Tigo wabuni wizi mpya!

Tigo wabuni wizi mpya!

Tangu jana nimejikuta nikibaguliwa kwenye mtandao huu wa tigo kwa kunipandishia gharama za muda wa vifurushi tofauti na wenzangu!

Vifurushi zamani vilikuwa vinaanzia 450 kuendelea lakini tangu juzi kifurushi cha chini tigo-tigo ni kuanzia 750.

Wakimaanisha kuwa kama nataka kuwasiliana ninunue vocha kuanzia 1000/= Tsh.

Nimewapigia wananijibu kua inatokana na matumizi yangu wakati mimi vocha na weka kwa wiki si zaidi ya mara tatu tena za 500!

Tena wakaongeza kua kama ninamalalamiko niende makao makuu yao!!

Hii imekua kwangu ni maajabu familia yangu na marafiki zangu wote vifurushi vyao bei ni ile ile ya zamani mimi tu ndo wameniona Dangote!

HUU NI UONEVU JAMANI!
ndio muwache kuwanakopakopa ovyo..
 
ndio muwache kuwanakopakopa ovyo..

Sijawahi kukopa tigo! Na hata kama mtu anakopa ndo umpandishie bei?

Mtu akikopa anamaanisha kapungukiwa sasa wewe unaona suluhisho ni kupandisha bei ili anunue??
 
Achana na mambo hayo...jiunge na vifurushi vya mwezi uokoe gharama zako
 
Kwa namna ulivyoeleza kiufundi haiwezekani wewe binafsi katika wateja wote ukawa unachajiwa tofauti.
 
Mpaka uwe fremanson kama hutaki utakimbia turn.
 
Back
Top Bottom