tiGO ni wezi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tiGO ni wezi!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tanzania 1, Mar 17, 2008.

 1. Tanzania 1

  Tanzania 1 Senior Member

  #1
  Mar 17, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 197
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni mara ngapi unachunguza salio lako? Km uko ktk mtandao wa tiGo, angalia salio kabla ya kutuma SMS, kisha, km Delivery Report inachelewa au msg iko pending, angalia tena salio. Utagundua kuwa pesa zimeshakatwa hata kabla msg haijafika ulikokukusudia. Hii ina maana kuwa wanakata pesa hata km msg ina-fail.

  Je, ni SMS ngapi zina-fail kwa saa moja kila siku?

  Wakati mwingine salio linapokaribia kwisha, hasa unapopiga simu kwenda kwenye simu ya mtandao tofauti na tiGO, basi ile sauti "salio lako halitoshi ..." pia unailipia. Yaani, kile kiasi kidogo ulichobakiwa nacho pia kinaliwa!!

  Hii ndio tiGO, EXPRESS YOURSELF!!!
   
 2. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kumbuka, Cheap is Expensive! Au wenyewe as would like to call it, "affordable".
   
 3. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilishawahi kulalamika mimi Tigo wakasema wao wanachaji kutuma message na sio ku deliver message. Akafafanua CS kuwa kitendo cha kubonyeza send ina maana mitambo yao itatumika kujaribu kupeleka Txt yako. Sasa wewe usingetumia mitambo yao wasingekuchaji kwa kuwa hiyo nafasi angetumia mtu mwingine.

  Mimi simu ilijituma message kama 10 hivi yenyewe kwenye namba za ajabu wakachaji zote. Sikuruddshiwa hata senti.
   
 4. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #4
  Mar 17, 2008
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Network zote Bongo zinakamua hivo hivo mkuu wangu. Asikudanganye mtu; tiGO walikuwa hawakamui walipogundua wenzao wanakamua nao wakaanza kukandamiza haswaa.

  Habari ndo hiyo!
   
 5. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii siyo Tigo tu ni mitandao yote duniani.

  Unopotuma msg kabla ya kupata ujumbe Msg sent simu yako inafanya mawasiliano kupitia minara iliyopo karibu kuona kama msg inaweza kwenda na kama kuna fedha kwenye account yako.
  Ikipata comfirmation kwamba kuna hela then unapata ujumbe kwamba msg sent.

  Ujumbe wako utakaa kwenye server ukijaribu kumfikishia mhusika(kuna maximum time ambayo server itajaribu kudeliver huo ujumbe ukishindikana ndio unapata msg ya Msg Failed.

  Basically, kitendo cha wewe kutuma msg tayari umetumia huduma. Kutokufika kwa ujumbe ni tatizo la mpokeaji, either wrong number, not reachable, no network(at the entire msg max.time limit)n.k

  Hii unaweza kuona hata kwenye internet wakai wa kutuma email, ukishasend imetoka subiri failure delivery, baada ya server kuona haiwezi kufikisha ujumbe kwa mhusika.
   
 6. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nadhani kitu cha muhimu kwa wewe kufanya ilikuwa ni kuangalia na mitandao mengine inakuwaje...

  Nimetumia mitandao mingine yote ni kwamba kwa Voda na Celtel iko kama ambavyo umeelezea tiGo wanafanya. Huamini jaribu kutuma msg kwa namba ambayo haipo kwa kutumia mitandao hiyo na angalia salio kabla na baada ya kutuma hiyo message. Hata kama haitakuwa delivered lazima utakatwa pesa. Mitandao yote inatuibia!

  Je umewahi tumia simu za TTCL na ukagundua kama unapiga simu katika TTCL Mobile, unapoambiwa 'The Number you have Dialled is Busy' bado unakatwa pesa. Unasemaje juu ya hapo?
   
 7. RR

  RR JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Nimejaribu Celtel hawajakata, au wamejua nipo hapa JF nini?
   
 8. Kisura

  Kisura JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2008
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Speaking of TTCL, Kwanza, hivi tofauti ya hizi ni nini, mbali na kuwa moja unaweza kutumia mita kadhaa zaidi ya nyingine, haswa nia yako ilikuwa nini kuweka TTCL mobile? Which one is more affordable?.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mambo ya ujiko....
   
Loading...