Time For Change: Sema "hapana" ngwe ya pili ya JK

Kikwete anaweza kuwa na mapungufu yake ila ni imani yangu kuwa yeye pekee si tatizo wala chanzo cha tatizo. Siasa, sera tekelezi na magenge pinzani ndani ya chama tawala ndio tatizo letu kubwa. Kwa jinsi CCM kusivyokuwa shwari kwa sasa hata hayati baba wa taifa angepata taabu kuongoza jahazi hili.

yep haina haja ya kusema sana abt our president , nchi yetu imeoza yote mfano anatowa mikopo watendaji wanakula sasa kikwete ndie msimamizi, kwa ufupi serikali yote imeoza inabidi kwanza sisi tubadilike na ndipo twawza kumchaguwa kiongozi bora , kama bado hatubadiliki hata kama tukichagua upinzani hakutakuwa na faida na uwozo utakuwa twice of that we have
 
- Bob ninasema hivi, ya Zitto sio ishu hapa the ishu ni politics of it, ni kwamba DR. Slaa ameshiriki kwenye vitendo vya kutoheshimu katiba ya chama chake mwenyewe, sasa eti unasema akipewa Jamhuri ataheshimu katiba ya Jamhuri? Are you serious?

- Bob ni mara ngapi hapa nimesema hivi haya maviongozi yote mafisadi, ukiyapekua pekua utakuta yalianza ufisadi toka siku nyingi sana, haiwezekani kwamba yalianza ufisadi baada ya Mwalimu kutoka uongozi au kutangulia mbele ya haki,

- Sasa eti unasema kwamba Dr. Slaaa akiwakamata mafisadi atawapeleka kwenye sheria na sio kwa hao wazee wa chama chake cha siasa wasioheshimu katiba ya chama chao wenyewe?

Pleaseee!

Respect.

Field Marshall Es!

Mkuu FMES siasa za ndani ya chama ni tofauti na siasa za kitaifa ama siasa za nje ya chama. Katiba hufuatwa na pia katiba hufanyiwa marekebisho pale inapoonekana kuna loopholes zinazoweza kupelekea maslahi either ya taifa ama ya chama kuwa hatarini....Katiba yetu mwenyewe unajuwa kwanza si tu kwamba inahitaji marekebisho,bali hata yale yaliyo sahihi hayafuatwi,la sivyo tusingekuwa hapa. Slaa yeye ni kinyume kabisa na yale yaliyotokea ya uvunjaji katiba na kutoifanyia marekebisho kulikosababisha ufisadi wote kushamiri...Ufisadi ambao amekuwa kinyume nao from the get go.

Ni rahisi kuunganisha dots kama ulivyofanya na kusema simply because of this,then that is possible,nimekupa mfano wa siasa za ndani na za nje ya chama hopefully zitatoa mwanga from where iam coming from.

Tutakuwa tunaplay politics tu kama tukihusisha issue ya CHADEMA moja kwa moja na uwezekano wa uvunjwaji wa katiba ya jamhuri ya mungano wa Tanzania bila kipima issue hii kwa mapana zaidi,je umeshawahi kujiuliza kuwa kama serikali ingetaka kumfungulia Slaa mashataka kwa uvunjaji wa katiba ya jamhuri ya muugano ingeshindwa? Tatizo ni ushahidi uliopo na wavunjaji wa katiba halisi ni mafisadi wenyewe,walioko kwenye power ndio wanaowalinda. Wote hao wakina Slaa ni kwasababu ya utu na ubinadamu na ndio maana inabidi waende na jinsi mambo yalivyo tu kwani ukweli ni kuwa huwezi kuwabadilsha watanzania ama kuibadilsha Tanzania kwa siku moja,na hivyo naamini hata wao wanajua tunahitaji mabadiliko ya kikatiba kabla ya kuanza kunyoosheana vidole kuhusu mambo ya chama na huku maslahi ya Taifa yakiwekwa kando kwa kutumia siasa zisizo na common sense...Kama ni maslahi a chama mbele je unadhani Zitto angeruhisiwa kujiunga kwenye kamati ya madini?CHADEMA walilalamikiwa sana hapa na kama unakumbuka mjadala ulikuwa mkali na sisi tukimwambia Zitto afikirie mara mbili mbili kwani inaweza kuja kum cost kisasa lakini mwishowe tukimpa go ahead kama kweli nia yake ya dhati ni kuyalinda maslahi yetu watanzania....Toka wakati ule na hadi sasa mengi ymeshoshatokea na ndio mana bado siwezi kumlaumu Slaa na kumvunia heshima yake anayostahili na kumfananisha na mafisadi simply because of this issue na Zitto humo CHADEMA.

Lengo la Dk Slaa kama ambavyo ameshawahi kuonyesha huko nyuma ni maslahi ya Taifa,na kwa jinsi mfumo wetu wa kisasa ulivyo,siasa za chama ni kama nganzi ya kufikia siasa za kitaifa,na ndio maana serikali inawekeza kwa nguvu zote kwenye chama,mara zote tumeshaona huko bungeni wakina Slaa wakipingana na kina Makamba kuhusiana na maslahi ya chama kuwekwa mbele zaidi,kwa hilo nabakisha imani yangu kwa Slaa kuwa malengo yake ni mazuri kwa mtanzania wa kawaida mwenye uchungu na nchi yake na mwenye kutaka kuona Mtanzania akipata mafaniko na kuishi vyema kwenye nchi yake mwenyewe...Tanzania ambayo bado tunaiota na ndio maana tunawapa sapoti wale wote wazalendo.
Peace.
 
Bwaaaana bwana! Hakuna chama chenye sera nzuri kama za CCM bwana we! Tatizo utekelezaji ZERO. Wala nchi hii haina matatizo ya kisiasa. Uongozi unahitajika ku-balance all conflicting interests, ndio maana ya uongozi, otherwise tusingehitaji sio? Uongozi sio kuchekacheka tu na watu saa zote. Mimi nasema SIDANGANYIKI katika hilo, uongozi wa juu sifuri.

Hivi hizo sera nzuri mnazosema ni zipi hizo. Mnazijua? Mmeziona? Mmezisoma? Mmezielewa?

Nijuanvyo mimi ni miaka mingi CCM imeacha kushughulika na sera. Kwao wao sera za serikali zinazotengenezwa na watu wasiojua hata imani za CCM ndio zinatosha...

Tafadhali mwenye sera mojawapo ya CCM iliyotoka ama hata kupitiwa upya kuanzia mwaka 1995 tulipopata serikali ya kwanza ya mfumo wa vyama vingi aiweke hapa tuione na kuipitia......

omarilyas
 
Niseme nini kisichojulikana? Alishinda kwa asilimia nyingi ya kura akijaza mioyo ya watanzania matumaini ya mwanzo mpya wa ujenzi wa taifa lao. Watu walitaraji mabadiliko. Walichopata badala yake ni mwendelezo wa sera ya uzembe, itikadi ya ufisadi na siasa za kubebana na ahadi za kuzugana. nchi yetu inastahili uongozi bora. Hatuitaji miaka mingine 5 ya viongozi walioshindwa. No 2nd term 4 kikwete. Yes i said it.

Tuwe na utaratibu wa kuhakikisha kiongozi anayestahili kuendelea kuwa madarakani kama Rais wa Tanzania amefikia vigezo vinavyoeleweka katika utendaji wake ambavyo vinamfanya astahili tena kugombea nafasi hiyo ya Urais, kama hakufikia vigezo mbali mbali katika utendaji wake basi hastahili kupewa awamu nyingine ya kuisarambaratisha nchi. Kikwete alitoa ahadi chungu nzima ambazo hata moja hajatimiza hivyo akae pembeni na kuwaachia wengine.
 
Mkuu FMES siasa za ndani ya chama ni tofauti na siasa za kitaifa ama siasa za nje ya chama. Katiba hufuatwa na pia katiba hufanyiwa marekebisho pale inapoonekana kuna loopholes zinazoweza kupelekea maslahi either ya taifa ama ya chama kuwa hatarini....Katiba yetu mwenyewe unajuwa kwanza si tu kwamba inahitaji marekebisho,bali hata yale yaliyo sahihi hayafuatwi,la sivyo tusingekuwa hapa. Slaa yeye ni kinyume kabisa na yale yaliyotokea ya uvunjaji katiba na kutoifanyia marekebisho kulikosababisha ufisadi wote kushamiri...Ufisadi ambao amekuwa kinyume nao from the get go.

Ni rahisi kuunganisha dots kama ulivyofanya na kusema simply because of this,then that is possible,nimekupa mfano wa siasa za ndani na za nje ya chama hopefully zitatoa mwanga from where iam coming from.

Tutakuwa tunaplay politics tu kama tukihusisha issue ya CHADEMA moja kwa moja na uwezekano wa uvunjwaji wa katiba ya jamhuri ya mungano wa Tanzania bila kipima issue hii kwa mapana zaidi,

je umeshawahi kujiuliza kuwa kama serikali ingetaka kumfungulia Slaa mashataka kwa uvunjaji wa katiba ya jamhuri ya muugano ingeshindwa? Tatizo ni ushahidi uliopo na wavunjaji wa katiba halisi ni mafisadi wenyewe,walioko kwenye power ndio wanaowalinda. Wote hao wakina Slaa ni kwasababu ya utu na ubinadamu na ndio maana inabidi waende na jinsi mambo yalivyo tu kwani ukweli ni kuwa huwezi kuwabadilsha watanzania ama kuibadilsha Tanzania kwa siku moja,na hivyo naamini hata wao wanajua tunahitaji mabadiliko ya kikatiba kabla ya kuanza kunyoosheana vidole kuhusu mambo ya chama na huku maslahi ya Taifa yakiwekwa kando kwa kutumia siasa zisizo na common sense...

Kama ni maslahi a chama mbele je unadhani Zitto angeruhisiwa kujiunga kwenye kamati ya madini?CHADEMA walilalamikiwa sana hapa na kama unakumbuka mjadala ulikuwa mkali na sisi tukimwambia Zitto afikirie mara mbili mbili kwani inaweza kuja kum cost kisasa lakini mwishowe tukimpa go ahead kama kweli nia yake ya dhati ni kuyalinda maslahi yetu watanzania..

..Toka wakati ule na hadi sasa mengi ymeshoshatokea na ndio mana bado siwezi kumlaumu Slaa na kumvunia heshima yake anayostahili na kumfananisha na mafisadi simply because of this issue na Zitto humo CHADEMA.

Lengo la Dk Slaa kama ambavyo ameshawahi kuonyesha huko nyuma ni maslahi ya Taifa,na kwa jinsi mfumo wetu wa kisasa ulivyo,siasa za chama ni kama nganzi ya kufikia siasa za kitaifa,na ndio maana serikali inawekeza kwa nguvu zote kwenye chama,mara zote tumeshaona huko bungeni wakina Slaa wakipingana na kina Makamba kuhusiana na maslahi ya chama kuwekwa mbele zaidi,kwa hilo nabakisha imani yangu kwa Slaa kuwa malengo yake ni mazuri kwa mtanzania wa kawaida mwenye uchungu na nchi yake na mwenye kutaka kuona Mtanzania akipata mafaniko na kuishi vyema kwenye nchi yake mwenyewe...Tanzania ambayo bado tunaiota na ndio maana tunawapa sapoti wale wote wazalendo.
Peace.

- Mkuu Mushi, heshima yako sana tatizo sio Zitto, isipokuwa ni kifo cha demokrasia na respect kwa katiba ya chama, asiyeheshimu katiba ya chama chake cha siasa hawezi kuheshimu katiba ya Jamhuri na hafai kwua rais wetu.

Respect.

FMEs!
 
Mara 3000000 nimpe KIKWETE kura yangu kuliko hawa wa fuatao
LIPUMBA-
MBOWE
Dr SLAA
ZITTO
Nitajieni mwingine mpinzani nani atafaa kupewa, saa nyingine tusiwe tunaropoka tuuuuu, na si kila anachosema Mzee mwanakijiji ni sawa...kiukweli TZ hatuna option...mwisho wasiku watakae mteuwa CCM ndo anachaguliwa......
 
Bwana COMO
hahahahahaha Mengi hafai hata kuwa rais, anawalipa wafanyakazi wake vibaya hawaonei hata uruma ndo ataweza kuwatumikia watanzania
Mengi kafanya ufisadi wake miaka hiyo, ajarudisha mpaka sasa hela alizokopa za walipa kodi
je mengi ni mpinzani?au ni CCM, anyway kama CCM wakimpitisha najua atashinda kama ni mpinzani hana sifa kabisaaaaaaaaa
anaudhaifu mkubwa na ni mfanyabiashara ambae anatamaaaaaa kubwa,
nahaya maneno ya Mengi kutaka kugombea yanakua sana, kama anampango huo mwambieni aache kabisaaaaaaaa,
 
Wakati ninaishi Sinza nilimfahamu sana Kikwete wakati akiwa Waziri wa fedha nikasema kuwa jamaa huyu hafai kuwa kiongozi. Mara nikasikia kuwa ndiye amiri jeshi mkuu wetu. I was right then, and I am still right know.

Tatizo ni kuwa kama upinzani ndio huo uliopo, basi ni wazi kuwa madaraka yote yataendelea kubaki mikononi mwa CCM. Swali la kujiuliza ni kuwa kama watu walioko CCM ndio hao tunaowafahamu, ni afadhali tudumu na Kikwete for another five years kwa vile naogopa sana taifa lisije likatumbukia mikononi mwa akina Lowasa au Makamba.
 
Niseme nini kisichojulikana? Alishinda kwa asilimia nyingi ya kura akijaza mioyo ya watanzania matumaini ya mwanzo mpya wa ujenzi wa taifa lao. Watu walitaraji mabadiliko. Walichopata badala yake ni mwendelezo wa sera ya uzembe, itikadi ya ufisadi na siasa za kubebana na ahadi za kuzugana. nchi yetu inastahili uongozi bora. Hatuitaji miaka mingine 5 ya viongozi walioshindwa. No 2nd term 4 kikwete. Yes i said it.
Mzee Mwanakijiji unajua kuna wakati watu wachache sana wanweza kuona hatari inayokuja mbele, na watu wachache zaidi wanaweza kuwashtua wenzao juu ya hiyo Tsunami inayokuja kama Nuhu alivyofanya wakati wa Gharika, kama Roti wakati wa Sodoma na Gomora.

Bw. George Bush Jr. alipokuwa anajiandaa kwenda kipindi cha pili cha Urais wake kuna Bw. Mmoja anaitwa Michael More (google) alimpinga vibaya sana, na aliwaonya wamarekani wasifanye kosa la kumchagua huyo mtu tena, alitengeneza Documentaries, alifanya interviews kwenye redio, Tv, Magazeti, aliandika makala na barua za wazi, lakini mwisho wa siku wamarekani wengi hawakumuelewa, wakamchagua tena George Bush.

Matokeo kila mtu ameyaona, sio tu ameiacha Marekani mahala pagumu bali ameiweka dunia nzima njia panda, inawayawaya kama mlevi, Dunia imekuwa ya mahangaiko, maisha yanapanda kila kukicha, hata Huko Kijijini kwangu nilikokuwa na uhakika angalau wa kunywa chai na magimbi au Viazi mambo yako tofauti.

Naamini ni watanzania wachache sana tunaokusikiliza, na wachache zaidi tunaokulewa, na watakuwa wachache zaidi watakao chukua hatua. Tumebaki na maswali yetu ya nani atabadili, kweli hakuna mtu kati ya watanzania wote tupatao mil.40 anayeweza kuongoza Vizuri kuliko JK?

Mimi nazidi kukupa Moyo, Mkuu nimekusikia, nakuelewa, nitachukua hatua, umekuwa Chachu kwangu umenichachusha. I am saying "No 2nd Term 4 JK"
 
matatizo yote ya ufisadi na ulaji rushwa kwa mara nyingi unaweza kukomeshwa au kukuzwa na kiongozi mwenyewe,
kwa Bwana JK, Uongozi ni zero kabisa hafai hata kuongoza kijiji, hivi kweli raisi hata siku moja huwezi kuonyesha sura ya seriousness na watu tukajua unachokisema ndicho unachokimaanisha
kama kipindi cha Mwanzo alishindwa kufanya la maana nadhani kw aterm ya pili ya lala salama ndio tusahahu kabisa
kwanza kuna mpango wa Bandari na Airport Bagamoyo, hiyo haikufanyika term ya kwanza kwa hiyo termu ya pili hatakuwa bize kujenga nyumbani nadhani visent vyote vya hii nchi vitaishia huko,
pili hii ni term ya lalasalama kwa mawaziri wengi yaani wanaweza wasirudi na kuwa mawaziri kwa hiyo ndio kitakuwa kipindi chao muafaka cha kuwekeza (kuchota), na kwa sababu mkuu wa kaya atakuwa analijua hilo bac itakuwa ni gombania goli
cha mwisho nadhani kitakuwa ni kipindi muhafaka cha kuandaa fedha kwa ajili ya kampeni ya mgombea atakayefuata, nadhani hapa ndipo ule ufisadi usio na ushahidi inabidi ufanyike, kama Mkapa alijitoa muhanga kwenye Kagoda kwa sababu ya JK, kwa nini yeye asijitoe muhanga kwa sababu ya Lowasa
 
Bwaaaana bwana! Hakuna chama chenye sera nzuri kama za CCM bwana we! Tatizo utekelezaji ZERO. Wala nchi hii haina matatizo ya kisiasa. Uongozi unahitajika ku-balance all conflicting interests, ndio maana ya uongozi, otherwise tusingehitaji sio? Uongozi sio kuchekacheka tu na watu saa zote. Mimi nasema SIDANGANYIKI katika hilo, uongozi wa juu sifuri.

I agree with your comment 1000%!! Tatizo tulilokuwanalo sio sera za chama cha mapinduzi bali watu waliokibaka chama hiki na kupindua malengo yake! Chama hakina uongozi thabiti na uliotukuka kama ilivyokuwa enzi ya Mwalimu.Nilipeleka swali lifuatalo wakati MUUNGWANA ALIPOSEMA TUMUULIZE kupitia TBC Television" JE UNADHANI CHENGE, LOWASSA, KARAMAGI, MSABAHA, ROSTAM, NA IDRIS RASHID WANGEKUWA BADO WANACHAMA WA CCM AU KUWA KATIKA AJIRA YA SERIKALI ENZI YA MWALIMU? Tido Mhando hakutoa fursa ya swali langu kujibiwa na nadhani halitajibiwa kamwe!! Kikwete angekuwa anaipenda nchi hii asingegombea tena bali angekubali yaishe na kukipa nafasi chama kuchagua mgombea mwingine!
 
Nimewasoma wote kwa umakini; miaka mitano inayoisha inatosha kabisa kwa kujaribu. Alitaka kuwa Rais, ameshakuwa Rais na anaweza kutia tiki bucket list yake.
 
Nimewasoma wote kwa umakini; miaka mitano inayoisha inatosha kabisa kwa kujaribu. Alitaka kuwa Rais, ameshakuwa Rais na anaweza kutia tiki bucket list yake.

Wasi wasi wangu ni hujuma za CCM ktk uchaguzi, kama hata Afghanistan wanaiba kura basi mimi sina imani na the preached western democracy.
 
Mwanakijiji,

Here is my theory>

A christian candidate (say Prof Mwandosya) rise to challenge JK inside CCM. With the current trend (growing religious mistrust) voting will be 80% based on religious lines within CCM Voters.....JK as incumbant wins and the loser moves to another party(not CUF)......Peoples Voting will be 90-95% based on religious devide.....then bang...its over....bye bye Tanzania and here comes WARLORD Rostam Aziz, WARLORD OLE SENDEKA, WARLORD LOWASA, WARLORD etc etc.

Guys, we are walking on a very thin line to bigbang......

Just a theory

omarilyas
 
Nipo New York sasa hivi. Cocacola moja ni dola tano. Hapo Dar es Salaam,ni nusu dola. Kwa hiyo,tunaweza kusema Rais Kikwete ni bora kuliko Rais Obama?
 
Niseme nini kisichojulikana? Alishinda kwa asilimia nyingi ya kura akijaza mioyo ya watanzania matumaini ya mwanzo mpya wa ujenzi wa taifa lao. Watu walitaraji mabadiliko. Walichopata badala yake ni mwendelezo wa sera ya uzembe, itikadi ya ufisadi na siasa za kubebana na ahadi za kuzugana. nchi yetu inastahili uongozi bora. Hatuitaji miaka mingine 5 ya viongozi walioshindwa. No 2nd term 4 kikwete. Yes i said it.
tupe mbadala bac
 
Hapo Mwandosya anaweza kufaa.Mwaka 1993 wakati Mzee Ruksa akiwa Rais,jamaa alijiuzulu ukatibu mkuu wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa Kikwete na wenzake walikuwa wamekubali waste za uranium toka USA zizikwe uvinza eti kwa kuwa deposit ya chumvi haipenyeshi uranium.USA kuna deposit kibao za chumvi kwa nini wasizizike kwao?Mshkaji aliona ni kinyume na taaluma yake akajiuzulu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom