Toa tathmini kuhusu katuni hii ya GADO kuhusu hatma ya EAC.!

Nikivyoelewa. Wawili wanabebwa na EA punda.
mmoja amekalia kiti cha kumvuta punda. Sasa sijui tangu lini kiti kikamvuta punda.
mmoja ameng'oa taili moja la kiti na anapanda nalo mlimani na amewaachia punda na kiti anawaonesha direction ya kupanda kwenye mlima.
Namuona mmoja anamvuta punda mkia. Nijuavyo punda huwa anapiga mateke. Nadhani atapigwa teke na kuuachia mkia.
Maelezo hapo naona ni mengi mno.
mtunzi wa katuni hii katumia akili sana.
Unaweza kuandika kitabu cha kurasa 100 kuelezea katuni hii.
 
Kabla ya yote, ili hiyo safari iwezekane ilipaswa punda awe mbele ya huo mkokoteni.

NB: Punda hasukumi.., anavuta!
 
Yule mfalme mwenye suit ya blue ni Nani? Anataka direction yake kwa mustakabali mzima wa EA, akisaidiwa na mvuta mkia mwenywe jicho la tatu.
Museveni ndiye mwenyekiti na Kagame mwenye suit nyeusi anamfuata lakini mwenye shati la kijani hataki na ameamua kuondoka na tairi tuone kama mtafika bila mimi.
Una akili nyingi....chukua konyagi Jibapa hapo nakuja kulipa
 
Huyo punda ana shida...anaendesha gari lipo mbele!? kweli Katuni imeonesha E.A hatujielewi
Simuoni mzee wa mmea wa kondeni
 
Nafuu Kiir amezuia kwanza labda aeleweshwe what is going on. Pombe yenyewe imeamua kusepa na tairi kabisa. Roho mbaya tu. Si uondoke kivyako bila kuondoka na parts za machine?!:D
 
Mbona simple sana:

Kwa ujumla safari ya east africa imekuwa kama ujenzi wa mnara wa babeli hv. Ndo tafsiri yake kubwa.
 
Inavyoonekana mambo yameanza kuharibikia kwenye tairi lililo bongonyolewa na kama limetoka tairi ndo hakuna mwendo tena
 
094ef994c3cfa4643f4cbc92c313e925.jpg

Malengo,dira, muelekeo wa kiuchumi, kimaendelo na sera za EA azina uwiano au malengo ya pamoja,
Kuna Tanzania ya viwanda anamuelekeo wake, M7 naye anamalengo yake na hao wengine wote wanamielekeo tofauti, so in short there is no common goals (economic,development,industrialization e.tc) within East Africa Community.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom