Timu a Polisi vs Magereza Kiteto kuumana leo

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Katika kile kilichoelezwa kuwa ni kijenga mahusiano mema na pia kuendeleza michezo, timu za mpira Jeshi la Magereza na Polisi leo zitakutana kugombea Mbuzi mnyama.

Mbuzi huyo ametajwa kuwa wa thamani ya zaidi ya elfu 80,000/ kama kifuta jasho kwa timu itakayoshinda

Aki,ungumza hayo Fadhili Luoga Mkuu Wa Polisi Kiteto amesema nia ya mashindano hayo ni kuibua bipaji na pia kujenga mahusiano mema kati ya jamii ya wakulima na wafugaji Kiteto

Mbali na mechi hiyo ambayo inatabiriwa kuwa kutakuwa na patashika, timu ya Polisi Kiteto imealika tena kutaka kucheza mchezo Wa kirafiki na timu ya jamii ya kifugaji Maasai

Baadaye pia watacheza na wakulima na mwisho kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya wakulima na wafugaji

Hii itakuwa moja ya njia ya kurejesha mahusiano mema kati ya wakulima na wafugaji ambao kila mwaka wanahasimiana

Wakulima na wafugaji Kiteto bado wanahusiano mabaya kufuatia shughuli za kiuchumi hivyo michezo hiyo inakusudiwa kujenga mahusiano mema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom