Je, wajua mwaka 2018, Tigo walilipishwa faini kwa kuchelewa kufunga laini ya mteja aliyeibiwa simu?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Moja ya kesi iliyowahi kufikishwa Kamati ya Malalamiko ya Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni kesi ya Suliman Shaban Suleiman dhidi ya MIC Tanzania Limited (Tigo). Katika kesi hii, mlalamikaji, Suleiman Shaban Suleiman, alikuwa mteja kampuni ya MIC Tanzania Limited. Huku MIC Tanzania Limited akiwa ni mtoa huduma za mawasiliano.

Suleiman alilalamika kwamba Tigo hawakuweza kuchukua hatua za haraka kusitisha huduma ya simu yake baada ya kutoa taarifa kuwa simu yake ilikuwa imeibwa tarehe 29 Julai 2017. Kuchelewa kwa Tigo kuchukua hatua ya kufunga laini yake mbali na yeye kuwataarifu Zaidi ya mara moja ilisababisha simu yake kutumiwa na wahalifu kufanya udanganyifu kwa familia yake ambao walituma zaidi ya elfu 50000 kwa tapeli.

Suleiman alilalamika kuwa utapeli huo ulishusha hadhi yake kwa kuwa yeye kama fundi umeme anategemea uaminifu kuvutia wateja. Na alidai fidia ya Tsh 25,000,000, japo alishindwa kusema kwanini anataka fidia ya kiasi hicho.

Tigo ambaye ni mlalamikiwa, alijitetea kuwa walichukua hatua za kuzima simu ya mlalamikaji ndani ya saa 24 baada ya taarifa, lakini hawakuwa na ushahidi wa kuthibitisha hilo. Pia, walisema kuwa suala hilo ni la jinai na lilipaswa kufikishwa kwa polisi.

Kamati ya Malalamiko ya Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania iliamua kwamba MIC Tanzania limited alishindwa kuchukua hatua za haraka kuzuia matumizi ya simu ya Suleiman mara baada ya kupokea taarifa, na hivyo alikuwa na jukumu la kutoa fidia kwa uharibifu na usumbufu alioupata. Kamati iliamuru MIC kumlipa Suleiman fidia ya Shilingi Milioni Mbili na Laki Tano (TZS 2,500,000) na kuandika barua ya kuomba radhi kwa mlalamikaji kwa usumbufu uliotokea.

Uamuzi huu ulitolewa na Kamati kwa kuzingatia hoja na ushahidi uliowasilishwa na pande zote mbili, na mlalamikaji aliruhusiwa kukata rufaa iwapo hajaridhika na uamuzi huo. Maamuzi haya yalifanyika dhidi ya lalamiko Na. TCRA/LAL/02/30/MEI/2018
 
Back
Top Bottom