To You..

Heshima mbele mkuu Big Braza ODM,wiselady ana admit kuwa amekumiss mbaya......... :hug:

Nami pie mekumisi,
Weziledi wangu miss,
Sijabakiza kipisi,
Nakumisi hata kiss.

Kwa msisitizo nakurusha na bongofleva kabisa.

Sasa huyu ndo wiselady sasa,
Huyu ndo yule babu ampenda sasa,
Asipomwona babu anahisi kufa,
Hebu njoo mama babu apate pona....
njoo kando yangu hapa,
Njoo nipe mahaba hapa

Rukeni wote, imbeni wote kule pigeni makofi kwa pamoja
pwapwapwapwapwa....pwaaa!
Tumshukuru Mungu kwa zawadi hii,
Wiselady ni ua la zawadi toka kwa Mungu Baba
.

Waizled avoumbika babu akimwona anawehuka,
Mzuri kama kasuku atembeaye ikulu,
Mungu kampendelea kampa rangi husu,
Umbo la kiafrika sura ya malaika,
Akipita njia wanaume mimacho,
wanamwangalia Wiselady wa babuuuuu.

Rukeni wote, imbeni wote kule pigeni makofi kwa pamoja
pwapwapwapwapwa....pwaaa!
Tumshukuru Mungu kwa zawadi hii,
Wiselady ni ua la zawadi toka kwa Mungu Baba.
 
Today 07:35 AM
WiseLady
JF Premium Member
This message has been deleted by WiseLady.

Na hapa ulikuwa umeandika nini Wise the Lady?
 
Nami pie mekumisi,
Weziledi wangu miss,
Sijabakiza kipisi,
Nakumisi hata kiss.

Kwa msisitizo nakurusha na bongofleva kabisa.

Sasa huyu ndo wiselady sasa,
Huyu ndo yule babu ampenda sasa,
Asipomwona babu anahisi kufa,
Hebu njoo mama babu apate pona....
njoo kando yangu hapa,
Njoo nipe mahaba hapa

Rukeni wote, imbeni wote kule pigeni makofi kwa pamoja
pwapwapwapwapwa....pwaaa!
Tumshukuru Mungu kwa zawadi hii,
Wiselady ni ua la zawadi toka kwa Mungu Baba
.

Waizled avoumbika babu akimwona anawehuka,
Mzuri kama kasuku atembeaye ikulu,
Mungu kampendelea kampa rangi husu,
Umbo la kiafrika sura ya malaika,
Akipita njia wanaume mimacho,
wanamwangalia Wiselady wa babuuuuu.

Rukeni wote, imbeni wote kule pigeni makofi kwa pamoja
pwapwapwapwapwa....pwaaa!
Tumshukuru Mungu kwa zawadi hii,
Wiselady ni ua la zawadi toka kwa Mungu Baba.

hahahaha! ODM swithat,c unajua mimi cjui vina?nashindwa kukujibu kwa vina!kloro akija ntamuajiri anitungie shairi la aspro,kama kawaida umeniongezea siku.. :hug:
 
babu watu vina vimeshaisha

Vina bado vijaisha, Hakika nakuambia,
Vina ni yao maisha, Hawa naokutajia.
Klorokwini anatisha, Kunaye na lizzy pia,
Vina havijatuisha, majukumu yamebana.

Tunaye Magalumangu, Vina mejaa kichwani,
Kipaji kampa Mungu, Kamleta kwenye fani,
Ukija na hapa kwangu, Vimejaa ubongoni,
Vina havijatuisha, Majukumu yamebana

Mwanajamii wani, Acid nakutajia,
Ni magwiji kwenye fani, muda umewabania,
Mwanakijiji kundini, Teamo anafwatia,
Vina havijatuisha, Majukumu yamebana.
 
Mimi babu niko juu, maneno yezi nishia,
Hiki ni chuo kikuu, cha vina na mizania,
Hili ndilo jungu kuu, ukoko wapi kosea,
Hima nitake radhi, Kabla sijakasirika.
Hehehheh

Hata usipokubali wote twajua umeishiwa..
Msamaha siwezi omba maana sijakosea..
Hata Magulu wangu mjomba anaweza kunitetea..
Babu kubali jamani fani na utuachie!

Uzee umeshakusonga macho yameisha kuona..
Wino wako umemaliza ila bado wang‘ang‘ana..
Ngazi hutaki achia wajukuu tupambane..
Babu kubali jamani ngazi na utuachie!
 
Babu atakubalije, wakati wamuonea?
Hapa na itakuwaje, mna gani naye nia,
Uzee hata uweje, Vina viwezi potea,
Katu babu hakubali, babu bado anaweza.

Babu ameshakomaa, ujuzi umemjaa,
Kujitoa hana nia, ukweli hataridhia,
Hoja zenye manufaa, babu bado anatoa,

Sasa fani imenoga, manguli wajibizana
Ikulu Lizzy kagonga, Aspirin katafuna
Nyote nyinyi ni malenga, Hamuishiwi na vina
Sasa mbele tunasonga, lugha ni yetu hazina

Babu watu wakubipu, tuliza bana mzuka
Hata utamu wa supu, ni chumvi ukiiweka
Suruali bila zipu , ina tabu kufunguka
Sasa ni yako tripu, kujibu kakubalika

Wengi wanakutambua, hii fani iko kwako
Ila wanakudonoa, umwage makeke yako
Sasa ukumbi tumia, simpe Lizzy kicheko
Namimi nashuhudia, nani apewe upako?
 
Ndugu yangu klorokwini, Lizzy ananichuria,
Ananitoa jamvini, kisa vina mefulia,
Hawezi nitoa ndani, hakika nakuapia,
Hili ndilo jamvi letu, hakuna wa kututoa.

Ha! Ha! Ha! acha nicheke, Nikachekee chumbani,
Hakika una mikeke, maneno mashairini,
Zipu ni mahali pake, kuwekwa surualini,
Ukipata haja ndogo, wamaliza fastafasta.

Ombi moja nakuomba, Fikisha wangu ujumbe,
Ukawe kama mjomba, na wala siyo mpambe,
Lizzy aje kuniomba, samahani na mjumbe,
Kwa kashfa alonipamba, Nitamchapa mangume.

Ushairi yangu fani, Nimepewa naye Mungu,
Vina hata na mizani, Navipanga kwa mafungu,
Kama wongo unadhani, Mulize Magalumangu,
Mashairi yangu ndani, kipaji hiki ni changu.
 
Hehehheh

Hata usipokubali wote twajua umeishiwa..
Msamaha siwezi omba maana sijakosea..
Hata Magulu wangu mjomba anaweza kunitetea..
Babu kubali jamani fani na utuachie!

Uzee umeshakusonga macho yameisha kuona..
Wino wako umemaliza ila bado wang‘ang‘ana..
Ngazi hutaki achia wajukuu tupambane..
Babu kubali jamani ngazi na utuachie!

Babu atakubalije, wakati wamuonea?
Hapa na itakuwaje, mna gani naye nia,
Uzee hata uweje, Vina viwezi potea,
Katu babu hakubali, babu bado anaweza.

Babu ameshakomaa, ujuzi umemjaa,
Kujitoa hana nia, ukweli hataridhia,
Hoja zenye manufaa, babu bado anatoa,
Katu babu hakubali, babu bado anaweza.

Ndugu yangu klorokwini, Lizzy ananichuria,
Ananitoa jamvini, kisa vina mefulia,
Hawezi nitoa ndani, hakika nakuapia,
Hili ndilo jamvi letu, hakuna wa kututoa.

Ha! Ha! Ha! acha nicheke, Nikachekee chumbani,
Hakika una mikeke, maneno mashairini,
Zipu ni mahali pake, kuwekwa surualini,
Ukipata haja ndogo, wamaliza fastafasta.

Ombi moja nakuomba, Fikisha wangu ujumbe,
Ukawe kama mjomba, na wala siyo mpambe,
Lizzy aje kuniomba, samahani na mjumbe,
Kwa kashfa alonipamba, Nitamchapa mangume.

Ushairi yangu fani, Nimepewa naye Mungu,
Vina hata na mizani, Navipanga kwa mafungu,
Kama wongo unadhani, Mulize Magalumangu,
Mashairi yangu ndani, kipaji hiki ni changu.

hehe lizzy asikusumbue, mpatie yake dozi
Hawa viumbe ujue , wana mbinu za mapenzi
Aweza akuchukie, kumbe ndani hajiwezi
Wewe endelea nae, wala sifanye ajizi

Ninaiona mikwara, anayochimba jamvini
Mimi sina papara, iko siku nitawini
Ninayo ya veto kura,hanishindi asilani
Ataruka kama chura, nasubiri mtegoni

Ujumbe nitafikisha, lengo likikamilika
Kwasasa nitachemsha, kijifanya kibaraka
Ila tamfahamisha , fani hii wewe kaka
Akileta za kubisha, ushahidi tutaweka
 
Babu atakubalije, wakati wamuonea?
Hapa na itakuwaje, mna gani naye nia,
Uzee hata uweje, Vina viwezi potea,
Katu babu hakubali, babu bado anaweza.

Babu ameshakomaa, ujuzi umemjaa,
Kujitoa hana nia, ukweli hataridhia,
Hoja zenye manufaa, babu bado anatoa,
Katu babu hakubali, babu bado anaweza.

Heshima natanguliza kabla ya kuendelea..
Siwezi muonea babu maana ndo alonilea...
Baada ya kukusikiliza nakuomba rejea..
Nisamehe mjukuu kukukwaza haikua nia.

Utupe yako mafunzo kwa kichwa yalolemea..
Utupe na mashauri wajukuu tusijepotea..
Njoo babu njoo mkongojo nakuletea...
Umpe somo Kloro aache kunimendea!!

Kloro i'll be back....
 
Hiyo kinga ya babu, haitokusaidia
Hebu fanya unijibu, nilichokielezea
Mimi ndo wako tabibu, unabishia?
Njoo upate zabibu , ninakungojea.
 
Back
Top Bottom