Tigo nani amewashauri hivyo?

Tigo nani amewashauri hivyo?

Aqua

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2012
Posts
1,657
Reaction score
1,237
Habari wadau wa jukwaa la Technologia,kuna jambo ambalo sijalipenda kuhusu mtandao wa tigo kwa sasa.Kutokana na eneo nililopo voda inasumbua nikaamua kujiunga tigo of course kwa muda tu.
Tatizo lilipo usipige simu au kutuma sms wakati salio lako limeisha au salio liishe wakati unaongea na simu.Kwa kweli tigo kukufahamisha kwamba salio lako halitoshi kupiga simu au kutuma sms watakutumia message chache tu kama sms 6 mpaka 15 kama utaonekana hutaki kurecharge haraka(au tunalazimishwa kuweka vocha kijanja?).Ambacho sijaelewa huko upande wa billing au kokote kunakohusika na sms hizo kuna nini?Je tatizo hili internal customers wa tigo halijawapata au hata hawajalisikia limeanza na external customers au ndiyo limepotezewa?Je ni haki kumsumbua mteja kwa sms zaidi ya moja zenye ujumbe uleule?Au simu yangu ni ya kichina?
 
Bro..i conquer with you..huwa wanaboa sn hasa wakishakutumia hiyo msg ukaifuta baasi we ni kama wanajua kuwa jamaa anafuta msg zetu bila kuzisoma..watakusumbua sn..kama umeishiwa salio usiombe ukakopa..aisee wanakusmbua mpaka saa nane usiku kwa msg kuwa unadaiwa hujalipa deni..I dont like Tigo sababu ya hii kitu yao..
 
sasa mnaongea nini? Humu ndani hamna tigo nendeni page yao ya facebook katoeni malalamiko au nendeni vituo vyao vya wateja mkawaface uso kwa uso muwaambie hivo ndo ujumbe utafika humu mtaongeaa wee mwisho wa siku no solution
 
Ku-deal na hiyo changamoto ni kuweka salio la kutosha na kukadiria mazungumzo, ukiweka buku ongea kwa interval ambayo lile buku litaisha na si kuongea utasema umeweka X-treme (kwanza hata status yako unaishusha unaonekana haupo organized)
 
Wakuu poleni kama na nyie yamewakuta! Mimi yamenikuta mara kadhaa, nilituma text kumbe salio lilikuwa halitoshi, nilitumiwa meseji hazipungui 50 zikinitaarifu kuwa salio halitoshi hivyo niongeze salio. Nikiwapigia simu wananipa maelezo yasiyo na msingi.
Pili, wana tabia ya ku-duplicate sms ukituma let say sms 5 wanaziongeza wanakuchaji hata 10 au zaidi.
Kwa kifupi wanakera na ni wezi.
 
Nafuu sipo mwenyewe. Huwa nakereka mpaka nabadilika rangi. Sijui huwa wanafikiria nini. The more I write, the more I vibrate kwa hasira. Ngoja niishie hapo.
 
ni kwel jamani hizi sms zimetulenga sisi wenye kipato cha chini inabidi tujipange
 
ina depend na simu unayotumia, kuna simu txt ikifail ina autoresend sasa kwa txt moja kufail wanatuma txt 1, ile txt itajiresend mara nying ndo kadri utakavopokea txt nyingi, solution wahi ifute outbox hautapata hzo txt zao!
 
hayo madai yenu mbona kwenye simu yangu siyaoni?
 
hayo madai yenu mbona kwenye simu yangu siyaoni?
piga simu salio likiwa dogo na ongea mpaka liishe utaona kimbembe chake, au subiri huna salio kabisa jifanye unatuma sms uone kimbembe chake au pokea sms zao kwa haraka kata simu kabla ya mlio uone kimbembe chake wanaboa niliwaambiaga kule fb wanitoelee hizo sms hawakusikia nikahama tigo
 
Mi nina wiki tatu sasa toka niwahame.. Natumia voda
 
tatizo halipo katika kuhama tatizo ni gharama utakazoingia kuwasiliana na wale uliowaacha nyuma kwa hiyo inabidi uwe na handset mbili ama dude la dual sim, au ufumbe macho na kutokuwajali walio nyuma yako. Hakuna mtandao usio na kasoro hapa nchini kwetu, ila Tigo ni baba ya wababaishaji wa mjini. Ahsanteni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom