Tinted zinaongeza uhalifu, zipigwe marufuku

Kweli kabisa, tinted noma kwa mengi tu, hasa mabaya.
 
Yaani sijawahi ona uzi wa kizushi kama huu! Mleta mada lazma utakuwa umepigiwa demu na mtu mwenye gari yenye tinted.
 
Kabla sijanunua gari miaka hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam alipiga marufuku matumizi ya tinted katika magari. Kama ilivyo ada katika nchi yetu, amri za aina hii huwa ni maoni ya kiongozi, na si utaratibu wa chombo cha Serikali. Kwa utaratibu huo, baada ya Kamanda huyo kung'atuka, amekuja Bwana Kova na kuachia tinted zitambe kwenye magari. Sasa wengine wanaweka hadi kwenye vioo vya mbele (wind screen). Gari linakuwa kama nyumba inayotembea!
Binafsi napata shida sana hasa ninapoendesha gari na nikawa nataka kuachiana njia na dereva mwenye gari lenye tinted. Mara nyingi huwa simwoni dereva na hivyo sijui nini anachotaka kufanya kwa wakati huo. Matokeo yake kumekuwapo ajali nyingi.
Si hivyo tu, bali hizi tinted zinaongeza uhalifu na mambo mengine machafu kama vile ngono ndani ya magari. Ushauri wangu kwa mamlaka zinazohusika ni kuzipiga marufuku hizi tinted kuingizwa nchini na kutozitumia katika magari.

Haya ni maoni yangu, sijui wengine mnasemaje.

Manyerere

Ushamba kweli mzigo.....! Sasa unatujuza kuwa umenunua gari? Then unatujuza kuwa gari yako haina tinted? Halafu unaona kukereka na tinted za gari za wenzako? Basi toa tamko wewe kuwa nawe hutaki watu waweke tinted! Eti zinaleta uhalifu kama ngono, umeonaje ngono ikifanyika wakati unashuhudia kuwa huwa hata huwaoni madereva kwenye gari zenye kioo tinted?

Ni ushamba pia kufikiri tinted zinawekwa kwenye vioo vya magari tu! Zile kwenye saloon huwa huzioni, nako pia wanaweka kwa ajili ya kufanya uhalifu na ngono?
 
Kabla sijanunua gari miaka hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam alipiga marufuku matumizi ya tinted katika magari. Kama ilivyo ada katika nchi yetu, amri za aina hii huwa ni maoni ya kiongozi, na si utaratibu wa chombo cha Serikali. Kwa utaratibu huo, baada ya Kamanda huyo kung'atuka, amekuja Bwana Kova na kuachia tinted zitambe kwenye magari. Sasa wengine wanaweka hadi kwenye vioo vya mbele (wind screen). Gari linakuwa kama nyumba inayotembea!
Binafsi napata shida sana hasa ninapoendesha gari na nikawa nataka kuachiana njia na dereva mwenye gari lenye tinted. Mara nyingi huwa simwoni dereva na hivyo sijui nini anachotaka kufanya kwa wakati huo. Matokeo yake kumekuwapo ajali nyingi.
Si hivyo tu, bali hizi tinted zinaongeza uhalifu na mambo mengine machafu kama vile ngono ndani ya magari. Ushauri wangu kwa mamlaka zinazohusika ni kuzipiga marufuku hizi tinted kuingizwa nchini na kutozitumia katika magari.

Haya ni maoni yangu, sijui wengine mnasemaje.

Manyerere
Zilopokatazwa mkalaum
 
Back
Top Bottom