Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,723
Nimeona yanga kwenye mechi ya coastal union nimejiridhisha kwamba msimu huu wamepania kufanya jambo ktk kuupigania ubingwa waliopoteza misimu 3 iliyopita, kuna kauli nazisikia zikisema yanga ilizidiwa umiliki wa mpira na coast lakini asiyeelewa ni kwamba yanga walikwenda mkwakwani wakijua ni pagumu na historia ya pale aikuwa upande wao ivyo walienda kwa taadhari zote kwa plani ya kucheza direct football na sio kuremba.
Kama ilivyozoeleka yanga kwa sasa wanaposess sana mpira lakini kocha nabi anapanga mbinu zake kulingana na timu anayocheza nayo au kiwanja anachochezea, Coastal union walikuwa wamebebeshwa mzigo mzito vichwani mwao kwanza ahadi ya milioni 50 pili presha ya mashabiki wao uwanjani ni vitu vilivyowavuruga Sana kisaikolojia ukizingatia walikuwa wanacheza na yanga ambayo imekuwa na mabadiliko makubwa ndani ya uwanja mpaka nje ya uwanja aikuwa yanga ile ya misimu 4 iliyopita.
Viashiria vya timu inayosaka ubingwa ni kushinda mechi ata Kama timu iyo imecheza vibaya, ata kama imekutana na timu ngumu kinachoangaliwa ni point 3 muhimu na hilo yanga wameshaanza kulionyesha bila shaka.
Ni vizuri timu zinazokwenda kucheza na yanga zikaheshimu ubora wake kwa sasa vinginevyo itaendelea kuvuna point na zile hadithi za kuhonga zitaendelea kwa wale wasiopenda kuukubali ukweli ya kuwa yanga ya sasa iko vizuri kiufundi na aina ya usajili walioufanya ni bab kubwa, inao wachezaji wanaoweza kuamua mechi mda wowote na dk yoyote, Iyo ni tabia ya timu inayocheza kibingwa!
NB: Hoja ujibiwa kwa hoja na sio viroja!