To You..

hehehe senks Mzee Moskwito aisee. Halaf mbona unaonekana kimachale au zali limeclick?

....ha ha haa....
00001570_No_comment-1570.jpg
....umeelewa ee?
 
E, Kloro muungwana, hakika umenishtua
Vipi asili wakana, kwa mambo ya vitumbua
Humuogopi maulana, dunia inazuzua
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

usemalo si la mana, ndugu wanihuzunisha
Tigo kitu ya laana, leo nakuhabarisha
Imekatazwa na rabana, mbona mwaihalalisha
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

Duniani tuwe wema, tusimuudhi rabuka
umalaya si jambo jema, vipi akighadhibika
Tutakosa pa kushika, mola kileta gharika
Usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

Ya dunia sitamani,bora niitwe mshamba
vipi nijivue thamani,nichane wangu msamba
Mengi ya sasa huzuni, twajigongeza na mwamba
usasa una mashaka ndugu yangu tahadhari

Na kama nimekukwaza, naomba niwie radhi
Ni wajibu kukukataza, tuyaepuke maradhi
Wengine wayasambaza, kweli hatuna hadhi
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

QUOTE=klorokwini;1996848]Nashika tena kalamu, kujibu lako shairi
Wewe ni mtaalamu , hata kama hujakiri
Vina vyako ni vitamu, nakubali sio siri
vimesheheni nidhamu, si vya kikiri kikiri

Msimamo wa mapenzi, ulonao ni mzuri
Ila hayo ni ya enzi , zama hizo za zaburi
Siku hizi ni utenzi , mapenzi yapo sifuri
Wathaminiwa kwa jinzi, wapuuzwa kwa msuri

Hata hao wazamani, sasa wamebadilika
Ya sasa wayatamani, muda umeshawatoka
Kibibi chavaa mini , kibabu nacho chabaka
Sana ukitathmini , kichwa kitakupasuka.

Kubali kwenda na muda, unusuru afya yako
Kuna tigo pia voda , huku ndiko tuendako
Pombe inaitwa soda, umalaya ni ujiko!
kiwa mkweli utadoda, uishie sikitiko .[/QUOTE]
 
E, Kloro muungwana, hakika umenishtua
Vipi asili wakana, kwa mambo ya vitumbua
Humuogopi maulana, dunia inazuzua
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

usemalo si la mana, ndugu wanihuzunisha
Tigo kitu ya laana, leo nakuhabarisha
Imekatazwa na rabana, mbona mwaihalalisha
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

Duniani tuwe wema, tusimuudhi rabuka
umalaya si jambo jema, vipi akighadhibika
Tutakosa pa kushika, mola kileta gharika
Usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

Ya dunia sitamani,bora niitwe mshamba
vipi nijivue thamani,nichane wangu msamba
Mengi ya sasa huzuni, twajigongeza na mwamba
usasa una mashaka ndugu yangu tahadhari

Na kama nimekukwaza, naomba niwie radhi
Ni wajibu kukukataza, tuyaepuke maradhi
Wengine wayasambaza, kweli hatuna hadhi
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari

QUOTE=.
[/QUOTE]

Ndugu yangu yakuonea, umenisoma visivyo
Yote nilioongea , ndo hali ya sasa ilivyo
Wala sikukusudia, namimi naamini hivyo
Sitojitwika dunia , kuiga mambo ya ovyo

Ninaloamini ni moja, kati ya orodha yangu
Uongo ni wenye tija, mapenzini ni chachandu
Hili limejaa hoja, kiswahili na kizungu
mengine niloyataja, yawahusu walimwengu.

Tukubali tukatae , hili janga tuko nalo
Hata vikao tukae, hatulipunguzi kilo
Tukisema tukimbie, labda tuende selo
Tukiamua tulie , zitalowana taulo

Nakubali ulonena, kuhusu hayo ya tigo
Ni kweli yana laana, si mema hata kidogo
Lakini yangu maana, tuukubali mzigo
Ukitaka kusonona, utaumiza mafigo.

Amini unavyoamini, uishi maisha yako
Wa sasa utamaduni, kuubadili ni mwiko
Wenyewe wauthamini, twaonekana vituko
watuita wa sabini , tukihoji machafuko.

Wala hukunikwaza, hiyo hofu iondowe
Nahisi umenikweza, kunifanya nielewe
Bado nimo najifunza, mwalimu usichelewe
Shairi si ukewenza, liweke tulichambuwe
 
Uongo una tija gani, katika hii dunia
umekatazwa na manani, vitabu vinatwambia
Ni jamno la upunguani, vipi twaufagilia
Kloro fanya hima, ya ulimwengu yanatisha

Mapenzi kitu tukuka, mola ametwambia
vipi leo twazuzuka, machafu twakimbilia
Eti twadai mizuka, mambo teknolojia
Kloro fanya hima, yaulimwengu yanatisha

Bora tukarekebisha, janga unalosema
Maisha haya yatisha, tufanye hima mapema
kizazi kisije kwisha, maadili jambo jema
Kloro fanya hima, yaulimwengu yanatisha

Wadai utamaduni, kubadili sasa mwiko
Hili sikubaliani, hoja haina mshiko
Mola tujaze imani, tupunguze mihemko
Kloro fanya hima, ya ulimwengu yanatisha

Twakubalije mzigo, lile jambo haramu
iweje tupende tigo, tazama ile sehemu
Dunia ina mitego, mola nijaze fahamu
Kloro fanya hima, ya ulimwengu yanatisha

Nivumile we ndugu, na kama nina kuudhi
Mimi si mtu vurugu, napenda yenye kukidhi
Tuachane na uzungu, mola tusije muudhi
Kloro fanya hima, yaulimwengu yanatisha

Ndugu yangu yakuonea, umenisoma visivyo
Yote nilioongea , ndo hali ya sasa ilivyo
Wala sikukusudia, namimi naamini hivyo
Sitojitwika dunia , kuiga mambo ya ovyo

Ninaloamini ni moja, kati ya orodha yangu
Uongo ni wenye tija, mapenzini ni chachandu
Hili limejaa hoja, kiswahili na kizungu
mengine niloyataja, yawahusu walimwengu.

Tukubali tukatae , hili janga tuko nalo
Hata vikao tukae, hatulipunguzi kilo
Tukisema tukimbie, labda tuende selo
Tukiamua tulie , zitalowana taulo

Nakubali ulonena, kuhusu hayo ya tigo
Ni kweli yana laana, si mema hata kidogo
Lakini yangu maana, tuukubali mzigo
Ukitaka kusonona, utaumiza mafigo.

Amini unavyoamini, uishi maisha yako
Wa sasa utamaduni, kuubadili ni mwiko
Wenyewe wauthamini, twaonekana vituko
watuita wa sabini , tukihoji machafuko.

Wala hukunikwaza, hiyo hofu iondowe
Nahisi umenikweza, kunifanya nielewe
Bado nimo najifunza, mwalimu usichelewe
Shairi si ukewenza, liweke tulichambuwe[/QUOTE]
 
Au Mohamed Shossi kaiba pasiwedi ya Kloro??
Siamini kama haya mashairi ni Kloro.
Dada angu mzazi!!!
 
Uongo una tija gani, katika hii dunia
umekatazwa na manani, vitabu vinatwambia
Ni jamno la upunguani, vipi twaufagilia
Kloro fanya hima, ya ulimwengu yanatisha
[/QUOTE]

Pendo huwa linanoga, lugha inapokolezwa
Bila uongo kuzuga, penzi halitotunzwa
"Ukiniacha takuwa mzoga", uongo ulofukizwa
"Nimependa ua na boga" , daima utaliwazwa

"Honey kwako nimeoza", kumbe wadunda mjini
Lakini ushamkweza , mwandani ajiamini
Daima atakusuuza, furaha itajaa ndani
Ukisafiri atauliza , darling unarudi lini?

"Nashiba nikikuona", huu mfano mwengine
Ugali wautafuna , tena tonge nene nene
Lakini ushamkuna, utazawadiwa sebene
Uongo una maana, mapenzini si kwengine
 
Uongo una maana, mapenzini si kwengine[/QUOTE]

Uongo hauna maana..acha kujidanganya..
Kumwongopea mwenzako..akili kuichanganya..
Eti wampenda sana huku nje wachanganya..
Ukweli ndo maana mapenzini nakwambia!

Mapenzi yale ya kweli hayahitaji uongo...
Kama umependa kweli utabadili mwenendo...
Na kila kilicho chake utakiona kirembo...
Ukweli ndio maana mapenzini nakwambia!

Ukimkosa kwa siku moyoni utanyong‘onyea..
Ukimweleza jioni ukweli utammegea..
Bila kuongeza chumvi matamu utamtendea..
Ukweli ndio maana mapenzini nakwambia!
 
Bora tukarekebisha, janga unalosema
Maisha haya yatisha, tufanye hima mapema
kizazi kisije kwisha, maadili jambo jema
Kloro fanya hima, yaulimwengu yanatisha

e
[/QUOTE]

Hapo nimekusikia, na sasa tuko pamoja
Bango tutawashikia, tutaunnda na sinema
Lizzy atasaidia , CPU keshakusoma
Mbu namuaminia, Asha D hayuko nyuma

Jeshi kamili tunalo, hapa hapa Jeiefu
Afrodenzi asemalo, lasikika kwa maelfu
MJ1 kwa midahalo, mjukuu mtiifu
Aspirin my fello , hoja zake ni nadhifu

The Finest wa mbagala, wengi wanamuheshimu
Uporoto hajalala , punde atatia timu
Michelle zake makala, amri utasalimu
Wiselady mpenda mola, achukiae mizimu

Tuna miss wa mpwapwa, Husninyo nae kundini
MTM wa kulipwa , kijana namuamini
Pauline sio chapwa, mada zake tathmini
Kaizer si wa kusepwa, hili jeshi la baharini.

Festiledi wa kwanza, nasaha zabubujika
Nyamayao apendeza, akiwepo patashika
wengine sitomaliza, muda umeshatimka
Hawa wakitekeleza, jamii itabadilika.
 
Au Mohamed Shossi kaiba pasiwedi ya Kloro??
Siamini kama haya mashairi ni Kloro.
Dada angu mzazi!!![/QUOTE]

hehehe kijana ukiendelea kuleta fujo tutakuondosha seat ya mbele. hapa tupo studio za torabora laivu
 
Uongo hauna maana..acha kujidanganya..
Kumwongopea mwenzako..akili kuichanganya..
Eti wampenda sana huku nje wachanganya..
Ukweli ndo maana mapenzini nakwambia!

Mapenzi yale ya kweli hayahitaji uongo...
Kama umependa kweli utabadili mwenendo...
Na kila kilicho chake utakiona kirembo...
Ukweli ndio maana mapenzini nakwambia!

Ukimkosa kwa siku moyoni utanyong‘onyea..
Ukimweleza jioni ukweli utammegea..
Bila kuongeza chumvi matamu utamtendea..
Ukweli ndio maana mapenzini nakwambia![/QUOTE]

Uongo ninaohubiri, ni ule wa kukoleza
Hiyo nyekundu shubiri, wala sitoichombeza
"Nakupenda sio siri" , "hata roho nitauza"
"Nitapoteza kamari" , "ili wewe kukutunza"

"Mimi nitakufa nawe", kuzimia waogopa.

"Sitolala bila wewe", wakoroma kama tipa
"Wanimaliza ujuwe", kila siku wanenepa
Lugha ina utamuwe, mapenzini bila shaka

Chumvi chumvi maneno, ni vizuri muelewe

"Hakika huna mfano", siri waijua wewe
"Nayapenda yako meno", usiombe yang'olewe
Hii ni yangu mifano, ipo toka nizaliwe
 
Fellow tablet,

Unaweza kunipa sababu tatu kuu kwanini hili liyuziful sredi lilinipita namna hii?

Ngoja nikaanze peji ya kwanza!
 
Uongo hauna maana..acha kujidanganya..
Kumwongopea mwenzako..akili kuichanganya..
Eti wampenda sana huku nje wachanganya..
Ukweli ndo maana mapenzini nakwambia!

Mapenzi yale ya kweli hayahitaji uongo...
Kama umependa kweli utabadili mwenendo...
Na kila kilicho chake utakiona kirembo...
Ukweli ndio maana mapenzini nakwambia!

Ukimkosa kwa siku moyoni utanyong‘onyea..
Ukimweleza jioni ukweli utammegea..
Bila kuongeza chumvi matamu utamtendea..
Ukweli ndio maana mapenzini nakwambia!

Uongo ninaohubiri, ni ule wa kukoleza
Hiyo nyekundu shubiri, wala sitoichombeza
"Nakupenda sio siri" , "hata roho nitauza"
"Nitapoteza kamari" , "ili wewe kukutunza"

"Mimi nitakufa nawe", kuzimia waogopa.

"Sitolala bila wewe", wakoroma kama tipa
"Wanimaliza ujuwe", kila siku wanenepa
Lugha ina utamuwe, mapenzini bila shaka

Chumvi chumvi maneno, penzi hudumisha sana

"Hakika huna mfano", siri waijua wewe
"Nayapenda yako meno", usiombe yang'olewe
Hii ni yangu mifano, ipo toka nizaliwe
[/QUOTE]

Hhahhahah

Kwanini utake shari uongo kuendekeza..
Hayo yote ulosema naona kama kengeza..
Kama yupo moyoni mengi utatekeleza..
Sio lazima umweleze ya uongo yaso tija!

Kama mapenzi ya mama na mwana yanavyokwenda...
Sio lazima amweleze kwa mengi anavyompenda...
Vitendo pekee vyatosha kuonyesha yake ajenda..
Sio lazima mwelezane ya uongo yaso tija!
 
Fellow tablet,

Unaweza kunipa sababu tatu kuu kwanini hili liyuziful sredi lilinipita namna hii?

Ngoja nikaanze peji ya kwanza!
hehehe fellow tablet bana hata mimi nilishangaa, weka vitu bana tulitungue "bundi la mwanakijiji"
itakuwa mods tu waliweka kauzibe
 
Nauliza klorokwini, Jibu hutaki nipea,
kwako nimekosa nini, hutaki kuniambia?
Siredi liko jamvini, ODM sijajua?
Kwanini hukunambia, kuna sredi umerusha.

Unajua yangu fani, ni kama ya kwako pia,
Tunapoingia vitani, Utengano twachelea,
Leo imekuwa gani, umesusa kunambia?
Kwanini hukunambia, kuna sredi umerusha?
 
hehehe fellow tablet bana hata mimi nilishangaa, weka vitu bana tulitungue "bundi la mwanakijiji"
itakuwa mods tu waliweka kauzibe

Hahahaha Fellow tableti bana...

Bundi la mwanakijiji, limekwisha kufulia,
Lalegea kama uji,Ambao umesha poa,
Halina wala kipaji, kuimba wala kulia,
Mamodi wakizibia, tamwambia invizibo
 
Hhahhahah

Kwanini utake shari uongo kuendekeza..
Hayo yote ulosema naona kama kengeza..
Kama yupo moyoni mengi utatekeleza..
Sio lazima umweleze ya uongo yaso tija!

Kama mapenzi ya mama na mwana yanavyokwenda...
Sio lazima amweleze kwa mengi anavyompenda...
Vitendo pekee vyatosha kuonyesha yake ajenda..
Sio lazima mwelezane ya uongo yaso tija![/QUOTE]

Mapenzi nayo huchoka, kama ilivyo ada
Kwa chombezi kutamka, penzi walipaka poda
Upya litatakasika, utaziona faida
Daima taimarika, huu wangu ushuhuda

Kila kitu kiloumbwa, chahitaji karabati

Maneno yaliofumbwa, ni penzi miliki hati
Kwa uzuri yakirembwa, maisha ni tanashati
Dhoruba halitokumbwa, love within your heart

Penzi bila uongo, liko doro nakwambia

Hata hizo isidingo, haya zayasimulia
Mkeo ana mapengo, vipi utamsifia?
Hapo utatunga tungo, hali yake kuridhia.
 
Nauliza klorokwini, Jibu hutaki nipea,
kwako nimekosa nini, hutaki kuniambia?
Siredi liko jamvini, ODM sijajua?
Kwanini hukunambia, kuna sredi umerusha.

Unajua yangu fani, ni kama ya kwako pia,
Tunapoingia vitani, Utengano twachelea,
Leo imekuwa gani, umesusa kunambia?
Kwanini hukunambia, kuna sredi umerusha?

Kwanini walalamika wakati macho unayo..
Eti wataka julishwa wakati simu kimeo...
Ungekua umestaafu ungeshakosa mafao..
Kloro endelea tuone yako mazao!
 
Hahahaha Fellow tableti bana...

Bundi la mwanakijiji, limekwisha kufulia,
Lalegea kama uji,Ambao umesha poa,
Halina wala kipaji, kuimba wala kulia,
Mamodi wakizibia, tamwambia invizibo

Tena hakuonekana, bundi ulipogundua
Ukweli hakuukana, kusepa aliamua
Kijana matata sana, gwiji limekukimbia
Watu wanaulizana , fani ameisusia?
 
Back
Top Bottom