Time Travel: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?

Naipenda Sana sayansi ya muda ila inapofikia hapa ndipo ambapo huwa napata kigugumizi!! Waje madaktari hapa watueleze seli inaathirika vipi na mtu kusafiri kwa Kasi ya mwanga.
 
Sio watoto tu na mama yao pia....
Kwani mkuu future tayari ipo?
I mean sasa hivi mimi ambaye hata mke sina kwenye future kuna watoto wangu..
Kwamba mtu akienda future atakuta watoto wangu wakati sina hata mke?
Naona ni easy kwenda past kuliko future maana nahisi future ndio tunaitengeneza sasa hivi haipo tayari
 
Hii story hta Mm nahisi nilishawahi kukasikia vile
Kuna haka kastory niliakandika kitambo kidogo ngoja nikaweke hapa ili tusijaze server za watu . haka kastori kanahusu viumbe wanaokuja duniani kutoka anga za mbali kuja kututembelea.. sometime waweza jiuliza tu kwanini Rc ilibadiri sala ya Mwanakondo uondoae dhambi za dunia kua mwanakondoo uondoae dhambi za ulimwengu! ni kwasababu Teknoljia inazidi kukua pia elimu yazidi kupanuka hivyo wakajua tu haiwezekani katika Ghalaxy yetu ya Milky way yenye solar system zaidi ya 1mil kuwe na binaadamu/viumbe duniani tu.
kastory kenyewe ni haka...
View attachment 1102218
Ilikua july 1954 ambapo maofisa wa wa uwanja wa Haneda Airport(kwasasa Tokyo airport) nchini Japan waliripoti tukio la kushangaza lilitokea uwanjani hapo… Msafiri kutoka Ulaya mwenye pasi ya kusafiria ya nchi iliyokua inaitwa Tuared.

Msafiri huyo alikua namwonekano mwenye ndevu kiasi na mwonekano wa Caucusian kama watu wanaotoka nchi za Ulaya, kwa mujibu wake alisema kua nchi hiyo ya Tuared iko ulaya pia alikua ana fedha za mataifa mbalimbali. Maofisa wa polisi walifikiraia kua watakua na maelezo kidogo tu kuhusu kwanini hawajui nchi hiyo ilipo hivyo wakaamua kumpelekea chemba kwa mahojiano zaidi… Walipoanza kumuuliza taarifa iliwapate kuifahamu hio nchi ilipo Yule msafiri alianza kua mkali na kusema kua hiyo ilikua safari yake ya tatu hapo nchini japan kwa safari za kampuni anayofanyia kazi, pia amekua akifanya safari nchini humu kwa muda wa miaka mitano iliyopita. Msafiri alishangaa kwanini maofisa wanachelewa ku-Approve safari yake, lakini maofisa walipoulizia kwenye hiyo kampuni aliyosema ndio anakwenda kikazi walikataa kua hawamfahamu mtu huyo pia hata hiyo kampuni aliyotoka pia maofisa waligundua kua haijawahi kuwepo pia hata hotel aliyosema kafanya Resevation/booking walikaa kua hawamfahamu mtu huyo na hajachukua chumba hapo.

Msafiri huyo alikua anaongea kifaransa, kijapan na lugha nyingine nyingii. Kuongea kwake kijapani kidogo ilikua ni ushahidi kua hua anakuja nchini Japani. Lakini walipomuonyesha ramani ya dunia aonyeshe wapi nchi yake hiyo ya Tuared ilipo alishangaa kua haioni kwenye ramani, akaonyesha sehemu inayoitwa Andorra kua ndiko nchi yake hiyo ilikuwepo. Akasema tured ipo miaka zaidi ya elfu hivyo ingekuwepo kwenye ramani, akahitaji maofisa wamalizane na hilo swala lake aondoke kachoka kukaa kwenye chumba cha mahojiano. Hivyo maofisa uhamiaji wale walimtafutia chumba kwenye hotel iliyopo jirani na uwanja wa ndege, maafisa uhamiaji wawili walipangwa kulinda chumba chake hicho usiku kucha ili kesho yake aendelee kufanyiwa uchunguzi. Asubuhi kulipokucha walikuta Yule msafiri katoweka. Haikujulikana alipitia wapi maana kama ni dirisha la chumba cha hoteli lilikua juu kabisa hotelini pia mtaa ule ulikua bize muda wote hivyo angeonekana dirisha pia lilikua limefungwa. Hadithi ya msafiri huyo inaishia hapo maana hakuonekana tena mpaka leo na hakuna mtu aliyewahi kujua nchi hiyo ya tuared iko wapi japo wanhistoria mbali mbali kutoka japani walijaribu kufuatiia nchi hiyo uwepo wake miaka iliyopita.
 
Hvi ujue mnanichanganya, hii time travel unasafiri kiaje? Unatumia nini haswa? Maana mim nasoma ila sielewi!!!
 
How sio kweli..
Unakubali kwamba Sayansi kuna vitu haiwezi kuvidiriki ?

Wanasayansi wana uelewa mbaya sana juu ya kifo,wao wanahisi kifo ni tatizo hali ya kuwa ukweli ni kwamba kifo ni haki na ni katika maumbile.

Kutokujua kwao ya kuwa kifo sio tatizo,ndio kunawapelekea kujishughulisha na jambo ambalo hawalijui na huko ni kupoteza muda na kutumia rasilimali ya akili kinyume na inavyotakiwa na huu ni ujinga ulio pea.

Hakuna uhusiano kati ya kifo na magonjwa,wala kati ya kifo na ajali,bali kifo ni amri toka kwa Mola muumba,kwani unaweza kufa nje ya viwili hivyo na hizo zinabaki kuwa sababu. Huwezi kutoka kifua mbele leo hii ukajinadi kwa kusema "Bila kuumwa mtu huwezi kufa" au "Bila ajali mtu huwezi kufa". Huu ni uongo mkubwa sana.

Kwahiyo kama kweli wanasayansi wanashughulika na jambo la kifo basi wanapotez muda kama wanawafurahisha watu na kuwatia moyo basi wanazidanganya nafsi zao.
 
Unakubali kwamba Sayansi kuna vitu haiwezi kuvidiriki ?

Wanasayansi wana uelewa mbaya sana juu ya kifo,wao wanahisi kifo ni tatizo hali ya kuwa ukweli ni kwamba kifo ni haki na ni katika maumbile.

Kutokujua kwao ya kuwa kifo sio tatizo,ndio kunawapelekea kujishughulisha na jambo ambalo hawalijui na huko ni kupoteza muda na kutumia rasilimali ya akili kinyume na inavyotakiwa na huu ni ujinga ulio pea.

Hakuna uhusiano kati ya kifo na magonjwa,wala kati ya kifo na ajali,bali kifo ni amri toka kwa Mola muumba,kwani unaweza kufa nje ya viwili hivyo na hizo zinabaki kuwa sababu. Huwezi kutoka kifua mbele leo hii ukajinadi kwa kusema "Bila kuumwa mtu huwezi kufa" au "Bila ajali mtu huwezi kufa". Huu ni uongo mkubwa sana.

Kwahiyo kama kweli wanasayansi wanashughulika na jambo la kifo basi wanapotez muda kama wanawafurahisha watu na kuwatia moyo basi wanazidanganya nafsi zao.
So kwanini tunakufa..
 
So kwanini tunakufa..

Kifo ni hatua ya kuelekea maisha ya kaburini kisha ufufuo kisha malipo na mwisho kabisa maisha ya milele.

Kama ilivyo hatua ya kutambaa mtoto kisha atembee.

Inabidi pia uchunguze je ni kweli hao Wanasayansi wanashughulika na kutafuta tiba ya kifo ? Isiwe wanafurahisha tu sababu wameshawajua mnapenda story za kisayansi huku Ukweli wakiujua ya kuwa haiwezekani kwa jambo hilo,kama vile wanavyowafurahisha katika "Time Travel" au kama walivyowafurahisha katika "Safari ya mtu kwenda Mwezini". Muwe mnawahoji hao Wanasayansi msifanywe kama jalala lisilochagua taka.

Mimi nipo,ila mnatakiwa mjue ya kuwa kifo si tatizo wala kifo si Ugonjwa sasa vipi utafute tiba ? Wanasayansi huwa wanafikiri kitoto sana na ujuaji ukiwa mwingi kuna maarifa wananyimwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom