Tim na Tom

Tim na Tom

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,029
Mida ya jioni jioni,watoto wawili,Tim naTom walikuwa wakicheza nje ya nyumba yao.Katika mchezo huo,Tim alichafuka usoni na Tom hakuchafuka.Mama yao aliwaita ndani ili wakalale.Kabla ya kwenda kulala,Tom alienda bombani kuosha uso wake lakini Tim hakwenda kunawa,alipanda kitandani na kuchapa usingizi.elezea,ni kwa nini Tom aliyekuwa msafi alienda kunawa uso na Tim aliyekuwa mchafu hakwenda kunawa?
 
hebu mwite kwanza huyo Tim aliyekuwa mchafu halafu akalala bila kunawa atujibu, maana yeye ndo atakuwa na sababu kwa kuwa ndiye mtenda

lol............
 
Tom alikua msafi wa nje, ila moyoni na rohoni alikua ni mchafu, hivyo alienda kutubu (kunawa) kabla ya kulala, wakati Tim alikua mchafu tu wa nje ila rohoni msafi kweli kweli............ Anyway, jst trying 2 think it loud and kivingine.............
 
Aaaaaah? Mimi siwezi changia,sijui ni fumbooo au methaliiiii au nahauuuuuu?
 
Nadhani sababu walikuwa wakicheza wote, Tom alipomwona Tim usoni kachafuka akajua na yeye pia kachafuka so akaenda kunawa.
japo hujamalizia,jibu lako ni sahihi.Tim na Tom ni mapacha,Tom alipomwona Tim mchafu akajua yeye naye ni mchafu akaenda kunawa na Tim naye alipomwona Tom msafi akajua naye ni msafi,akaenda zake kuchapa usingizi!
 
haukusema kama hawa wana ni mapacha katika post yako a kwanza........ anyway tumeelewa.
 
haukusema kama hawa wana ni mapacha katika post yako a kwanza........ anyway tumeelewa.
kugundua tu kwamba hawa watoto walikuwa mapacha ni sehemu ya jibu!
 
kugundua tu kwamba hawa watoto walikuwa mapacha ni sehemu ya jibu!

FUNDISHO:

Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi. Ni heri kuchukua tahadhali kabla ya hatari/ajali. Ukiona mwenzio kanyolewa wewe tia maji.
 
Tom alikuwa msafi kwa jadi - ndio maana (a) hakuchafuka ovyo (b) alinawa kabla ya kulala. Kinyume chake kwa TIM ambaye ana jadi ya kuwa mchafu
 
Tom alikuwa msafi kwa jadi - ndio maana (a) hakuchafuka ovyo (b) alinawa kabla ya kulala. Kinyume chake kwa TIM ambaye ana jadi ya kuwa mchafu
Hilo pia wazo!
 
msafi kwa jadi maaanake nini mtoto akiwa mdogo uchafu ndo sehemu yake...watoto mpaka wakaitwa TIM na TOM bado unataka uambiwe kuwa ni mapacha? Ofcoz swali limekaa kihesabu zaidi...yule alivyomwona mwenzie ni msafi naye akajihisi ni msafi pia na TOM naye kumuona TIM mchafu akajihisi kwa vyovyote atakua kachafuka coz walikua wanacheza wote DATZ A PERFECT ANS I LOVE IT
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom