TLC vs LG

Mkuu nimenot kitu hapo. Umesema MKV inatumika kwenye piracy. HOW na ni format gani nyingine amabazo sio official recognized.
siku hizi baadhi ya makampuni makubwa yameanza kuitambua mkv, mfano microsoft kweny windows 10 ame add support ya mkv native bila kutumia 3rd party software kama vlc, ila bado safari ni ndefu. kuna makampuni makubwa mengi tu kama Apple, makampuni ya movies etc bado hawana time na mkv.

kivipi mkv inatumika kwenye piracy? unatakiwa ujue hizi mp4, avi, mkv etc unazoziona mbele ya jina la video sio format za video bali ni macontainer tu. yenyewe ndani ndio yanahifadhi video, audio, subtitle etc. container la mkv linakubali almost video format yoyote ile na audio yoyote ile na idadi yoyote ile.

leo naweza download movie torrent ikawa na audio halisi mfano kingereza, halafu ikawa na audio zaidi, kirusi, kichina, kihindi etc utaona kwa mbele ya movie wanaadika neno kama dual audio, mambo haya yanawezekana kwa mkv.

na unaweza ukakuta video ya mkv ina audio kali sana, pengine lossless ambayo hio audio isingewezekana kuwekwa kwenye mp4.

mp4 yenyewe kila video au audio inayokaa kwenye container lake lazima iwe imekuwa defined na MPEG. huwezi kujiamulia.

vitu vingi vya piracy kwenye movies vinatokana na rips, mtu ananunua cd kisha anairip kwenye computer yake na kuisambaza online watu wadownload. wanaorip wengi wanaprefer uhuru wa kutumia video/audio/subtitle format anayoitaka yeye hivyo kupelekea kutumia zaidi mkv.

tofauti na mkv zipo format nyengine za macontainer kama avi, mov na mp4 ila hizi sio maarufu kwenye piracy kama mkv.
 
Mkuu nimekupata vizur sana. Nna muvie fulan ni format ya MKV ina 500Mb na ina saa moja na nusu na inaonesha HD quality kitu ambacho ni cha ajabu.

Asante kwa kunielewesha.
 
Umuuzie jamaa angu kitu cha kueleweka sasa ili afurahie pesa yake, sio copy ya mzigo mtaftie kazi OG toka malaysia.
Nicheki 0658 18 47 97 unapata mpya na free delivery kama upo dar. Mkoan tunatuma buree
 
Mkuu nimekupata vizur sana. Nna muvie fulan ni format ya MKV ina 500Mb na ina saa moja na nusu na inaonesha HD quality kitu ambacho ni cha ajabu.

Asante kwa kunielewesha.
kuhusu mb kidogo pia inaweza kusababishwa na format ya video sasa. ndani ya mp4 au mkv kuna format za video kama x264 au x265, hii 265 ni mpya na mikononi mwa mtaalamu wa kurip atakutolea video ndogo hadi utashangaa. kuna kipindi cha marehemu kat kuna uploader walikuwa wanaweka episode za HD mb 80 mpaka 150. na movies hadi mb 300 mpaka 400 za HD.
 
Hio kitu nshakutana nayo mara kadhaa hadi nikawa nashangaa yani imewezekanaje. Coz movie ya resolution ya HD ikiwa ni .mp4 blu ray rip inaweza kuwa kati ya 700MB mpaka 1GB na kwa full hd ikawa kati ya 1.3GB mpaka 3GB maranyingi.

Ila kwa format ya .mkv unaweza kuta resolution ya hd ukaipata kwa 500MB tu na full hd kwa 800MB. Nmekuwa nikijiuliza ni utundu gani umefanyika maana picha ya .Mkv iko clear almost kama tu quality ya .mp4 HD na full HD
 
Tcl ndio nini? TV NI SAMSUNG NA LG...MKOREA MWENYEWE
TCL ndiyo HITACHI wameamua kutumia jina lingine kukimbia waliokuwa wanaowatumia kutengeneza vifaa fake kupitia jina lao.Ndivyo nilivyosikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…