Iringa: Polisi yanasa gari dogo iliyowarundika wanafunzi 33

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,804
21,400
  • Wakati Kikosi cha Usalama Barabarani kikiendelea na misako mbalimbali inayosaidia kupunguza ajali za barabarani, mkuu wa kikosi hicho Mkoani Iringa , Mosi Ndozero ameikamata haice iliyyokuwa imejaza wanafunzi 33 wakati uwezo wake ni kubeba abiria 10 hadi 12 tu.

Iringa. Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Iringa, Mosi Ndozero amelikamata gari aina ya Hiece iliyokuwa imejaza wanafunzi 33 wanaosoma katika shule za msingi tatu za Ummusalama, Gangilonga na Mapinduzi zilizopo ndani ya Manispaa ya Iringa na hivyo kuhatarisha usalama wao ikiwa ajali itatokea.

Kutokana na hali hiyo licha ya kumshikilia dereva wa hiece hiyo, ameagiza wazazi na walezi wa watoto hao kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wazazi wengine wanaoruhusu watoto kurundikana kwenye magari za shule kinyume cha taratibu na sheria.

Hiece hiyo ikiwa na tinted imekamatwa jana Aprili 28, 2023 katika maeneo ya Manispaa ya Iringa wakati ikiendelea kuwasambaza wanafunzi hao baada ya kutoka shuleni, majira ya jioni.

Akizungumza na Mwananchi, Ndozero amesema wanafunzi wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri ni abiria kama walivyo abiria wengine hivyo wanayo haki ya kukaa kwenye siti na sio kupakatana jambo linalohatarisha usalama wao.

“Uwezo wa ile gali ni kubeba abiria 12 tu lakini watoto walijazana kiasi cha kukosa hata hewa, hii sio sawa kabisa na kamwe hatuwezi kuruhusu hali hii hata kidogo,” amesema Ndozero na kuongeza; “Nasikitika kuona tunao wazazi ambao hawajui hali wala wajibu wao kwa watoto wao, wanachofanya wao ni kupakia tu watoto kwenye gari bila kujali usalama wala wanasafirije.”

Ameagiza wazazi na walezi wote kuhakikisha watoto wao wanapanda usafiri bora huku akiwaagiza madereva wanaoendesha magari ya shule kusingatia sheria za usalama barabarani.

“Huu tunaita ni ukatikili kwa watoto kwa hiyo wazazi wao watachukuliwa hatua na tutawaelimisha zaidi umuhimu wa kuwahakikishia watoto wao usalama wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri,” amesema.

Alisema kitu kibaya ni kwamba gari inayopakia watoto hao imewekwa tinted kiasi kwamba mtoto akifanyiwa ukatili wa kingono hawezi kuonekana nje wala kubainika.

“Marufuku kupakia watoto kwenye magari tinted, watoto wakifanyiwa ukatili humo hata akipiga kelele hakuna mtu wa kumsikia. Gari hili ni bovu na wala halina utaratibu wa kuonekana kwamba ni lashule. Rai yangu kwa mkoa wa Iringa kwamba ikiwa kuna wazazi hawajui wajibu wao waanze kuujua tangu sasa,” amesema Ndozero.

Alisema ikiwa wazazi na walezi wa watoto hao wakichukuliwa sheria itasaidia kuwafanya wazazi wengine kuwajibika kwa kuhakikisha watoto wanasafiri salama.

Baadhi ya wazazi na walezi waliozungumza na Mwananchi wamesema hawakuwa wakijua kama gari hiyo nyakati za jioni inajaza kiwango cha kushindwa kuwafanya watoto wao wawe hatarini.

“Mie mwanangu huwa karibia wa mwisho kushuka kwa hiyo sikuwa najua kama anajazwa kwen ye gari kiasi hicho. Tunashukuru kwa gari hili kukamatwa na tunaahidi kuwa makini zaidi,” amesema Huruma Kikoti, Mkazi wa Zizi la Ng’ombe, Manispaa ya Iringa.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom