiliano ya karibu sana.

Baada ya muda tukapoteana kumbe alikumbana na madhila mazito makubwa na hii ndio simulizi yake kwa mwandiko wake mwenyewe.

Nilikua nimetokea kariakoo kwa sababu binafsi kuna kitu nlienda kununua, wakati najiandaa kurudi nyumbani Machimbo nkapanda bajaji, wakati nakaribia home simu ikaita, nikamwambia bajaji anishushe tu nimalizane nae cas nataka niongee na simu ya muhimu na pia home ni hapo mbele tu tatembea mdogo mdogo, bajaji akasimama, nkamlipa nikashuka nikaweka earphone maskioni nkaendelea kuongea na simu.

Kumbe niko relini na sijanotice cas niko busy na simu na treni inakuja sjaiona, basi ikanigonga, bahati haikunisaga. So cku naamka najikuta nipo wodini madaktari wamejaa kuniangalia, wakaniambia nipo Moi muhimbili na nina almost mwezi sjafumbua macho napumulia machine tu, hata skujua wanaongea nini sababu kumbe nilikua nmepoteza fahamu zote , hata mtu nnaemfahamu akija nakua simfahamu.

Sasa baada ya kuwa nimeanza kurecover kiasi nikaruhusiwa na nkarudi nyumbani, kumbuka hospital nilikua nafanyiwa kila kitu, nalishwa, naogeshwa, natembelea whealchair nk, hivyo baada ya kurudi home nikaanza kupata nguvu, nikaanza kusimana mwenyewe, nkaweza kutembea kidogo kidogo, pia nikaanzaz kutamka neno moja moja , sababu nilikua siwezi kuongea kabisa, naona, nahisi ika nlikua siwezi tamka.

Baada ya kuona hivyo, sababu mama yangu makazi yake kwa sasa amejenga Tabora, na yeye tayari anabiashara zake Tabora hivo alihamiaga Tabora na wadogo zangu, hivyo akanileta Tabora ili aniangalie kwa karibu, lakini nikamuuliza, nmeanza kupata nguvu, lakini kwa nini mikono haifanyi chochote na haina nguvu kabisa?

Akanipeleka kitete hospital ya tabora ili waniangalie pia wanianzishie mazoezi, after like one week mkono wa kushoto ukaanza kupata nguvu, nikaweza hata kujilisha mwenyewe kwa kijiko but wa kulia haufanyi chochote, pia haunyooki moja kwa moja umejikunja siwezi unyoosha direct, ila nahisia zote ziko.

Daktari akaniandikia rufaa nikaenda bugando cas kuna madactari bingwa zaidi. Bugando walinianzishia vipimo, wakaniweka kwenye MRI machine, wakacheck kila kitu wakaona hakuna any big damage kwa kuangalia MRI machine report.

Hivyo wakadecide kutonifanyia operation sababu hakuna kitu kinahitaji operation, zaidi niendelee na mazoezi ya nguvu kunyoosha mifupa ya mikono irudi sawa. Kuhusu mkono wangu wa kulia wameona tatizo la mishipa ya fahamu (neuro systerm) za huu mkono zinazopitia shingoni hadi kichwani ndio zimepata hitilafu ndio sababu mkono haufanyi chochote wala haujavunjika ila una hisia kidogo tu, ndio sababu hakuna haja ya operation sababu neurose hupona zenyewe, inaweza chukua miezi kadhaa au hata mwaka kupona au isipone kabisa.

Hivyo ndugu, hiyo ndio changamoto ilonikuta, najiskia hudhuni sana, yes naendelea na mazoezi malolo hospital lakini nahitaji msaada wenu, mama yangu hadi amechanganyikiwa, sababu nilikua kila kitu kwake kama msaada mkubwa zaidi lakini sasa niko hivi, ameshatumia fedha nyingi ili nipone, akachukua hadi mkopo mkubwa crdb sababu nilipokua nimepoteza fahamu hawakua na uwezo kuniuliza kama nina bima, hivyo walilipa cash jwa kuchangishana hivo hivo ndugu na marafiki na kumbe nina bima, moi hadi imebaki tunadaiwa 3.4 million na washatumia karibu 8 million ukiangalia gharama zote hadi sasa. Ana madeni kama yote hajui aanzie wapi na kupona sjapona bado.

Ombi langu ni moja tu ndugu zangu, naomba michango yenu, natamani hata nipate mtu wa kunipeke india cas nimeambiwa huko issue za neurose wanaziwrza hasa na itakua rahisi kunitibu, ikiwezekana sawa isipowezekana pia sawa, ila sitaki yote hayo kuwasumbua watu, nachotaka ni michango yenu niweze kuendelea na mazoezi sababu bima yangu ishafika limit, mama ndo huyo anajipiga sana smelize madeni na amalizie mkopo crdb, mdogo wangu nae amemaliza form 6 mwaka huu na amefaulu vizuri sana alipata dvn 1.7, na amechaguliwa udsm nae anamuangalia huyu huyu mama.

Mwingine nae alikua CBE hajamaliza ila alipata mimba ya ghafla amejifungua, yupo nyumbani tu sasa anataka kumaliza na yeye anamuangalia mama, bibi yangu nae alianguka ghafla amevunjika nyonga analala tu sasa, nae anamuangalia mama, yani najaribu kuekeza kiuharisia mama ana stress kiasi gani kwa sasa, naomba msaada wenu, najua mama atafix issues zake yes but yangu ni moja tu, nipone, nahitaji hata million 1 tu ili nilinew bima yangu niendelee na mazoezi, pia angalau nijaribu hospital tofauti tofauti, hasa aghakan sababu hua najua wako vizuri pia

Kwa kifupi haya ndio anayopitia ndugu yetu. Nimeamua kuweka hii mada hapa kwa ushauri, kwa neno la pole ama kwa namna yoyote ile kwa yeyote yule atakayeguswa na hili analopitia ndugu yetu huyu.

Zaidi soma
 
Aisee, ya dunia ni mengi mno.

Mkuu Mshana Jr na ambao mna mawasiliano ya karibu jaribu kufanya utaratibu wa kuweka harambee ili tuweze kumchangia ndugu yetu kwa chochote.
Je, itakuwa sawa tukimualika mhusika afike hapa? Japo ana changamoto ya kuandika, anatumia left kwasasa na muda mwingi analala kutokana na dawa anazopewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom