To You..

kwa vina hivo klorokwini lazima uopoe kimwana JF...afu wanajiletaga wenyewe... Nakuonea wiiiiivuuuuu
 
Vina bado vijaisha, Hakika nakuambia,
Vina ni yao maisha, Hawa naokutajia.
Klorokwini anatisha, Kunaye na lizzy pia,
Vina havijatuisha, majukumu yamebana.

Tunaye Magalumangu, Vina mejaa kichwani,
Kipaji kampa Mungu, Kamleta kwenye fani,
Ukija na hapa kwangu, Vimejaa ubongoni,
Vina havijatuisha, Majukumu yamebana

Mwanajamii wani, Acid nakutajia,
Ni magwiji kwenye fani, muda umewabania,
Mwanakijiji kundini, Teamo anafwatia,
Vina havijatuisha, Majukumu yamebana.


sema mwana sema,kati weka songa mbele,
nilizani wewe kihema,kosa ni langu milele,
samahani mwana nasema,kamwe si kihelehele,
Vina kwetu vikiisha,gamba na tutalivua,

Sante mwana kunirusha,hapo yote kumi juu,
nilianzia upusha,sione sa niko juu,
kamwe sijapata gusha,twende mambo juu,
Vina kwetu vikiisha,gamba na tutalivua,

Wanitajia asidi,kwa fani ndie kuwadi,
umemsahau judi,mwadada asi miadi,
mwanajamii kinadi,klorokwini sinadi,
Vina kwetu vikiisha,gamba na tutalivua,

mimi sie sharobaro,wala yule wake wema,
kwangu wale ni viharo,mwadui mpaka kahama,
kwa arumasi vinaro,dhahabu hadi kiama,
Vina kwetu vikiisha,gamba na tutalivua,

acha nirushe miaki,kwako mwana wa heri,
nipe stari mikiki,kloro rusha shairi,
pagawisha mpaka diki,afe asiye himiri,
Vina kwetu vikiisha,gamba na tutalivua,
 
Hehehheh

Hata usipokubali wote twajua umeishiwa..
Msamaha siwezi omba maana sijakosea..
Hata Magulu wangu mjomba anaweza kunitetea..
Babu kubali jamani fani na utuachie!

Uzee umeshakusonga macho yameisha kuona..
Wino wako umemaliza ila bado wang‘ang‘ana..
Ngazi hutaki achia wajukuu tupambane..
Babu kubali jamani ngazi na utuachie!

Lizzy mama nakumisi,zawadi yako mezani,
watoto walopromisi,ya mama siku yajani,
kwangu mama una kesi,kutulizia tandani,
Babu kaachia ngazi,njoo uwanja ni wetu,

wino wake ni hafifu,kwishneli ninasema,
mwache awe mtiifu,kwa bibi mzaa mama,
kamwe hakuwa dhaifu,alishusha dinadama,
Babu kaachia ngazi,njoo uwanja ni wetu,
 
Sasa fani imenoga, manguli wajibizana
Ikulu Lizzy kagonga, Aspirin katafuna
Nyote nyinyi ni malenga, Hamuishiwi na vina
Sasa mbele tunasonga, lugha ni yetu hazina

Babu watu wakubipu, tuliza bana mzuka
Hata utamu wa supu, ni chumvi ukiiweka
Suruali bila zipu , ina tabu kufunguka
Sasa ni yako tripu, kujibu kakubalika

Wengi wanakutambua, hii fani iko kwako
Ila wanakudonoa, umwage makeke yako
Sasa ukumbi tumia, simpe Lizzy kicheko
Namimi nashuhudia, nani apewe upako?

lizzy kamwaga mboga,aspirini ugari,
mimi nitamwaga chenga,tuone nani sukari,
klorokwini malenga,kwa vina na mistari,
Bongo flava ni wezi,waiselady tulia,

kamwe usije mdipu,babu lazima apige,
Tigo voda yeye kipu,ukome mpaka uringe,
salimia yule taripu,mwambie nipo samunge,
Bongo fleva ni wezi,waiselady tulia,
 
Back
Top Bottom