Tinted zinaongeza uhalifu, zipigwe marufuku

Tinted zinaongeza uhalifu, zipigwe marufuku

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Kabla sijanunua gari miaka hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam alipiga marufuku matumizi ya tinted katika magari. Kama ilivyo ada katika nchi yetu, amri za aina hii huwa ni maoni ya kiongozi, na si utaratibu wa chombo cha Serikali. Kwa utaratibu huo, baada ya Kamanda huyo kung'atuka, amekuja Bwana Kova na kuachia tinted zitambe kwenye magari. Sasa wengine wanaweka hadi kwenye vioo vya mbele (wind screen). Gari linakuwa kama nyumba inayotembea!
Binafsi napata shida sana hasa ninapoendesha gari na nikawa nataka kuachiana njia na dereva mwenye gari lenye tinted. Mara nyingi huwa simwoni dereva na hivyo sijui nini anachotaka kufanya kwa wakati huo. Matokeo yake kumekuwapo ajali nyingi.
Si hivyo tu, bali hizi tinted zinaongeza uhalifu na mambo mengine machafu kama vile ngono ndani ya magari. Ushauri wangu kwa mamlaka zinazohusika ni kuzipiga marufuku hizi tinted kuingizwa nchini na kutozitumia katika magari.

Haya ni maoni yangu, sijui wengine mnasemaje.

Manyerere
 
Watu wakifanya ngono ndani ya gari zao,inakuhhusu nini?
Na tint ina ongeza uhhalifu gani?

Labda ungeongelea dereva kutokuona vizurii usiku..
 
Huu mtindo wakuweka tinted wind screen naona unaongezeka kwa kasi hapa Dar, sijawahi kuendesha gari lenye tinted kioo cha mbele labda ningeweza kueleza zaidi..
 
Binafsi napata shida sana hasa ninapoendesha gari na nikawa nataka kuachiana njia na dereva mwenye gari lenye tinted. Mara nyingi huwa simwoni dereva na hivyo sijui nini anachotaka kufanya kwa wakati huo. Matokeo yake kumekuwapo ajali nyingi.
Si hivyo tu, bali hizi tinted zinaongeza uhalifu na mambo mengine machafu kama vile ngono ndani ya magari. Ushauri wangu kwa mamlaka zinazohusika ni kuzipiga marufuku hizi tinted kuingizwa nchini na kutozitumia katika magari.

Haya ni maoni yangu, sijui wengine mnasemaje.

Manyerere
Hebu madereva nisaidieni hapo kwenye red.
Ili uweze kuachiana njia na gari unalopishana nalo ni lazma umwone dereve wa hiyo gari?
 
Nadhani mleta mada kasema kweli. Nani amewahi kukaa pale Mlimani city wakati hasa wa jioni na kujionea kinachoendelea kwenye magari? Pia kwa sasa hizi tinted nyingi zinawabeba waharifu, unakuta mtu katoboa kwenye eneo la kuangalia side mirror the rest iko black, mpaka unajiuliza huyo anasafirisha watoto washule wa kike ama wake za watu au anasafirisha madawa ama ni mharibu maarufu anatafutwa....why all these troubles?
 
kwani tinted zinaTia khofu gani.... au unaendesha bajaji?
 
Tint zilipigwa marufuku ni zile za kungaa kama kioo cha kujitizamia kwani zile zilikuwa zinaficha kila kitu kilichopo ndani tint zilizoruhusiwa ni zile nyepesi zila za kung'aa hata wauzaji walisha acha kuzileta...

Hizi zingine me naziona nipoa tu nikiwa nimebea gash nakuwa huru sana.... Tint Oyeeeeeeee
 
Akili za kitoto hizi. Kitu kikikutia hofu wewe basi kipigwe marufuku!!!
 
Tinted ni uhuru wa mtu binafsi! Hata mtu akiwekea tint hadi kwenye rim its okey cz ni gari yake mazee!
 
Sina hakika jama mleta mada ana gari maana unapopishana na gari nyingine unachotakiwa kuona ni indicator na huna haja ya kumwona dereva . Kila mtu akitaka anachoona hakifai kipigwe marufuku kwenye magari itakuwa kero
 
Zilipigwa marufuku kwa sababu za kiusalama. Kama umetekwa na wazee wa kazi watu wa nje hawawezi kugundua na kutoa msaada
 
Jamaa atakuwa haoni mbali...wacha wenye macho yetu tujisiribe na tnt hadi kwenye side mirror
 
Tinted ni uhuru wa mtu binafsi! Hata mtu akiwekea tint hadi kwenye rim its okey cz ni gari yake mazee!

Wengi wanaoweka tinted ni matapeli, majambazi na wahalifu wa aina nyingine mtu mwenye akili timamu anaweka tinted ya kawaida na siyo full tinted.Usibishe we fanya research utakubali matapeli wote hutumia aina hiyo ya magari.
 
Sasa uhalifu uko wapi, kwenye tinted mirrors au kwenye mioyo ya watu? Nenda kwenye chanzo bwana!
 
Ila ukimpata mke au mume wa mtu ndo utaona raha ya tinted! wanaoiba wake za watu au waume za watu,wanajua ninachomaanisha!!
 
zamani ulipo kuwa unaendesha bodabaoda hukuona tinted ni ttz sasa tajiri yako kakununulia ka sprinter T 004 AAC unanza mbwembwe kama unataka kuweka tinted kwenye hako kamkweche mwambie tu tajiri yako, atakubali kwa jinsi anavyo penda sifa wee msifie tu mwambie tinted ndio fashion ya mjini kwa sasa
 
mie sio dereva mzoefu, ila unapokuwa unakatiza barabara, sehemu ambako hakuna taa, inakuwa rahisi unapokuwa unamwona dereva anaetakiwa kukuachia njia unaelewa kirahis body language kuwa upitae au la
 
Back
Top Bottom