Jidondofila
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 286
- 105
Da Vinci nafaham Uzi huu sio wakidin.ila ninachotaka kuwaeleza hio Time travell ni Real ila haiwezi kuzuia Kifo...Mkuu unanishawishi niongelee kitu kinachoitwa Multi Universe.. sema nikiongea hapa tutazidi kuachana gizani. Matukio ya hvyo kuhusu picha zinapigwa afu intakea jambo lisilo la kawaida kwenye picha nadhani yako mengi.. baadhi yameelezwa kwenye nyuzi humu. Naomba tu siku Time Travelling ikiwa possible watu wote waliosoma uzi huu wawe hai
Fact:Hio kitu imeelezwa waziwazi na Abal Qassim kwenye safari yake ya miraji..
1,Aliwaona wanawake wengi wamejaa motoni. .jambo ambalo hata hukumu haijapita
2,Speed ya buraq na ngazi ya miraji kama iliwezekana kwake basi ni ishara tosha ipo cku kitaundwa chombo chenye 0mass na kitakua na speed kuliko mwanga..
3,Jawabu alilotoa swahaba wake alimuuliza Kati ya Mwanamume na Mwanamke nani anaenjoy zaidi kwenye tendo la jimai...Swahabu huyu alijibu ni Mwanamke..kisa chenyewe kipo hivi..
Swahaba huyu alikua kwenye darsa la Abal Qassim jioni ya siku ya Akhamis Akamuuliza Abal Qassim hivi..Ewe Mjumbe wa Allah naomba uujulishe Umma na Wanadam kwa ujumla Kati ya M/mke na M/mme ni nani Anafaidi zaidi kuliko mwenzie katika Tendo la jimai..Kabla hajatoa jawabu muda wa swala ukawa umeingia akamwambia atamjibu kesho baada ya swala ya yaumul jumaa..
Siku ya ijumaa ikaingia na Huyu swahaba aliposikia ile adhana ya mapemama akawahi mtoni ili akaoge na kuchukua udhu kwa ajili ya swala ya jumaa na shauku ya kupata jibu la swali lake.
Akafika mtoni akavua nguo zake na kujrusha mtoni...wakati anajiandaa kupiga mbizi mtoni alimsikia muadhiini ndio anasema Maneno ya Mwanzo kabisa yaani "Allahu akbar Allahu akbar..
Swahaba huyu alipoibuka hakuona nguo zake na wala sehemu alioibukia hakuwahi fika wala kuijua kabisa na cha kushangaza aliibuka akiwa bint kigori kabisaa..na alipotoka mtoni akakuta nguo za kike akajistiri..
Alipoanza kuelekea sehem za makazi akakutana na m/mme mmoja akamueleza yeye ni mgeni na hana makazi..
Kwa Urembo na uzuri aliokua nao yule mwanaume alimpenda na kuamua kumuoa..Swahabu huyu aliebadilika na kuwa binti Alishiriki tendo la ndoa na mumewe na katika vipindi tofauti na kumzalia watoto wawili...
Siku moja akapata hamu yakwenda mtoni kuoga na kuchota maji.akaenda mtoni akavua nguo zake na kujitumbukiza mtoni..
Alipoibuka akaibukia palepale alipoziacha nguo zake za kiume na akiwa mwanamume na cha kushangaza zaidi alimsikia muadhini yuleyule akimalizia Adhana kwa maneno ya Mwisho "Laila hailallah" .
Alivaa nguo zake na kuelekea msikitini..
Baada ya swala maswahaba walimkumbusha mtume juu swali aliloulizwa jana..na kabla hajajibu alimsimamisha Swahaba yuleyule aliemuuliza swali ili atoe jibu.
Alijibu ni Mwanamke na kisha Abal Qassim alikielezea kisa kizima kilichomkuta swahaba yule kama nilivyokihadithia.
4 Kwa suleiman bin Daudi hali hii ilitokea ya Time travell.Sulemain alikua na mwanafunzi wake ambae hakupenda kufa akiwa kijana..na kifo ni siri ya Allah Sw.basi yule kijana akamuomba suleiman amuombee afe akiwa mzee..suleiman akamuombea..kijana akafurah na kua na yakini za Dua za mtume ni Makubuul.
Siku ilifuata suleimani akiwa katka misafara yake na kijana wake Malaika mtoa roho akamfikia yule kijana.kijana aliogopa sana na akaamua kumfuata Suleiman na kumueleza kuna mtu amemjia anatisha sana.akamuelekeza mahala alipo.
Suleimani alupomuona akamwambia yule ni malaika mtoa roho.na amekuja kuichukua Roho yako.kijana akapagawa na kumuuliza kama dua yake haikukubaliwa.Suleimani akamwambia Asihofu dua yake ilkubaliwa.
Alichofanya suleimani ni kuuamrisha upepo umpeleke mashariki linapochomoza jua..sehemu hio kwa mwendo wa farasi mwenye kasi sana wakati huo angetumia miaka 50 kufika..na kuuamrisha upepo popote anapotaka apelekwe huyo kijana basi upepo umtii..
Upepo ule ulimsafirisha mpaka mashariki linapochomoza jua.kwa muda mfupi sana.alipofika hakukaa hata muda mrefu akamuona tena yule malaika mtoa roho..alipoona hivyo akauamrisha upepo umpeleke magharibi jua linapozama..ukafanya hivyo.ila alupofika msgharibi jua linapozama akamkuta pia malaika mtoa roho anamgojea..baada ya kuana hakuna pa kumkwepea mtoa roho akaamua kuuamrisha upepo umrudishe palepale alipoanzia safari yake akiwa na suleimani.alipofika kwanza alishangaa mno na alipowauliza wenyeji juu ya mfalme suleimani walimjibu kwa kumwambia mfalme huyo alikuwepo miaka 200 iliopita hali ya kua yeye bado kijana .
Muda mchache baadae malaika mtoa roho alimfikia na kuichukua roho yake..
Kisa hiki kina mafunzo mawili
1Time travel ipo na inatendeka ndani ya ulimwengu huu.
2.Pamoja na kuwepo kwake haitazuia kifo na hata utaratibu wa Qadari ya Allah sw.inawezekana kabisa watu kuishi kwenye past zao na Hata future zao..
Kinachofanyika ktk uweza wa Allah sw ni kun faya kun(kuwa na inakua),
Wanachofanya wanajitihada ( wanasayansi wa mambo haya) ni kupata kifaa maalumu kitakachothibitisha juu ya Nadharia hii ambayo imekuwepo enzi na enzi.