To You..

Ukuu ninaukana, hilo si daraja langu
Ni sifa ya maulana, mjuzi wa toka tangu
Niepushie laana, wewe kimbilio langu
Mapenzi haya ya sasa, akili kichwani mwako


Mapenzi haya ya leo, yana mingi mitihani
watu wapenda vileo, nafsi zi mashakani
Tumekosa mwelekeo,bora yale yazamani
mapenzi haya ya sasa,akili kichwani mwako


Mimi sintodanganya, sababu eti ni penzi
sitaki kujichanganya, siwezi nunua benzi
mapesa sintotawanya, naogopa utelezi
mapenzi haya ya sasa, akili kichwani mwako






Mkuu umekubalika, katika hii hii fani
Mistari imetukuka, tukuite namba wani?
Mwenyewe nimetishika, Naogopa kusaini
Kwangu usiwe na shaka, najipa matumaini

Mapenzi ni usanii, babu aliniusia
Jifanye kuwa mtii, mapenzi kukumbatia
Lakini yakikuudhii, haraka mbele timua
Mapenzi ni ulaghai, Lugha tamu kutumia

Nikisema sili sinywi, hivi nitaishi vipi?
Ila kama hadanganywi, atakuthamini vipi?
Atakuona nyang'anywi, takataka za makapi
Lugha mapenzi haifinywi, Hata nepi yaitwa chupi.
 
Klorokwini watisha

1. Klorokwini u bingwa, kwenye fani uko juu
Hakuna anayepinga, na tena huna makuu
Mistari waipanga, twapenda zako nukuu
Klorokwini watisha

2. Wachache mlo bakia, wataalamu wa fani
Twaomba usije kimbia, twazipenda zako ghani
Yalo mema simamia, uzidishe burudani
Klorokwini watisha

3. Ghani zako ni makini, tena zinapendeza
Siuoni ulakini, kweli zajitosheleza
Wang'ara humu kundini, wengi zawabembeleza
Klorokwini watisha

4. Hii si fani ya wote, wachache mna vipaji
Sisemi wajua yote, ila nakuvisha taji
Tuongoze sasa sote, mwenzetu una kipaji
Klorokwini watisha

5. wanikumbusha kandoro, gwiji yule wa zamani
Hutomtoa kasoro, alikuwa namba wani
Ongeza kasi kloro, usiwe na mpinzani
Kloro watisha
 
Ukuu ninaukana, hilo si daraja langu
Ni sifa ya maulana, mjuzi wa toka tangu
Niepushie laana, wewe kimbilio langu
Mapenzi haya ya sasa, akili kichwani mwako


Mapenzi haya ya leo, yana mingi mitihani
watu wapenda vileo, nafsi zi mashakani
Tumekosa mwelekeo,bora yale yazamani
mapenzi haya ya sasa,akili kichwani mwako


Mimi sintodanganya, sababu eti ni penzi
sitaki kujichanganya, siwezi nunua benzi
mapesa sintotawanya, naogopa utelezi
mapenzi haya ya sasa, akili kichwani mwako

Nashika tena kalamu, kujibu lako shairi
Wewe ni mtaalamu , hata kama hujakiri
Vina vyako ni vitamu, nakubali sio siri
vimesheheni nidhamu, si vya kikiri kikiri

Msimamo wa mapenzi, ulonao ni mzuri
Ila hayo ni ya enzi , zama hizo za zaburi
Siku hizi ni utenzi , mapenzi yapo sifuri
Wathaminiwa kwa jinzi, wapuuzwa kwa msuri

Hata hao wazamani, sasa wamebadilika
Ya sasa wayatamani, muda umeshawatoka
Kibibi chavaa mini , kibabu nacho chabaka
Sana ukitathmini , kichwa kitakupasuka.

Kubali kwenda na muda, unusuru afya yako
Kuna tigo pia voda , huku ndiko tuendako
Pombe inaitwa soda, umalaya ni ujiko!
kiwa mkweli utadoda, uishie sikitiko .
 
Klorokwini watisha

1. Klorokwini u bingwa, kwenye fani uko juu
Hakuna anayepinga, na tena huna makuu
Mistari waipanga, twapenda zako nukuu
Klorokwini watisha

2. Wachache mlo bakia, wataalamu wa fani
Twaomba usije kimbia, twazipenda zako ghani
Yalo mema simamia, uzidishe burudani
Klorokwini watisha

3. Ghani zako ni makini, tena zinapendeza
Siuoni ulakini, kweli zajitosheleza
Wang'ara humu kundini, wengi zawabembeleza
Klorokwini watisha

4. Hii si fani ya wote, wachache mna vipaji
Sisemi wajua yote, ila nakuvisha taji
Tuongoze sasa sote, mwenzetu una kipaji
Klorokwini watisha

5. wanikumbusha kandoro, gwiji yule wa zamani
Hutomtoa kasoro, alikuwa namba wani
Ongeza kasi kloro, usiwe na mpinzani
Kloro watisha

Mengi uliyoyasema , nami ninayathamini
Shukrani ewe mwema, ulonipa tumaini
Ni nyingi zako hekima, shairi limesheheni
Namuomba karima , akuweke furahani

Ubingwa ulionipa, nauvua hapa hapa
Taji lako ninakupa, kwako nimetoka kapa
Vina nimevipa chapa, "yakuonea" uko supa
Shairi hili ni kopa , burudani umetupa

Cheo chako kiko juu, siwezi kukufikia
Uwanja wako ni huu, wengine tunadandia
Twaiga zako nukuu, kwengine twazitumia
Bahari yako buluu, fani waiogelea.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mengi uliyoyasema , nami ninayathamini
Shukrani ewe mwema, ulonipa tumaini
Ni nyingi zako hekima, shairi limesheheni
Namuomba karima , akuweke furahani

Ubingwa ulionipa, nauvua hapa hapa
Taji lako ninakupa, kwako nimetoka kapa
Vina nimevipa chapa, "yakuonea" uko supa
Shairi hili ni kopa , burudani umetupa

Cheo chako kiko juu, siwezi kukufikia
Uwanja wako ni huu, wengine tunadandia
Twaiga zako nukuu, kwengine twazitumia
Bahari yako buluu, fani waiogelea.

...aiseee!...braza you are multi talented bana!
Lyrics zako zimetulia kuliko za hawa Bongo fleva
 
...aiseee!...braza you are multi talented bana!
Lyrics zako zimetulia kuliko za hawa Bongo fleva
hehehe senks Mzee Moskwito aisee. Halaf mbona unaonekana kimachale au zali limeclick?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom