To You..

Kwa hiyo kwa kifupi: Hili sredi liko klozdi au watu wameishiwa vina tuanzisha bongo fleva?
 
Kwa hiyo kwa kifupi: Hili sredi liko klozdi au watu wameishiwa vina tuanzisha bongo fleva?

Maneno yako yaonyesha kwa vina unefilisika..
Baada ya kumsema MM na wewe umefulia..
Mbwembwe zimekuishia huna pa kukimbia..
Umebaki kuuliza wapi vina wapi vina!
 
bado sie tunashuka,kwa vina pia virazi,
kama wewe si mshuka,nenda kale maviazi,
Klorokwini mwa eka,nipe babe la azizi,
Karibu mwana karibu,tule tunda mwana iri,

Aspirini kasema,malaria yake sugu,
samunge hata kigoma,haitoisha usugu,
kama mapenzi zahama,sitaje magulumangu,
karibu mwana karibu,tule tunda mwana iri,
 
Maneno yako yaonyesha kwa vina unefilisika..
Baada ya kumsema MM na wewe umefulia..
Mbwembwe zimekuishia huna pa kukimbia..
Umebaki kuuliza wapi vina wapi vina!

hafirisiki jamani,sema yeye masikini,
mbwembwe zake sakafuni,za panya ndio mwishoni,
mwanakijiji shambani,kafulia vya mjini,
Vinani sio tajiri,muache jama muache,
 
Maneno yako yaonyesha kwa vina unefilisika..
Baada ya kumsema MM na wewe umefulia..
Mbwembwe zimekuishia huna pa kukimbia..
Umebaki kuuliza wapi vina wapi vina!

Na huyu ndie Lizzi, kajibu bila kusita
Kimwana hana mapozi, aitika ukimwita
Hata kama kwa herizi, iko siku nitampata
Ingawa ana walinzi , tamaa sijaikata.

Mwambie akusikie, Aspirin ni babu
Mistari mrushie , ashindwe hata kujibu
Mwishowe akukimbie, au kwako aje tubu
Vina sisi vituishie ?, hii kwetu ni aibu.

Khaaaa!
 
bado sie tunashuka,kwa vina pia virazi,
kama wewe si mshuka,nenda kale maviazi,
Klorokwini mwa eka,nipe babe la azizi,
Karibu mwana karibu,tule tunda mwana iri,

Aspirini kasema,malaria yake sugu,
samunge hata kigoma,haitoisha usugu,
kama mapenzi zahama,sitaje magulumangu,
karibu mwana karibu,tule tunda mwana iri,

Magulu mwana wa mangu, pacha wangu kwenye fani.
Gwiji la tangu na tangu, kwenye fani sultani.
Waswahili kwa wazungu, tuwawekee mizani
Weka niweke kirungu , JF furahani.

Kuishiwa kwetu mwiko, hilo liwazi daima
Mashairi na vituko , tunazishinda sinema
Haliukosi ukoko , Jungu kuu walisema
Sio huku wala huko, washindi tutasimama.
 
Vinani tuna vinani,virazi tuna viraza,
kama vipi kina nani,isiwe wao viraza,
asipirini mnani,acha mpaka kibaraza,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

nakujua veve mwana,kwa kihindi ninanena,
ita ile veve bana,jaribu iba pajana,
saidia yote kana,ita inji zenu gana,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

sasa narudi kikwetu,wabeja nangho namhala,
shinyanga mpaka meatu,vina hata mwamala,
naliho kunhu gwaitu,nzugu nangho ngwana nzila,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

Siishi kilimanjaro,wanakotoka warangu,
lizzy kwao Tairo,mwambie aje namangu,
mpe vina kimaro,mangi meru jina langu,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

Tupite kwa wamasai,yero eva lugha yao,
wanyiramba maksai,singida mkoa wao,
sina mengi ila ai,wote waende makwao,

Simama mimi na wewe,vinani lizzy na yupo,
kama kashindwa ni mawe,kwetu hilo ni malipo,
rukaruka kwa haragwe,kuiva kwake na kupo,
Vina vikiisha kwetu,ni mwisho wake malenga,

liwazi daima hilo,klorokwini wasemaa,
asipirini mwailo,daraja kwetu daima,
first lady kitalo,kasema bila lawama,
Vina vikiisha kwetu,ni mwisho wake malenga,
 
Code:
Natamani kuwa nawe, sekunde kila dakika
Liwalo acha na liwe, moyoni nimekuweka
Mola acha asifiwe, alokuumba ukaumbika
Daima mimi na wewe, wazi wazi natamka

Maria Roza haya kweli 7atoka moyoni au kumhadaa tu mtu wa watu........................
 
Vinani tuna vinani,virazi tuna viraza,
kama vipi kina nani,isiwe wao viraza,
asipirini mnani,acha mpaka kibaraza,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

nakujua veve mwana,kwa kihindi ninanena,
ita ile veve bana,jaribu iba pajana,
saidia yote kana,ita inji zenu gana,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

sasa narudi kikwetu,wabeja nangho namhala,
shinyanga mpaka meatu,vina hata mwamala,
naliho kunhu gwaitu,nzugu nangho ngwana nzila,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

Siishi kilimanjaro,wanakotoka warangu,
lizzy kwao Tairo,mwambie aje namangu,
mpe vina kimaro,mangi meru jina langu,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

Tupite kwa wamasai,yero eva lugha yao,
wanyiramba maksai,singida mkoa wao,
sina mengi ila ai,wote waende makwao,
Vina kwetu ndo nyumbani,nchini kwetu vinani,

Ukurasa umefunga, sina la kuongezea
Lugha ulivyozipanga, hakuna wa kupangua
Fasaha bila ya chenga, kiziwi angesikia
Cheo chako ni malenga, leo twakitangazia

Umesahau kingereza, you are really a star
Grammar nikiteleza , please forgive me sir
Lizzy asijenibeza , I dont wanna loose her
Fani nisijedumaza, give me one tusker!

Kwa lugha za kijiwen, mwaga razi jibaba
Mchovu katinga tawn, analeta za kizoba
Tulimpa hamsin , akauza mkoba
Tutapaisha spain, pipa boda la bukoba

Tuko gado kinoma, wazembe si walifuja
Walileta za sodoma, tukawapa za kisolja
Ishu tumeshaifuma, mwaka huu tutachuja
Mkwanja watautema, hatuuzi reja reja

Acha sasa nilipoze, ngeli ziko mwake mwake
Mnyamwezi niko bize, si unajua babaake?
Nipe tano mchize!, tukomae kieleweke
Volt kali wasichezee, anomaind kivyake
 
Kwa hiyo kwa kifupi: Hili sredi liko klozdi au watu wameishiwa vina tuanzisha bongo fleva?[/QUOTE]
hehehe fellow tablet bana! hivi kandabongo man alifariki? tukiona hakieleweki tutaingia anga za inde monieee, inde moniee! kumba ee kumba. Dah! kumbe nipo JF?. khaaa!
 
Kloro sio wanasemaga inde moniee mwana mamaa???!

Heehe asante kwa kunifurahisha hapo juu!!Ngoja nijipange kushusha mistari ya ukweli!!
 
Maneno yako yaonyesha kwa vina unefilisika..
Baada ya kumsema MM na wewe umefulia..
Mbwembwe zimekuishia huna pa kukimbia..
Umebaki kuuliza wapi vina wapi vina!

Mimi babu niko juu, maneno yezi nishia,
Hiki ni chuo kikuu, cha vina na mizania,
Hili ndilo jungu kuu, ukoko wapi kosea,
Hima nitake radhi, Kabla sijakasirika.
 
bado sie tunashuka,kwa vina pia virazi,
kama wewe si mshuka,nenda kale maviazi,
Klorokwini mwa eka,nipe babe la azizi,
Karibu mwana karibu,tule tunda mwana iri,

Aspirini kasema,malaria yake sugu,
samunge hata kigoma,haitoisha usugu,
kama mapenzi zahama,sitaje magulumangu,
karibu mwana karibu,tule tunda mwana iri,
Ndugu Magulumangu, hakika wanionea,
Muogope japo Mungu, kwa haki kunitendea,
Unanipaka majungu, mimi sugu malaria?
Vina hapa ndiyo kwake, Mizani ni yangu fani.

Mimi nikale viazi, nani atakunywa bia?
Mie silagi mizizi, vinywaji navishushia,
Tena bila ya ajizi, na minyama nashushia,
Kwa vina hapa mefika, Na mizani yake pia.
 
Na huyu ndie Lizzi, kajibu bila kusita
Kimwana hana mapozi, aitika ukimwita
Hata kama kwa herizi, iko siku nitampata
Ingawa ana walinzi , tamaa sijaikata.

Mwambie akusikie, Aspirin ni babu
Mistari mrushie , ashindwe hata kujibu
Mwishowe akukimbie, au kwako aje tubu
Vina sisi vituishie ?, hii kwetu ni aibu.

Khaaaa!

Kamwe haujakosea, Asipirini ni babu,
Babu aliyekomaa, Babu aso na aibu,
Wajukuu wanajua, nilivyopiga kitabu,
Babu ashindwe kujibu, Kumbe nani ataweza?

Nasema tena na tena, Narudia tena tena,
Tena na tena na tena, na kwa msisitizo tena,
Babu asisemwe tena, asikasirike tena,
Tena na tena nasema, Nidhamu irudi tena.
 
Back
Top Bottom