Tigo Mnakera Kupita Kawaida

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,879
33,319
Wiki nzima mnatuma matangazo tangu asubuhi hadi usiku wa manane ni kama mmeajiri mtu anayemaliza kozi ya kutuma matangazo, anachoweza yeye ni kubonyeza bonyeza tu bila kujua athari anazosababisha kwa wateja
Haya ni baadhi ya matangazo mnayotumia wateja wenu wiki nzima kwa kujirudiarudia zaidi ya mara 10 kwa siku;
  1. BAHATI YA MTENDE imekuangukia .... UMOO kwenye DROO ya Tsh 2,000,000 na ya sehemu ya Tsh 6,200,000. Jiunge CHUKUA USHINDI sasa tuma neno STAA!
  2. Ndugu Mteja, sasa unaweza kupata huduma na bidhaa zetu mbalimbali katika duka letu lililopo KIHONDA MAGHOROFANI karibu na MAGHOROFA YA SUA.
  3. Ndugu Mteja, sasa unaweza kupata huduma na bidhaa zetu mbalimbali katika duka letu lililopo SOKO STREET-JUWATA na Hema la Tigo stendi ya zamani ya daladala
  4. Ndugu Mteja, sasa unaweza kupata huduma na bidhaa zetu mbalimbali katika duka letu lililopo KIHONDA MAGHOROFANI karibu na MAGHOROFA YA SUA.
  5. Furahia OFA ya hadi TSh 1000 kila siku unaponunua muda wa maongezi kuanzia TSh 500 au zaidi kupitia Tigo Pesa, ofa ni mara moja kwa siku. Piga*150*01#chagua 2
Je mna akili kweli?
Mnajua kiasi cha usumbufu mnaowasababishia wateja wenu?
Mnatambua kuwa kuna mitandao ya wenye akili wanaojua thamani ya mteja?
Je huu ujinga mnaupeleka mpaka kwa viongozi wa ngazi za juu?
Hamna mambo mengine ya msingi mnaweza kufanya?
Hapo ndipo uwezo wenu wa kufikiri umekomea?
Je ninyi wenyewe mnapokea meseji zenye usumbufu kama huo na mnajisikiaje?
Mbona wateja wanawasilisha kero nyingi mnashindwa kuzitatua mnaishia kuwapiga kalenda tu
 
Wakati unasajili line hakuna mkataba wa makubaliano mliosaini kwamba hautotumiwa matangazo

Kama unaona wasumbufu ungeanzisha mtandao wako mkuu
 
fanya kama hivi

dd.png
 
Back
Top Bottom