First of all, Tik Tok ni ujinga na upuuzi kwa mwanaume. Second una idea gani na content gani? Tik Tok wanaoingiza pesa ni nje tu hasa wanawake kwa dancing, twerking, singing labda na upuuzi mwingine. na wanaume labda comedy za kujidharirisha. Na ndio maana nasema tiktok ni upuuzi sababu hakuna cha maana, watumiaji wengi ni wanawakenna watoto, na kutengeneza pesa kwa Mtanzania mwanaume ni almost impossible.
Njia bora ya kutengeneza pesa kwa Tanzania ni youtube angalau. Na uwe na content zenye akili either kwa kiswahili au kingeereza. Ila kama unajua kingeereza kile fluent basi inakuwa rahisi kidogo. Kwa mfano mimi naongea fluent American English. Nilijaribu kutengeneza short kuongelea topic fulani kwa kiingereza then nikapata views 1700 na 2 subscribers immediately, na views wangu wote wametokea USA, UK, Germany na India sema nikaachana nayo sababu sina muda. Na kitu kizuri kuhusu youtube ni kwamba kila unavyozidi kupost consistently ndio unavyozidi kupata more views sababu the youtube algorithm inakuwa ina soma aina ya content yako na kupush kwa watu sahihi.
Malipo ya youtube ni kwamba kutegemea na niche yako na traffic yako baada ya kukizi vigezo vya monetization ni sio chini ya 0.5$ mpaka 1$ kwa 1000 views kwa Tanzania, ila kama traffic yako ni kutoka nje kama mimi basi sio chini ya 1$ mpaka 6$ per 1000 views. Means kama ukiwa na bahati ya kupata views at least 100,000 per video means haukosi 300$ mpaka 600$ au kwa tsh ni laki 6 mpaka million 1.2 per video, sasa itategemea una upload video gani kwa siku na niche yako ni kubwa au maarufu kiasi gani. Mfano niche yangu watu wanaofanya kama mimi hawakosi views 500,000 mpaka 1,000,000 a day. It's fuking incredible. Na kizuri ni kwamba youtube hauitaji bando la kustream sijui na upuuzi gani. Jero tu inatosha kuupload video moja baada ya kuicompress kwa premier pro kazi imeisha.
So ushauri wangu ni kuwa na idea solid, then fanya youtube either kwa kiswahiliau kingeereza, na kama ukiwa na commitment na consistency basi utaona kitu. Ila ukweli ni kwamba Tik Tok ni upuuzi kiujumla.